Sponji ya uzuiaji mimba ni nini?
Sponji ya uzuiaji mimba, pia inayojulikana kama sponji ya uke ya kuzuia mimba, ni kipande mviringo cha kisponji plastiki nyeupe yenye unyevu ambacho kinaingizwa ndani ya uke kabla ya ngono.Ina upana wa sentimita 5 na kibonyo kidogo upande unaoyoingizwa ndani ya uke kabla ya ngono, na kitundu cha poliesta kilichoshonwa upande mwingine ya kusaidia kuitoa.
Unaweza kuiingiza mapema, hata saa 24 kabla ya ngono, na kila sponji inaweza kutumiwa mara moja tu(1).
Sponji ya uzuiaji mimba hufanyaje kazi?
Sponji inazuia mimba kwa njia mbili:
-Inazuia manii kuingia kwenye mji wa mimba kwa kuziba shingo ya kizazi. Kibonyo kilicho upande mmoja kinawekwa juu ya shingo ya kizazi kama kizuizi halisi kinacho zuia manii kufikia shingo ya kizazi.
-Inaendelea kuwachilia dawa ya kuua manii.
Sponji ya uzuiaji mimba hufanana aje?
Sponji ya uzuiaji mimba ina ufanisi wa kiasi gani?
Ufanisi wa sponji ya kuzuia mimba inategemea jinsi unavyoitumia. Hatari ya kushika mimba huongezeka ikiwa hautatumia sponji kila wakati unafanya ngono.
Sponji sio njia yenye ufanisi wa juu zaidi, hasa ikiwa tayari una mtoto. Kwa matumizi ya kawaida, ni watu 76 hadi 88 wanaoitumia wataweza kuzuia mimba.
Kwa wanawake ambao hawajazaa, kiwango cha kufeli kwa njia hii ni asilimia 16 kwa matumizi ya kawaida na asilimia 9 kwa matumizi kamili. Hii inamanisha kwamba kwa matumizi ya kawaida, ina ufanisi wa asilimia 84 na kwa matumizi kamilifu ina ufanisi wa asilimia 91 kwa kuzuia mimba.
Kwa wanawake ambao tayari wana watoto, kiwango cha kufeli kiko juu zaidi ikiwa asilimia 32 kwa matumizi ya kawaida na asilimia 20 kwa matumizi kamilifu. Hii inamaanisha kwamba na matumizi ya kawaida ina ufanisi wa 68 na kwa matumizi kamilifu ina ufanisi wa 80 kwa kuzuia mimba (2).
Ingawa imeainishwa kama mojawapo wa njia zenye ufanisi wa chini (hata chini zaidi ya dayaframu), ufanisi wa sponji ya kuzuia mimba inaongezeka ikitumiwa pamoja na kondomu (3).