Manufaa ya sponji ya kuzuia mimba
Manufaa ya kiafya
-Haina homoni. Sponji haina homoni, kwa hivyo utaweza kushika mimba mara unavyowacha kuitumia. Jikinge kwa njia nyingine ukiwacha kutumia sponji na hautaki kushika mimba.
-Unaweza itumia ukiwa unanyonyesha.
Manufaa kwa mtindo wa maisha
-Unaweza ingiza sponji hadi saa 24 mapema kabla ya ngono.
-Saizi moja itatosha wote kwa hivyo sio lazima iingizwe na mtoa huduma za afya.
-Ndani ya muda wa saa 24 ambamo inatoa kinga, unaweza kufanya ngono mara nyingi unavyotaka.
-Ni chaguo nzuri ikiwa haujali kushika mimba. Watu wengi hawatumii sponji sahihi, kwa hivyo wanawake hushika mimba. Ikiwa hautaki kushika mimba au kupata mtoto, zingatia kutumia njia tofauti.
-Wewe au mwenzi wako hamupaswi kuhisi sponji.
-Hauhitaji agizo la daktari.
Ni nini madhara ya sponji ya kuzuia mimba?
-Wanawake ambao wana mzio wa dawa zenye sulfa, polyurethane au dawa za kuua maani wanaweza kupata madhara.
-Inaweza kusababisha mwasho ukeni.
-Ikiwa spongi itawachwa ndani kwa zaidi ya saa 24, inaweza kusababisha harufu mbaya au mchozo.
Mabaya ya kutumia sponji ya kuzuia mimba
-Wanawake wengine wanapata ugumu wa kuingiza au kutoa sponji.
-Inahiti jitihada kubwa. Inahitaji nidhamu ya kibinafsi na mpangilio kwasababu unapaswa kukumbuka kuingiza sponji kila wakati unafanya ngono.
-Sio njia ya uzuiaji mimba yenye ufanisi sana, hasa kwa wanawake ambao tayari wamezaa.
-Unahitaji kuridhika na mwili wako. Ikiwa haupendi kuweka vidole vyako ndani ya uke wako, pengine sponji haikufai. Hata hivyo, ni kama tu kuweka tamponi, kwa hivyo ikiwa unaweza kufanya hivyo, basi unaweza kutumia sponji.
-Lazima iwachwe ndani kwa angalau saa sita baada ya ngono.
-Inaweza haribu starehe ya ngono.
-Ni ngumu kukumbuka kutumia wakati umelewa.
-Inaweza kufanya ngono uwe mkavu zaidi.
Je, sponji ya kuzuia mimba hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs)?
Sponji haitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kama klaimidia
Ni kwa hali gani haupaswi kutumia sponji?
-Kama umewahi kuugua kutokana na sumu mwilini inayoletwa na baktreia (toxic shock syndrome).
-Kama haijapita wiki sita tangu ujifungue.
-Kama una mzio wa salfa(sulfites).
-Kama uko kwenye hedhi.
-Kama umewahi kuwa na mzio wa nonoxynol-9 (kemikali inayotumiwa kwa dawa za kuua manii).
Pia unapaswa kuchua tahadhari kwa kupata ushauri wa mtoa huduma za afya kabla utumie sponji kama
-umepata mashauri ya kitiba kwamba usishike mimba;
-mimba imeharibika au umetoa mimba hivi karibuni; au
-una hali kwenye mji wa mimba au uke kama vile uke kujigawa mara mbili (vaginal septum) au mji wa mimba dhaifu (uterine prolapse), ambayo inaweza kuzuia sponji kufanya kazi (5).