Ni wapi ninaweza kutolewa kipandikizi cha kuzuia mimba?
Mtu anaweza kuamua kutoa kipandikizi cha kuzuia mimba kwa sababu mbalimbali, ikiwemo, kupata mimba, kutumia njia tofauti ya uzuiaji mimba, au kuweka kipandikizi kipya. Kama tu uingizaji, uondoaji lazima ufanywe na mtoa matibabu aliyehitimu.
Kwa utoaji, mtoaji matibabu wako atakufa ganzi mkono wako, achanje sehemu ndogo ya ngozi yako na atoe kipandikizi. Ukitaka kuendelea kutumia kipandikizi kama njia ya uzuiaji mimba, unaweza kuwekewa kingine mara hio hio [5].
Je, niwaweza kutoa kipandikizi changu nikiwa nyumbani?
Hapana. Kutoa kipandikizi ukiwa nyumbani haiwezekani. Mtu tu anayehitimu kukitoa ni mtoa matibabu aliyepata mafunzo maalum.
Ni nini itafanyika wakati kipandikizi changu cha kuzuia mimba kitafika tarehe yake ya mwisho wa matumizi?
Kipandikizi cha kuzuia mimba kimeundwa kuwachilia homoni ambazo zitakuzuia kushika mimba kwa kipindi fulani. Mara tu kipindi hiki kimeisha, kiwango cha kuwachilia homoni hupungua. Kwa hivyo, utakuwa katika hatari ya kushika mimba, kukiwemo hatari kidogo ya mimba hio kujitunga nje ya mji wa mimba. Wakati wa uingizaji, andika siku ya utoaji au omba mtoa matibabu akukumbushe wakati siku ya utoaji inakaribia. Iwapo utachelewa kutoa kipandikizi ambacho tarehe yake ya mwisho wa matumizi imepita, lazima utumie njia ziada ya uzuiaji mimba hadi utakapoweka kipandikizi kipya au utakapo anza kutumia njia tofauti ya uzuiaji mimba.
Na ikiwa nitashika mimba wakati nina kipandikizi cha kuzuia mimba?
Ingawa kipandikizi cha kuzuia mimba ni cha muda mrefu ambacho kinaweza kufanya kazi hadi miaka 5, unaweza kukitoa wakati wowote kwa sababu zozote, ikiwemo ukitaka kushika mimba. Sawa na njia zingine za uzuiaji mimba za homoni, kipandikizi madhara yake inaweza kupinduliwa, na wanawake wengi yai litapevuka wiki chache baada ya kutoa kipandikizi. Watengenezaji wa Nexaplanon wamedai kwamba mwanamke anaweza kushika mimba ndani ya wiki moja baada ya kutoa kipandikizi.