Njia za dharura za uzuiaji mimba tembe za Asubuhi ya kufuata

Njia za dharura za uzuiaji mimba tembe za Asubuhi ya kufuata
Njia za dharura za uzuiaji mimba tembe za Asubuhi ya kufuata

Tembe za Dharura za Kuzuia Mimba ni nini?

Tembe za Dharura za Kuzuia Mimba (ECPs) pia zinajulikana kama Morning-after pill, Plan B au njia ya uzuiaji mimba baada ya ngono, ni tembe zinazosaidia mwanamke kuepuka kushika mimba baada ya kufanya ngono bila kujikinga na aina yoyote ya njia ya uzuiaji mimba au ikiwa njia ya uzuiaji mimba haikufanya kazi. Kulingana na unapoishi, unaweza kuwa na aina kadhaa ya ECPs ya kuchagua. Aina nyingi hufanya kazi hadi siku tano (au saa 120) baada ya kufanya ngono bila kinga, lakini zinakuwa na ufanisi wa juu zikichukuliwa punde iwezekanavyo. Kulingana na mahali ulipo, unaweza kununua tembe za dharura kwa dozi ya tembe moja au dozi ya tembe mbili. Dozi ya tembe mbili na dozi ya tembe moja zote zina ufanisi sawa.

Tembe za Dharura za kuzuia mimba hufanya aje kazi?

Tembe ya dharura ya kuzuia mimba imeundwa kuzuia mimba baada ya ngono bila kinga; kwa kuchelewesha kupevuka kwa yai ama kusimamisha upandikizaji wa yai lililorutubishwa. Inakuja kwa muundo wa tembe za dharura za uzuiaji mimba ama kama kifaa cha ndani ya mji wa mimba.
Tembe za Dharura za Kuzuia Mimba (ECPs) zinafanya kazi tu kwa kuzuia yai kuwachiliwa kutoka kwa ovari (kupevuka kwa yai). Haziwezi kufanya kazi kama mimba tayari imetungwa. Hii inamaanisha kwamba zikotofauti kabisa na tembe za kutoa mimba. ECP haiwezi kusimamisha mimba inayomea au kuharibi kiinitete [1].

Vifaa vya ndani ya mji wa mimba (IUDs) kama njia ya dharura ya kuzuia mimba hufanya kazi kwa kuzuia upandikizaji. Ikiwa unahitaji njia ya dharura ya uzuiaji mimba na unataka suluhu yenye ufanisi na ya kudumu muda mrefu, IUD ya shaba ndio njia yenye ufanisi zaidi. Njia hii ya dharura ya kuzuia mimba inaweza kuingizwa kwenye mji wa mimba hadi siku tano baada ya kufanya ngono bila kinga. Baadaye, utakuwa na njia ya uzuiaji mimba rahisi kutumia na yenye ufanisi wa juu kwa hadi miaka 12.

Kuna aina tatu za tembe za dharura za kuzuia mimba.

Tembe za Ulipristal acetate (UPA)

Inatumika ikiwa dozi moja ya tembe moja. Njia hii mpya ya tembe ya dharura ya kuzuia mimba ni dozi ya tembe moja ambayo inafanya kazi hadi siku tano baada ya ngono bila kinga, na tofauti na tembe za dharura zingine (EC), haitapunguza ufanisi wake ndani ya hizo siku tano. Ulipristal inapatikana katika nchi nyingi, kwa maagizo ya daktari au bila.

Tembe za Levonorgestrel.

Inatumika kama dozi moja au dozi mbili zinayomezwa moja kwanza na ingine baada ya saa 12. Mifano ni kama Lydia Postpil, Postinor 2, Norpill, Unwanted72, Nowill Pill, Plan B One-Step, Next Choice One Dose, Next Choice, My Way, After Pill, na Levonorgestrel. Kulingana na nchi unamoishi, hizi zinaweza kupatikana kwa duka la dawa na au bila maagizo ya daktari. Ziko sawa na tembe zingine za kuzuia mimba, lakini zina viwango vya juu vya homoni.

Tembe mchanganyo za uzuiaji mimba za njia ya mdomo

Zina estrojeni na projestini-norgestrel, levonorgestrel au norethindrone (pia inayoitwa norethisterone). Aina zingine za njia za uzuiaji mimba za kawaida zinaweza kutumika kama njia za dharura za uzuiaji mimba.Ukitumia njia hii, ambayo inaitwa Yuzpe regimen, utahitaji kumeza tembe kwa dozi mbili, saa 12 kati yao. Na inafanya tu na chapa maalum ya tembe. Pia haina ufanisi kama tembe zingine za dharura za kuzuia mimba. Inafanya vizuri sana hadi siku tatu baada ya ngono bila kinga [2].

Tembe za dharura za kuzuia mimba ziko salama kwa mwanamke au msichana yeyote, hata wale ambao hawawezi kutumia njia ya uzuiaji mimba yenye homoni. Zinaweza kutumika kwa hali kadhaa, ikijumuisha:
1.wakati hakuna njia yoyote ya uzuiaji mimba ilitumika wakati wa ngono. Ikiwa haukutumia kinga yoyote wakati wa ngono na hautaki kushika mimba, hakikisha umetumia njia ya dharura ya kuzuia mimba ndani ya siku tano baada ya kufanya ngono bila kinga.
2. baada ya kushambuliwa kingono (ikiwa umenajisiwa au umefanya ngono na mtu ambaye alikataa kutumia aina yoyote ya kinga ya njia ya kuzuia mimba)

3. ikiwa kuna wasiwasi kwamba njia ya uzuiaji mimba inayotumika huenda ilifeli kwa ajili ya matumizi yasiyo sahihi au yasiyofaa, kama vile

