Kupata kipandikizi kunahitaji mchakato mdogo wa upasuaji ambayo hufanywa na mtoa matibabu wako. Wakati bora zaidi wa kuingiziwa kipandikizi ni ndani ya siku tano za kwanza za hedhi yako kwasababu wakati huo utakuwa na hakika kabisa kwamba hauna mimba. Hata hivyo, inaweza kuingizwa wakati wowote ingine, bora hakuna uwezo kwamba una mimba.
Kuanza mchakato huu, mtoa matibabu atakuuliza maswali kadhaa ambayo yatasaida kubaini ikiwa unafaa kutumia kipandikizi.Pia unaweza kufanyiwa vipimo vya kimatibabu. Mara imebainiwa kwamba unaweza kutumia njia hii ya uzuiaji mimba, hatua ya kufuata itakuwa kufa ganzi eneo ndogo ya mkono wa juu kwa kutumia dawa ya kutuliza maumivu.Kifaa cha kuweka kisha kitatumika kuingiza vijiti au kapsuli chini ya ngozi yako.[3].
Wategenezaji wa Nexaplanon wanashauri kwamba , mara tu kipandikizi kimeingizwa, wewe na mtoa matibabu mnapaswa kuthibiti kwamba kipandikizi kiko kwenye mkono wako kwa kukitafuta kwa kugusa. Juu ya hiyo, ikiwa wakati wowote hautakigusa kwenye mkono wako, unapaswa kuanza kutumia njia ya uzuiaji mimba bila homoni mara hio hio ili kuepuka mimba na utembelee mtoa matibabu wako haraka iwezekanavyo, kuthibitisha kwamba kipandikizi kiko mahali pake.
Mara imebainika kwamba kipandikizi kiko pahali pake, mtoa matibabu atafunga sehemu aliyopasua kwa pamba za kinga kisha aifunike na bandeji la shinikizo ili kuounguza damu na michibuko yoyote.
Ni nini napaswa kutarajia baada ya uingizaji wa kipandikizi cha kuzuia mimba?
Hakuna uchungu utahisi wakati wa uingizaji wa kipandikizi. Wanawake wengi wameripoti tu kuhisi mchuno wakati wanadungwa sindano ya ganzi. Hata hivyo, mara dawa ya kutuliza maumivu inaisha nguvu, unaweza kupata mchubuko mdogo eneo lililo chanjwa na uchungu kwa mkono kwa siku chache za kufuata. Hizi hazihitaji matibabu yoyote na zitapungua ndani ya siku chache. Mtoa matibabu atakushauri uwache eneo lililo chanjwa likiwa limekauka kwa angalau siku mbili. Bandeji inaweza kutolewa baada ya saa 24, na pamba za kinda ziondolewe ndani ya siku tatu au tano, au baada ya ngozi kupona [4].
Kipandikizi cha kuzuia mimba huwa na ufanisi muda gani baada ya uingizaji?
Ikiwa utaingiziwa kipandikizi cha kuzuia mimba ndani ya siku tano za kwanza za hedhi yako, mara hio hio utapata kinga dhidi ya mimba. Ikiwa siku hizo tano zimepita, utahitaji kutumia njia ya uzuiaji mimba ya ziada kama; kondomu ya nje au ya ndani, diaframu, au sponji kwa siku saba za kufuata. Ikiwa utafanya ngono bila kinga ndani ya siku hizi saba, unapaswa kutumia njia za dharura za kukinga mimba [6].
Je, unaweza kukunywa pombe baada ya kuingiziwa kipandikizi cha kuzuia mimba?
Ndio.Kukunywa pombe haitapunguza ufanisi wa vipandikizi vya kuzuia mimba. Lakini kumbuka kukunywa kwa uwajibikaji. Pombe hupunguza uwezo wa mtu kujidhibiti,ikiwemo uwezo wa kufanya ngono salama. Kumbuka, kipandikizi cha kuzuia mimba hakikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa.
JInsi ya kukomesha matone ya damu wakati wa matumizi ya kipandikizi cha kuzuia mimba
Kwa mujibu wa planned parenthood, ni kawaida kuona mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi, baada ya kuingiziwa vipandikizi vya kuzuia mimba. Watu wengine watatokwa matone ya damu ndani ya miezi 6-12 ya kwanza. Wengine watatokwa matone ya damu kwa muda mrefu au hedhi nzito na inayoendelea kwa siku nyingi zaidi. Kwa idadi kubwa ya watumiaji, hedhi yao hupotea kabisa. Ikiwa utajipata unatokwa matone ya damu kwa muda mrefu na hali hii inakusumbua, tembelea mtoa matibabu wako kwa matibabu. Ikiwa matone ya damu nyepesi hayataisha baada ya matibabu, zingatia kutumia njia tofauti ya uzuiaji mimba.