Manufaa ya Kiafya
Chaguo zote za njia za uzuiaji mimba zina ufanisi wa juu. Tembe za dharura, zilizo na Ulipristal acetate au projestini pekee, zina ufanisi wa asilimia 99 wa kuzuia mimba, na tembe mchanganyo za kuzuia mimba zenye estrojeni na projestini zina ufanisi wa asilimia 98. Hata hivyo, njia unazoweza kutumia kabla au wakati wa ngono zina manufaa zaidi.
Tembe za Ulipristal acetate zinafanya kazi hadi siku tano baada ya ngono bila kinga na, tofauti na tembe zingine za dharura, ufanisi wao hautapungua ndani ya hizo siku tano.
Wanawake wanaotumia tembe za dharura za kuzuia mimba za Ulipristal acetate au levonorgestrel wana uwezo mdogo wa kupata kichefuchefu au kutapika ikilinganishwa na wanawake wanaotuimia tembe mchangano za dharura za kuzuia mimba.
Manufaa kwa mtindo wa maisha
Njia za dharura za kuzuia mimba ziko salama kwa wanawake wote ikijumuisha wasichana balehe na wanawake ambao hawawezi kutumia njia za kawaida za kuzuia mimba.
Unaweza kumeza tembe ya dharura ya kuzuia mimba bila kumwona mtoa matibabu kwanza.
Mchakato wa kumeza temba ya dharura ya kuzuia mimba unadhibitiwa na mwanamke.
Njia ya uzuiaji mimba ikifeli au haijatumika kamwe, njia ya dharura ya kuzuia mimba inapunguza haja ya kutoa mimba.
Unaweza kuweka tembe za dharura za kuzuia mimba karibu, ikiwa utazihitaji.
Tembe za dharura za kuzuia mimba zinakupa amani wa moyo baada ya ngono bila kinga au ikiwa njia ya uzuiaji mimba imefeli.
Haicheleweshi kurudi kwa urutubisho wa kizazi. Utaweza kushika mimba haraka sana baada ya kumeza tembe ya dharura ya kuzuia mimba.
Je, tembe za dharura za kuzuia mimba ndio njia pekee ya dharura ya kuzuia mimba?
Chaguo kadhaa zinaweza kutumika kama njia ya dharura ya kuzuia mimba. Kando ya tembe za dharura za kuzuia mimba ,IUD ya shaba inazingatiwa kama moja ya njia za dharura ya uzuiaji mimba yenye ufanisi wa juu. Juu ya hayo, inawapa wanawake fursa ya kuanza kutumia njia kawaida ya uzuiaji mimba. [6].
Ni mara ngapi unaweza kumeza tembe ya Morning-after?
Matumizi ya mara kwa mara ya tembe ya Morning-after haidhuru afya. Kinyume na jinisi inavyo aminiwa, tembe hizi zinaweza kumezwa mara nyingi inavyohitajika, hata zaidi ya mara moja ndani ya mzunguko moja wa hedhi. Hata hivyo, hauwezi kuzitegemea kikamilifu ziwe na ufanisi wa kuzuia mimba, kwasababu ufanisi wao unategemea wakati wako wa kupevuka kwa yai.Juu ya hayo, matumizi ya mara kwa mara yanaweza kukuletea madhara zaidi. Ukijipata unahitaji kutumia tembe hizi mara kwa mara, unashauriwa kuzingatia kutumia njia ya uzuiaji mimba ya muda mrefu.
Tembe ya Morning-after itakupa kinga kwa muda gani?
Tembe ya Morning after imeundwa kwa njia maalum iwe na ufanisi wa kuzuia mimba kwa siku 5-7 pekee. Ukijipata unaitumia mara kwa mara, unapswa kuzingatia kutumia njia ya kawaida ya kuzuia mimba. Hii itakusaidia kupata kinga yenye ufanisi dhidi ya mimba.