Uzuri na Ubaya za kipandikizi cha kuzuia mimba (Madhara)

Uzuri na Ubaya za kipandikizi cha kuzuia mimba (Madhara)
Uzuri na Ubaya za kipandikizi cha kuzuia mimba (Madhara)

Kutumia kipandikizi kama njia ya uzuiaji mimba inaweza kuwa na madhara ambayo athari yake yanaweza kuwa mzuri au mbaya. Kwa mfano, watu walio na chunusi wanaweza ona chunusi zikiisha au zikiongezeka. Pia kuna uzuri na ubaya zinazohusiana na mabadiliko kwenye mzunguko wa hedhi na inaweza kuwa nzuri kwa mtu ambaye anapendelea kutokuwa na mzungo wa hedhi unaotabirika. Ikiwa unapendelea kukuwa na mzunguko wa hedhi unaotabirika, kipandikizi cha kuzuia mimba huenda hakitakua chaguo bora kwako.

Madhara ya kipandikizi cha kuzuia mimba

Madhara ya kawaida kabisa ya kipandikizi cha kuzuia mimba yanahusiana na kutokwa damu kwenye uke.
Watumiaji wa kipandikizi cha kuzuia mimba wameripoti kupata hedhi isiyotabirika, hasa ndani ya miezi 6-12 ya kwanza (hii imaweza kumanisha kutokwa matone ya damu kabla ya hedhi inayofuata, au hedhi nzito inayoendela kwa muda mrefu;hedhi isiyotabirika wakati wote kipandikizi kiko ndani;au kutokuwa na hedhi kabisa). Unapaswa kuwa sawa kupata hedhi isiyotabirika ikiwa unapanga kutumia kipandikizi. Watumiaji wa kipandikizi wana uwezo wa juu ya kupata hedhi inayokuja mara chache au kutopata hedhi kabisa zaidi ya kupata hedhi isiyotabirika.

Madhara mengine yanajumuisha

  • Chunusi (inaweza kuongezeka au kupungua)
  • Mabadiliko kwa hamu ya chakula;
  • Maumivu ya tumbo au/na tumbo kujaa
  • Mabadiliko kwa tamaa ya ngono;
  • Uvimbe kwenye ovari
  • Msongo wa mawazo
  • Ngozi kubadilika rangi au kuwa na makovu pahali palipo ingizwa kipandikizi (wanawake wengine hupata kovu ndogo au kovu nene)
  • Kizunguzungu;
  • Kupoteza nywele;
  • kuumwa kichwa;
  • kichefuchefu;
  • wasiwasi;
  • ulaini wa matiti; na
  • uchungu au mchubuko pahali palipo ingizwa kipandikizi, lakini hii itaendelea tu kwa wiki moja au wiki mbili.[9]

Ikiwa, baada ya miezi sita, unahisi madhara yamezidi kiasi unaweza kuvumilia, unaweza kutoa kipandikizi na utumie njia ya uzuiaji mimba tofauti.

Kumbuka kwamba kipandikizi cha kuzuia mimba hakikukingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs)

Matatizo ya kipandikizi cha kuzuia mimba

Isiyo ya kawaida

Maambukizi eneo la uingizaji- Maambukizi mara nyingi hutokea ndani ya miezi miwili ya kwanza baada ya uingizaji.

Utoaji mgumu- Hii hutokea nadra ikiwa kipandikizi kiliingizwa kwa njia sawa na ikiwa mtoa matibabu ana ujuzi wa utoaji wa kipandikizi.

Nadra

Kipandikizi kutoka pahali pake, ambalo likifanyika mara nyingi litafanyika ndani ya miezi nne ya kwanza baada ya uingizaji. Iwapo katika hali nadra, kipandikizi kitoke chenyewe, unapaswa mara hi hio kuanza kutumia njia ya uzuiaji mimba ya ziada na umuone mtoa matibabu wako kwa suluhu.[10]

Nadra kabisa

Kusonga kwa kipandikizi. Kumekuwa na ripoti chache za vipandikizi kupatikana kwenye sehemu zingine za mwili, hasa kwasababu ya uingizaji usio sahihi. kwenye jarida lililoandikwa na Zhang na wenzake, inasemekana kwamba kusonga kwa kipandikizi cha kuzuia mimba ni nadra sana, na ikifanyika, kipandikizi hakisongi mbali na mkono. Kwa hali nadra kabisa, kipandikizi kinaweza kuhamia mapafu, kupitia mkondo wa damu.

Na ikiwa sipendi kutokwa matone ya damu inayosababishwa na kitanzi cha kuzuia mimba?

Kutokwa matone ya damu au kutokwa damu kwa hali isiyotabirika ni kawaida lakini ni madhara isiyo na athari yoyote mbaya.

Ikiwa nina kipandikizi cha kuzuia mimba na sipati hedhi, nitajua aje kwamba sina mimba?

Ni kawaida kwa hedhi kupotea baada ya mwaka wa kwanza wa kutumia kipandikizi cha kuzuia mimba. Hii sio ishara ya mimba. Ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi, chini ya asilimia 1 ya wanawake wanaotumia kipandikizi cha kuzuia mimba watashika mimba, na hii ikifanyika, kuna uwezo kwamba mimba itajitunga nje ya mji wa mimba. Mimba njee ya mji wa mimba hutokea wakati yai lililorutubishwa linajipandikiza nje ya mji wa mimba, mara nyingi kwenye mirija ya uzazi. Ikiwa unashuku kwamba una dalili za kwanza za mimba, pima mimba ili kuthibitisha ikiwa una mimba kwa ukweli

Dalili za kwanza za mimba nje ya mji wa mimba ni kama za mimba ya kawaida. Wiki za mimba zikiongezeka, unaweza kuanza kupata ishara zingine kama kutokwa damu kwenye uke,maumivu makali yanayokuja ghafla kwenye sehemu ya chini au upande mmoja wa tumbo, maumivu mabegani, na maumivu kwenye ngongo wa chini. Ikiwa kipimo kitaonyesha kwamba una mimba, mara moja nenda ukamuone mtoa matibabu kwa vipimo sahihi. Kwa sababu virutubisho vinayopatikana kwenye mji wa mimba haviwezi kufika kwenye mirija ya uzazi, kijusi wa mimba nje ya mji wa mimba hawezi kuishi. Mimba nje ya mji wa mimba kwa kawaida hutibiwa kwa dawa zinazokomesha ukuaji wa kijusi. Kwa hali nadra ikiwa mirija ya uzazi imepasuka, mimba hutolewa kwa njia ya upasuaji

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...