Manufaa ya kiafya
- Kinapunguza hatari ya mimba kutunga nje ya mji wa mimba.
- Kinaweza kusaidia kukinga dhidi ya anemia ya ukosefu wa madini ya chuma. Mara mwili imeshazoea kipandikizi, wanawake wengi wameripoti kupata hedhi chache na nyepesi.
- Kinaweza kupunguza dalili zinazokuwepo kabla ya hedhi (PMS), msongo wa mawazo na dalili za ugonjwa wa endometriosis.
- Kinaweza kutumika na wanawake ambao hawawezi kutumia estrojeni, kwa mfano, wakati wananyonyesha.
- Ni salama kwa wavutaji sigara, na wale walio na shinikizo la damu na ugonjwa wa sukari.
Manufaa kwa mtindo wa maisha
Kinatoa kinga ya muda mrefu dhidi ya hatari ya kushika mimba.
Mara Kipandikizi kimeingizwa, hauhitaji kufanya chochote. Kipandikizi kinabaki chini ya ngozi yako, kikikupa kinga dhidi ya mimba kwa miaka tatu hadi tano, kulingana na aina ya kipandikizi ulichoingiza[7].
Kipate na uisahau
Kina ufaragha
Watu wengi hawawezi kugundua kwamba una kipandikizi. Hakuna pakiti na pia hakuna chochote unastahili kufanya kabla ya kufanya ngono.
Ni rahisi kutumia.
Hakuna pakiti au dawa zozote za kuandikiwa ukachukue kwenye duka la dawa-hakuna kitu kinachoweza kupotea au kusahaulika.
Kinahitaji bidii ndogo
Mara kipandikizi kimeingizwa, hakuna unachohitajika kufanya. Kipandikizi kinabaki chini ya ngozi yako, kikikupa kinga dhidi ya mimba kwa miaka tatu hadi tano, kulingana na aina ya kipandikizi umekiingiza.
Urutubisho wa uzazi hautachelewa kurudi.
Unapaswa kuweza kushika mimba wakati wowote baada ya kipandikizi kutolewa. Ikiwa itatolewa lakini hautaki kushika mimba, jikinge kwa njia nyingine ya uzuiaji mimba mara hio hio
Kinapatikana kwa wingi
Ungependa Kutumia kipandikizi cha kuzuia mimba? Kinapatikana kwa wingi; hata hivyo, aina na chapa maalum zinatofautiana nchi moja hadi nyingine.