Kipandikizi cha kuzuia mimba ni nini?
Kipandikizi cha kuzuia mimba, pia inayojilikana kama kipandikizi cha kupanga uzazi ni njia ya uzuiaji mimba ya muda mrefu,inayoweza kugeuzwa athari yake na yenye homoni ambayo ina umbo wa vijiti vidogo vyebamba ambavyo vinaingizwa kwenye sehemu ya juu ya mkono. Vijiti hivi huachilia homoni ambayo huzuia mimba kwa miaka 3 hadi 5.
Kipandikizi cha kuzuia mimba ni kubwa kiasi gani?
Kipandikizi cha kuzuia mimba huja kama vijiti vidogo nyumbufu vya plastiki au kapsuli (inatoshana na njiti) inayoingizwa chini ya ngozi ya sehemu ya juu ya mkono. Mwanamke hawezi kuanzisha au kukomesha matumizi ya kipandikizi cha kuzuia mimba mwenyewe. Vipandikizi vinaweza tu kuingizwa au kutolewa na mtoa matibabu aliyehitimu.
Je, kipandikizi cha kuzuia mimba hufanya aje kazi?
Kipandikizi cha kuzuia mimba huachilia homoni ya projestini, ambayo hufanana na projestini inayopatikana kwa mwili wa mwanamke. Inafanya kwa:
- Kuzuia ovari kuwachilia yai kufanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito na kuzuia manii kufikia yai [1].
Kipandikizi cha kuzuia mimba hudumu kwa muda gani?
Kipandikizi cha kuzuia mimba kinaweza kuzuia mimba hadi miaka tano;na kuna aina tofauti:
- Implanon, au Nexplanon, ni kijiti kimoja kilicho na etonogestrel. Ina ufanisi wa miaka tatu,ingawa tafiti zimeonyesha kwamba inaweza kudumu hadi miaka tano (inaweza kuonekana kwa X-ray).
- Jadelle ni vijiti viwili vilivyo na levonorgestrel. Ina ufanisi hadi miaka tano.
- Levoplant-pia inajulikana kama sino-implant-inakuja kwa umbo wa vijiti viwili vilivyo na levonorgestrel. Ina ufanisi wa miaka tatu [2].
Kipandikizi cha kuzuia mimba kina ufanisi wa kiasi gani?
Inatoa kinga ya asilimia 99 dhidi ya mimba na hatari zingine husika, ikiwemo mimba nje ya mji wa mimba. Hata hivyo, kuna dawa zinaweza kupunguza ufanisi wa kipandikizi. Ikiwa unazingatia kutumia kipandikizi cha kuzuia mimba, kumbuka kutaja dawa zozote unazotumia kwa mtoa matibabu wako.