Kutumia tembe za dharura za uzuiaji mimba kunaweza kuleta madhara fulani ya kawaida, lakini kwa wanawake wengi, madhara hayaleti shida kwasababu yataisha baada ya saa 24 [8]..
Zinajumuisha:
-mabadiliko kwenye mzunguko wako wa hedhi (hedhi kuanza mapema au kuchelewa isivyotarajiwa, au kutokwa damu isiyotabirika kwa siku moja au mbili baada ya kumeza tembe ya dharura ya kuzuia mimba);
-ulaini wa matiti;
-tumbo kusumbua;
-kichefuchefu na kutapika ( wanawake huwa na madhara mengi-hasa kichefuchefu-wakitumia Yuzpe kushinda wakitumia tembe zingne za dharura za kuzuia mimba);
kizunguzungu;
-kuumwa kichwa; na
-uchovu.
Hakuna hatari zozote za kiafya zinazojulikana ambazo zinahusishwa na tembe za dharura za kuzuia mimba.
Kumbuka kwamba tembe za dharura za kuzuia mimba hazikukingi dhidi ya magonjwa ya zinaa.
Je, kuna madhara yoyote ya muda mrefu kutokana na matumizi ya tembe za dharura za kuzuia mimba? (ECPs)?
Madhara ya kawaida yanayotekea baada ya kutumia tembe ya dharura ya kuzuia mimba hayadhuru wala hayaendelei kwa muda mrefu. Yako sawa na yale watu hupata wakitumia tembe za kumezwa za kuzuia mimba, lakini hayako kali na yataisha haraka. Hii pia huwa tofauti kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine, na wanawake wengine hawapati madhara yoyote, kamwe.
Nitapata hedhi yangu baada ya muda gani baada ya kutumia tembe ya Morning-after?
Kutumia tembe ya Morning-after kwa kawaida itafanya hedhi yako ichelewe kwa hadi siku saba. Ni sawa kabisa ikiwa hedhi yako itakuja mapema au kuchelewa kidogo visivyo tarajiwa. Pia ni kawaida kutokwa damu kati ya hedhi zako (siku moja au mbili baada ya kumeza tembe).Ikiwa hautapata hedhi yako wiki 3-4 baada ya kutumia tembe ya morning-after, unapaswa kupima mimba. Jinsi tu ya kujua kama tembe zilifanya kazi ni kwa kupata hedhi zako.