Tembe za dharura za kuzuia mimba zina uwezo wa kuzuia mimba kabla itungwe. (Hii inamaanisha kwamba tembe za dharura za kuzuia mimba ni tofauti na tembe za kutoa mimba). Kulingana na unapoishi,unaweza kuwa na aina nyingi za tembe za kuzuia mimba za kuchagua. Aina nyingi hufanya kazi hadi siku 5 (masaa 120) baada ya kufanya ngono bila kinga, na zitakuwa na ufanisi wa juu ukizitumia punde baada ya ngono bila kinga.
Mifano ya tembe za dharura za kuzuia mimba:
Tembe za Ulipristal acetate. Aina hii mpya ya tembe za dharura za kuzuia mimba ni dozi ya tembe moja inayofanya kazi hadi siku 5 baada ya ngono bila kinga, tofauti na tembe zingine za dharura za kuzuia mimba, hazitapungua kwa ufanisi ndani ya hizo siku 5.
Tembe zilizo na Levonorgestrel: Lydia Postpil, Postinor 2, Norpill, Unwanted72, Nowill Pill, Plan B One-Step, Next Choice One Dose, Next Choice, My Way, After Pill, Levonorgestrel. Hizi zinaweza kupatikana kwenye duka la dawa ukiwa au usipokuwa na agizo la daktari, ikilingana na nchi unamoishi. Zinafanana na tembe zingine za kuzuia mimba lakini kwa dozi za juu zaidi. Zinaweza kufanya kazi hadi siku tano baada ya ngono bila kinga, lakini ufanisi unapungua kila siku. Ukitaka kutumia njia hii, unapaswa kuitumia punde iwezekanavyo baada ya ngono bila kinga.
IUD bila homoni. Hii ndio njia ya dharura yenye ufanisi wa juu kabisa. Enda kwa mtoaji akuingizie ndani ya siku 5 baada ya ngono bila kinga. Itapunguza uwezekano wa mimba kwa asilimia 99.9.
Njia ya Yuzpe. Unaweza kutumia tembe fulani za kawaida za kuzuia mimba kama tembe za dharura ukifuata hatua maalum. (Tazama sehemu ya “Jinsi ya kuzitumia” hapa chini) Haina ufanisi kama njia zingine. Itakuwa bora zaidi ukizitumia ndani ya siku 3 baada ya ngono bila kinga.