Dawa ya kuua manii

Dawa ya kuua manii
Dawa ya kuua manii

Dawa ya kuua manii ni nini?

Dawa za kuua manii ni dawa ambazo zinaweza kufanya manii isisonge au ziuwe manii. Ni njia ya kizuizi ya uzuiaji mimba ambayo unaweka ndani kabisa kwenye uke, karibu na shingo ya kizazi, mara tu kabla ya kufanya ngono ili kuangamiza manii kabla ifike kwenye mji wa mimba (1).

Kuna aina na chapa tofauti za dawa za kuua manii zinazopatikana sokoni. Aina inayotumiwa zaidi ni ile ina nonoxynol-9. Aina hii ya dawa ya kuua manii imethibitishwa kutoa kinga dhidi ya maambukizi ya kisonono na kalmidia.

Aina zingine za dawa za kuua manii zinajumuisha zile zina menfegol, benzalkonium chloride, octoxynol-9, chlorhexidine, na sodium docusate.

Dawa za kuua manii zinapatikana kama krimu, jeli, tembe za povu, utando za kuyeyuka, dawa za kuingiza za kuyeyuka ama za povu, na makopo ya povu ya kufinywa.

Dawa za kuua manii ambazo zinapatikana kama krimu, jeli na povu kutoka kwa makopo zinaweza kutumika pekee yake, pamoja na kondomu ama pamoja na dayaframu.

Zile zinazopatikana kwa muundo wa tembe za kuingiza za kuyeyuka, utando, tembe za povu ama dawa za kuingiza za povu zinaweza kutumiwa peke yao ama pamoja na kondomu.

Dawa ya kuua manii hufanya aje kazi?

Dawa ya kuua manii hufanya kazi kwa kusababisha utando wa seli za manii kuvunjika kwa njia inayoziuwa au kuzifanya zisonge polepole. Hii huzuia manii kukutana na yai.

Dawa za kuua manii zina ufanisi wa kiasi gani?

Ufanisi wa dawa ya kuua manii inategemea kwa kiasi kikubwa jinsi inatumiwa kwa njia sahihi na mfululizo. Hatari ya mimba huongezeka wakati dawa ya kuua manii haitumiwi kwa kila kitendo cha ngono. Dawa ya kuua manii huwa inapakwa mara tu kabla ya kila kitendo cha ngono , na ufanisi wake hubaki kwa saa moja tu. Ingawa inaweza kutumiwa kama njia ya msingi ama ya pili, dawa ya kuua manii hufanya kazi bora zaidi ikitumiwa pamoja na njia zingine za kizuizi za uzuiaji mimba, kama vile dayaframu, kofia ya shingo ya kizazi au kondomu. Ikitumiwa peke yake, dawa za ukeni za kuua manii zinatoa kinga ya chini mno dhidi ya maambukizo ya magonjwa ya zinaa (STIS) na hazitoi kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.

Inavyotumiwa kwa kawaida, dawa za kuua manii zina ufanisi wa asilimia 79 ndani ya mwaka wa kwanza. Hii inamaanisha kuwa wanawake 21 kati ya 100 wanaotumia dawa ya kuua manii watashika mimba. Kwa matumizi sahihi kwa kila kitendo cha ngono, dawa ya kuua manii inaweza kukuwa na ufanisi wa asilimia 84 wa kuzuia mimba. Hii inamaanisha kuwa wanawake 16 kati wa 100 wanaotumia dawa ya kuua manii watashika mimba (3).

Kwa ujumla, ufanisi wa dawa ya kuua manii unaweza kukuwa chini, hadi asilimia 50 ama uwe juu, hadi asilimia 99.9 kulingana na jinsi inavyotumiwa kwa usahihi, peke yake, au ikiwa pamoja na njia zingine za vizuizi. Uwekaji sahihi wa dawa ya kuua manii kwenye shingo ya kizazi na kuipa muda wa kutosha wa kuenea ni muhimu na unaweza kuathiri ufanisi. Kutumia dawa ya kuuwa manii pamoja na njia zingine za vizuizi huongeza pakubwa ufanisi wake. Kutumia dawa ya kuua manii pamoja na kondomu inajulikana kuleta ufanisi wa asilimia 99.9. (4).

Jinsi ya kutumia dawa ya kuua manii

Kwa matumizi sahihi, hakikisha umesoma maagizo kwenye pakiti na uangalie tarehe ya mwisho ya matumizi. Dawa za kuua manii ni rahisi kutumia-unaingiza tu kwa urahisi ndani ya uke kwa kutumia vidole au kifaa cha kupaka.

-Paka au ingiza dawa ya kuua manii ndani kabisa ya uke ili kufunika shingo ya kizazi.
-Tumia kiwango cha kutosha cha dawa ya kuua manii.
-Ingiza dawa zaidi ya kuua manii wakati wa kila kitendo cha ndoa.
-Ngoja kwa muda uliopendekezwa kati ya kupaka dawa na kufanya ngono. Dawa zingine za kuua manii huhitaji kwamba ungoje kwa dakika 10-15 kabla ya kufanya ngono.Hii hupatia dawa ya kuua manii muda wa kuyeyuka na kutawanyika. Aina hizi za dawa za kuua manii pia zina ufanisi tu kwa saa moja baada ya kuziweka ndani. kama zaidi ya saa tatu zimepita kabla ya kufanya ngono, paka dawa ya kuua manii tena.
-Utandu wa uke wa uzuiaji mimba (safu ya inchi 2-kwa-2 iliyo na asilimia 28 ya nonoxynol-9) unaingizwa angalau dakika 15 kabla ya ngono ili uyeyuke na kutawanyika. Kama zaidi ya saa tatu zimepita, lazima uingize utandu mwingine.
-Dawa ya kuua manii ya aina ya povu iliyo na asilimia 12.5% ya nonoxynol-9 ina ufanisi mara hio hio inapoingizwa na hadi saa moja baada ya kuingizwa. Inaingizwa kwenye uke kutumia kifaa cha kupaka, na utahitajiwa kuipaka tena kabla ya kila kitendo cha ngono kingine.
–Usioshe uke kwa angalau saa sita baada ya ngono.
-Kila mara, kuwa na dawa ya kuua manii ya ziada karibu nawe (5).

Mazuri ya dawa ya kuua manii

-Ni rahisi kutumia na inapatikana kwa urahisi. Hauhitaji ujuzi maalum kuitumia.
-Inaweza kuingizwa kama sehemu ya unyegereshano.
-Haina homoni.
-Hauhitaji agizo la daktari. Hauhitaji kuona mtoa huduma za kitiba ili utumie dawa ya kuua manii.
-Unaweza kuitumia wakati unanyonyesha.

Je, unaweza kutumia dawa ya kuua manii baada ya ngono?

La, ili iwe na ufanisi wa kuzuia mimba, dawa ya kuua manii inaweza tu kuingizwa kabla ya kufanya ngono.

Je, ninaweza kutumia dawa ya kuua manii wakati wa hedhi?

Ndio, unaweza kutumia dawa ya kuua manii wakati wa hedhi yako. Hata hivyo, haushauriwi kuitumia pamoja na dayaframu ama kofia ya shingo ya kizazi kwasababu utakuwa katika hatari ya sumu mwilini inayoletwa na baktreia. Unachaguo ya kuitumia pamoja na kondomu. Dawa ya kuua manii haiathiri hedhi yako ama homoni kwa namna yoyote.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...