Kuchagua njia ya uzuiaji mimba.

Kuchagua njia ya uzuiaji mimba.

Kuna aina nyingi za njia za uzuiaji mimba zinazopatikana. Lakini ni wewe binafsi utaamua njia utakayotumia. Ni wewe tu unaelewa kabisa mwili wako, mtindo wa maisha yako na mahitaji yako. Fanya kile kinachokufaa, sio kile mtu mwingine anakuambia ufanye. Tuko hapa kukupa ukweli na kukusaidia kuchagua moja kati ya yote yalioko.
Tulia, weka kikombe cha chai, na tuanze!

Mwongozo wa kuchagua njia ya uzuiaji mimba

Muda

IIkiwa bado mpango wako wa mimba uko mbali ( kama zaidi ya miaka 3)- Basi VipandikiziIUD ya shaba na IUD ya homoni  zitakufaa. Ufanisi wao unaweza enda miaka 3 hadi 12. Juu ya hayo, njia hizi zitakupa uwezo wa kurudisha rutuba wako punde tu unavyo zitoa.

Ikiwa hio ni muda mrefu sana, kuna njia za muda mfupi kama vile sindano ambayo huenda mwezi 1 hadi miezi 3.

Njia zingine zitakupa kinga kila mara moja ukizitumia, zingine zinahitaji kutayarishwa kabla ya ngono kama vile  diaframu, dawa za kuuwa mbegu za kiume, sponji, kofia ya kizazi na pete. Pia, kwenye kikundi hiki, kuna Pia, kwenye kikundi hiki, kuna kondomu za kike na za kiume. Kumbuka kutumia kondomu tofauti kila mara.

Homoni

Kuna taarifa nyingi za uongo kuhusu njia za uzuiaji mimba zenye homoni.- haswa kuhusu madhara zinazoletwa na matumizi zao. Hata hivyo, taarifa hizi hayajathibitishwa kisayansi, na kuna tafiti nyingi zimethibitisha usalama zao.

Pia kuna michanganyiko mbalimbali ya homoni. Hakuna moja inayofaa miili yote-Miili tofauti hupokea homoni kwa njia tofauti. Homoni nyingi huwa na projesteroni pekee au mchanganyiko wa projesteroni na estrojeni ambazo husaidia kudhibiti hedhi yako na kuzuia mimba. Kwa kweli, njia za uzuiaji mimba zenye homoni zinaweza kusaidia wanawake walio na uvimbe wa mji wa mimba ambayo husababisha maumivu makali na kutokwa damu nyingi. Njia zingine unaweza kuzingatia ni kama IUD ya homoni, vipandikizi, tembe au kiraka.

Ikiwa hukuona mazuri na njia moja, usiwe na fikra kwamba njia zote za homoni za uzuiaji mimba hazikufai. Kuna uwezekano kwamba njia ingine itafaana na mwili wako. Hata hivyo,ikiwa hupendelei njia za homoni; IUD ya shaba ni chaguo mbadala mzuri, kwani bali na kuwa na ufanisi, inakupa kinga kwa muda mrefu na haihitaji kuchunguzwa na daktari zaidi ya mara moja. Unaweza pia kutumia kondomu (ya kike na ya kiume).

Njia unayoweza kutumia peke yako au njia ambayo unahitaji kuenda kwa daktari?

Njia kama vile kiraka, tembe, kondomu, kofia ya kizazi, diaframu au dawa za kuuwa mbegu za kiume huwa zinapatikana mara nyingi kwenye maduka ya dawa na unaweza kuzitumia peke yako bila kuenda kwa daktari. Hata hivyo, ukichagua njia hizi, uwajibikaji wa matumizi sahihi ni wako mwenywewe. Kwa mfano, utahitaji kukumbuka kumeza tembe kila siku; na utahitaji kuvaa/ingiza kondumu vizuri na kuitumia kila mara ili ikupe matokeo!

Ikiwa unapata ugumu wa kufanya haya, basi pengine uzingatie njia ambayo haihitaji kazi nyingi na itakupa kinga kwa muda mrefu; IUD, vipandikizi au sindano. IUD (ya homoni na bila homoni) na vipandikizi vitahitaji kuingizwa na daktari; na sindano itahitaji matembezi kwa daktari kila miezi 1, 2 au 3 kulingana na ile umechagua.

Kinga ya muda mrufu

Ikiwa uko katika uhusiano wa muda mrefu na unafanya ngono mara nyingi, unashauriwa kutumia njia ambayo itakupa kinga siku zote kama vile tembe, sindano, vipandikizi au IUD.

Na ikiwa uhusiano zako ni za muda fupi fupi, unaweza kutumia “ njia za kuzuia manii” kama vile kondonu, diaframu na dawa za kuuwa mbegu za kiume. Njia hizi zina faida ya kuwa zinatumika tu wakati wa ngono.

Msaada wa dharura

Tembe za dharura za uzuiaji mimba ni chaguo bora ikiwa una shaka kwamba pengine hukutumia vizuri njia ya uzuiaji mimba ama ikiwa hukutumia kinga yoyote. Aina mbili za tembe ni tembe ya kumezwa ikiwa moja au tembe za kumezwa zikiwa mimbi, au mchanganyiko wa aina hizo mbili.

Kumbuka kuitumia punde iwezekanavyo ndani ya masaa 72 baada ya ngono kwasababu ufanisi wake hupungua kila siku inayopita.

Njia za dharura za uzuiaji mimba haziathiri rutuba, na mwili hauchelewi kurudisha rutuba baada ya kutumia tembe za dharura za uzuiaji mimba, kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni.

Pia IUD ya shaba inaweza kutumika kama njia ya dharura ya uzuiaji mimba. Inafanya kazi hadi siku 5 baada ya kufanya ngono bila kinga, na utapata kinga hadi miaka 12.

Uliza daktari wako

Usisite kumwuona daktari wako kwa ushari. Kulingana na historia yako ya kimatibabu na miaka yako, kuna uwezekano kuwa njia moja ni bora kwako kushinda njia ingine. Lakina pia fanya utafiti wako kuhusu njia za uzuiaji mimba, na upate ushauri wa daktari. Ikiwa itakusaidia, unaweza enda na rafiki wako au mwenzi akusaidie kuchagua!

Ikiwa unataka kujua zaidi kuhusu njia za uzuiaji mimba, tembelea findmymethod.org na ujaribu kurasa yetu ya kutafuta njia za uzuiaji mimba itakayo kufaa, na pia unaweza kuzilinganisha zikiwa pamoja.

Timu ya find my method wanapatikana kujibu maswali yako, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii: Facebook, Instagram na Twitter, au tutumie maswali yako kupitia barua pepe kwenye info@findmymethod.org.


References:

  • World Health Organization Department of Reproductive Health and Research (WHO/RHR) and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health/Center for Communication Programs (CCP), Knowledge for Health Project. Family Planning: A Global Handbook for Providers (2018 update). Baltimore and Geneva: CCP and WHO, 2018
  • Burkman R, Schlesselman JJ, Zieman M. Safety concerns and health benefits associated with oral contraception. American Journal of Obstetrics and Gynecology 2004, https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/15105794
  • Emergency contraception, World Health Organization, February, 2018, https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/emergency-contraception