Je, dawa ya kuua manii ni njia ya uzuiaji mimba salama?
Watu wengi hawapati matatizo yoyote mwilini wanapotumia dawa ya kuua manii; wakipata matatizo, yataisha kwa kawaida baada ya kuwacha kutumia dawa ya kuua manii.
Watu wengine wana mzio wa dawa ya kuua manii. Dawa nyingi za kuua manii zina kiungo sawa hai-nonoxynol-9. Nonoxynol-9 inaweza kusababisha mwasho ukeni ama kwenye uume wa mwenza wako (hasa ukiitumia zaidi ya mara moja kwa siku). Hii inaweza kuongeza hatari ya VVU na kuenea kwa magonjwa ya zinaa. Kama utahisi kuwashwa wakati unatumia dawa ya kuua manii, basi huenda sio chaguo bora kwako.
Mabaya ya kutumia dawa ya kuua manii
-Inaweza kuleta uchafu na/ au kuvuja kutoka kwa uke.
-Inafanya kazi bora zaidi kama wenza wote hawana VVU. Mojawapo ya viungo hai, nonoxynol-9, inasababisha mabadiliko kwa ngozi yenye shida. Hali hii inafanya iwe rahisi kwako kuambukizwa VVU. Kama wewe ama mwenza wako mna VVU, hamjapimwa hivi karibuni, au mnafanya ngono na wenza wengine tofauti, pengine mchague njia ya uzuiaji mimba ambayo itasaidia kukulinda dhidi ya maambukizi ya VVU.
-Kiwango cha kufeli kwa dawa ya kuua manii kiko juu. Kama hautaki kushika mimba, basi tumia njia ingine ya uzuiaji mimba ama utumie dawa ya kuua manii pamoja na njia ingine ya kizuizi.
-Ina jitihada kubwa kwasababu unahitaji kuipaka kila mara unafanya ngono.
-Huenda hautapenda ladha yake.
-Haikupi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.
-Ni ngumu kukumbuka kuitumia kama umelewa.