Jinsi ya kutumia sponji ya kuzuia mimba

Jinsi ya kutumia sponji ya kuzuia mimba
Jinsi ya kutumia sponji ya kuzuia mimba

Unaweza kuingiza sponji mapema, hadi saa 24 kabla ya kufanya ngono. Kinga inaanza mara baada imeingizwa na inaenda hadi saa 24, licha ya mara ngapi utafanya ngono ya ukeni. Inachukua muda wa mazoezi kabla ujue kuitumia sahihi (4).

Jinsi ya kuingiza sponji ya kuzuia mimba

-Nawa mikono kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe kwa upepo.
-Weka sponji iwe yenye unyevu kwa kuimwagia angalau milimita 30 ya maji safi. Sponji inahitaji kulowana kabisa ili kuchochea dawa ya kuua manii. Finya sponji kwa upole kwa njia ambayo itasambaza maji kwa usawa.
-Ikiwa upande ulio na kibonyo umeangalia juu, kunja sponji katikati, ikiangalia juu.
-Telezesha sponji ndani kabisa kwa uke, hadi mahali vidole vyako vitafika. Sponji itajikunjua yenyewe na kufunika shingo ya kizazi ukiiwachilia.
-Telezesha kidole kwenye mzingo wa sponji kuhakikisha imeingia vizuri mahali pake. Unapaswa kuhisi kitundu cha nailoni upande wa chini wa sponji.
-Unapaswa kuingiza sponji mara moja pekee.Usitumie tena sponji ambayo umetoa ndani ya mwili wako. Ikiwa ndani, unaweza kufanya ngono mara nyingi unavyotaka.
-Mara iko ndani, uko tayari kufanya ngono!
-Wacha sponji ndani kwa angalau saa sita baaday ya ngono, lakini haipaswi kubaki ndani kwa zaidi ya saa 30 baada ya kuingizwa.

Jinsi ya kutoa sponji ya uzuiaji mimba

-Nawa mikono kwa sabuni na maji.
-Weka kidole ndani ya uke utafute kitundu.
-Mara ukishapata tundu, ivute sponji nje bila haraka na kwa upole.
-Tupa sponji kwenye pipa la takataka. Iweke mbali na watoto na wanyama.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...