Tembe za dharura za kuzuia mimba ni salama na zina ufanisi kwa wanawake wote. Hii inajumuisha wanawake ambao, kwa sababu yoyote ile, hawawezi kutumia njia za uzuiaji mimba zenye homoni. Kwa sababu tembe za dharura za kuzuia mimba zinatumika kuzuia mimba kwa muda mfupi, hakuna hali za kitiba zinazoweza kuzifanya zisiwe salama kwa mwanamke yeyote.
Hata hivyo, kuna hali chache ambamo tembe ya dharura huenda haitakuwa chaguo bora:
-kwa wanawake wanaotumia glucocorticoids za njia ya mdomo ili kudhibiti pumu kali, tembe za dharura za kuzuia mimba Ulipristal acetate hazipendekezwi;
-ikiwa mwanamke ametumia projestojeni ndani ya siku saba kabla ya kutumia tembe ya dharura ya Ulipristal acetate,ufanisi wake huweza kupungua; na
-kwa wanawake walio na BMI ya juu au uzito wa mwili, kuna uwezo kuwa tembe za dharura za kuzuia mimba za kumeza, hasa LNG-EC, zinaweza kuwa na ufanisi wa chini [9].
Wakati tembe za dharura za kuzuia mimba sio chaguo bora, mtoa matibabu wako kuna uwezo atapendekeza IUD bila homoni kama njia ya dharura ya kuzuia mimba.
Wakati matumizi ya tembe za dharura za kuzuia mimba hayafai
Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba
Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.
Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.
Compare with similar Contraceptive Methods
Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.
Give a try to our Contraceptive Tool
In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page
Need to learn more things?
Read about other Contraceptive methods
Our Monthly Top Articles
Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo
Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...
Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume
Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...
Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba
Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...