-matumizi yasiyo sahihi ya kondomu, kupasuka au kuteleza;

-kuchomoa uume haukufaulu;

-ikiwa kifaa cha ndani ya mji wa mimba (IUD) au kipandikizi cha kuzuia mimba kilitoka;

-kutohesabu vizuri siku salama au kutotumia njia za kizuizi wakati wa siku za hatari;

-ikiwa umechelewa kwa zaidi ya siku saba kupata sindano mchanganyo ya kuzuia mimba;

-ikiwa umechelewa kwa zaidi ya wiki nne kupata sindano ya DMPA yenye projestini pekee (ya miezi mitatu) ya kuzuia mimba;

-ikiwa umechelewa kwa zaidi ya wiki mbili kupata sindano ya NET-EN yenye projestini pekee (ya miezi miwili) ya kuzuia mimba;

-ikiwa umechelewa kwa zaidi ya saa tatu ya saa yako ya kawaida ya kumeza tembe yenye projestini pekee (tembe ndogo) au ikiwa imepita saa 27 tangu umeze tembe ya mwisho; na

-ikiwa ulikosa kumeza tembe mchanganyo ya kuzuia mimba kwa siku tatu mfululizo au ikiwa umechelewa kwa siku tatu kumeza tembe wakati wa wiki ya kwanza ya mzunguko [3].

Tembe za Dharura za kuzuia mimba zinafanana aje?

Image

Tembe za Dharura za kuzuia mimba zinatumika aje?

Mara wewe au mtoa matibabu wako mmebaini kuwa hali yako inahitaji utumie njia ya dharura ya kuzuia mimba, unaweza kumeza tembe mara hio hio. Tembe inaweza kupatikana kwenye kituo cha afya au katika duka nyingi za dawa karibu nawewe bila maagizo ya daktari.
Ukinunua pakiti ya tembe moja, yote unapaswa kufanya ni kuimeza na maji na hio ndio mwisho wa mchakato huo.
Ukinunua pakiti ya tembe mbili, utahitaji kumeza tembe ya kwanza, ngoja saa 12 zipite, kisha meza tembe ya pili.

Ni lini napaswa kumeza tembe ya Morning-after?

kwa ufanisi wa juu, aina zote za tembe za dharura za kuzuia mimba zinapaswa kumezwa punde iwezekanavyo.tembe za dharuza za Ulipristal acetate zinaweza kuwa na ufanisi wa kuzuia mimba kushinda tembe zingine za dharura za kuzuia mimba, hata kama ni kati ya saa 72 na 120 baada ya ngono bila kinga. Ingawa tembe za darura za uzuiaji mimba za levonorgestrel pia zina ufanisi sawa na zinaweza kufanya kazi hadi kufikia siku tano baada ya ngono bila kinga, ufanisi wake unapungua kila siku. Ukitaka kutumia njia hii, unapaswa kuitumia punde iwezekanavyo baada ya ngono bila kinga.

Vidokezo muhimu

Kumbuka: Tumia tembe ya dharura punde iwezekanavyo baada ya ngono bila kinga. Ni bora ukiitumia punde iwezekanavyo.- ndani ya saa 24 hadi siku 3 ni bora zaidi. Njia ya dharura ya uzuiaji mimba bado itapunguza uwezekano wa mimba hadi kufikia siku ya tano.
Kila mara, hakikisha una tembe za dharura za kuzuia mimba karibu.Njia za dharura za kuzuia mimba zina ufanisi wa juu ukizimeza punde iwezekanavyo. Kwa hivyo, sio wazo mbaya kuweka pakiti ya tembe za dharura za kuzuia mimba, ikiwa itahitajika.
Ukimeza tembe ya dharura ya Ulipristal acetate wakati unanyonyesha, inapendekezwa kwamba usimnyonyeshe mtoto wako. Badala yeke, kamua maziwa na uitupe kwa siku saba baada ya kumeza tembe.
Madhara ambayo unaweza kupata huenda haitafanana na madhara ya mtu mwingine. Kila mtu ako tofauti.

Ni kwa muda gani tembe ya Morning-after huchelewesha kupevuka kwa yai?

Tembe ya Morning-after inazuia au kuchelewesha kupevuka kwa yai kwa siku 5-7. Hii inaipa manii ndani ya mwili wa mwanamke muda wa kutosha wa kukufa. Manii inaweza kuishi ndani ya mfumo wa uke hadi siku 5. Ikiwa yai limewachiliwa tayari, tembe ya dharura ya kuzuia mimba haiwezi kuzuia upandikizaji au kuharibu mimba iliyotungwa tayari.

Je tembe ya Morning-after itafanya kazi ikiwa tayari kupevuka kwa yai kumefanyika?

Hapana.Tembe ya Morning-after hufanya kazi kwa kuchelewesha kupevuka kwa yai. Ikiwa tayari kupevuka kwa yai kumekamilika, bado unaweza kushika mimba, hata baada ya kutumia tembe. Njia bora ya uzuiaji mimba ya kutumia wakati wa kupevuka kwa yai au baada ya kupevuka kwa yai ni IUD bila homoni (ya shaba) kwasababu inaweza kuzuia upandikizaji kufanyika. Hata hivyo, utahitaji kuweka miadi na mtoa matibabu ili uingiziwe IUD bila homoni. Itafanya kazi ikiwa itaingizwa ndani ya siku tano baada ya ngono bila kinga, kwa kupunguza uwezo wako wa kushika mimba kwa asilimia 99.9. [5].

Contraception Quiz

Not sure on the method? - Take our dynamic Contraception Quiz.
When it comes to sex, protection is as important as pleasure. But what should one do to start their safe sex journey? Answer some simple questions and based on the responses, we will recommend the next steps.

Take the quiz
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...