Ingawa kipandikizi cha kuzuia mimba ni salama na kina ufanisi, kwa wanawake wengi, kuna hali zinaweza kufanya matumizi ya kipandikizi isiwafae. Hizi ni kama kuwa na hali inayohitaji uepuke matumizi ya projestini au dawa unazotumia zitapunguza ufanisi wa homoni ya projestini kwa kuzuia mimba.
Ni wakati gani sifai kutumia kipandikizi cha kuzuia mimba?
- Ikiwa unashuku kwamba uko na mimba;
- ikiwa una ugonjwa wa ini au uvimbe;
- ikiwa unatokwa damu kwenye uke kwa hali isiyoelezeka (daktari wako atahitaji kuchunguza chanzo cha hiki, kabla ya uingizaji wa kipandikizi);
- una historia ya saratani ya matiti; na
- unatumia dawa zozote ambazo zinaweza kuzuia kipandikizi cha kuzuia mimba kufanya kazi kwa ufanisi.