Kondomu za nje ni nini?
Kondomu za nje,ambazo saa zingine zinaitwa,Kondomu za kiume, “mwavuli”, “koti za mvua”, “ngozi” au “prophylactics”- ni vitu vya kufunika au ala ambazo zinavaliwa kwenye uume uliyosimama ili kuzuia manii iliyo ndani ya kondomu kuingia ndani ya uke, mkundu au mdomo. Zinachukuliwa kama njia ya kizuizi bora zaidi, na ni njia maarufu sana inayotumika kuepuka mimba na kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs). Iingize tu kwenye uume uliyosimama au kwenye mwanaserere wa ngono kabla ya aina wowote wa ngono wa kupenya.
Kondomu za nje zinakuja kwa mamia ya umbo na ukubwa na pia unaweza kuzinunua na mafuta ya kulainisha au bila. Aina ya kawaida zaidi ya kondomu za nje zimeundwa na ulimbo wa mpira (latex), lakini kondomu zinaweza kutengenezwa kutoka kwa nyenzo zingine, zikiwemo ngozi ya mwana kondoo, nitrile, polyurethane, na polyisoprene.
Kondomu za nje zingine zimefunikwa na dawa ya kuua manii-kemikali ambayo inaua manii. Kondomu zilizo na dawa ya kuua manii hazipendekezwi kwa ngono ya mdomo au mkundu. Ikiwa wewe au mwezi wako mna mzio wa dawa ya kuua manii, tafuta kondomu bila dawa hizo.
Je, kondomu za nje hufanyaje kazi?
Kondomu ya nje inazuia mimba kwa kuweka kizuizi kinacho sitisha manii kuingia kwenye uke. Pia inazuia maambukizi kutoka kwenye uume, shahawa,uke au mkundu kutopita na kuenda kwa mwenzi.
kwa ufanisi wa juu zaidi, kondomu ya nje inahitaji matumizi sahihi katika kila tendo la ngono (1).
Aina za kondomu za nje
Kondomu za Latex (ulimbo wa mpira). Kondomu za latex zimeundwa kwa mpira unaoweza kunyooroka hadi asilimia 800. Hizi ndizo aina za kondomu za kawaida zaidi. Usizitumie pamoja na mafuta ya kulainisha yenye oili kwasababu yanaweza kusababisha kondomu kupasuka au kuteleza, na kuongeza hatari ya mimba au magonjwa ya zinaa.
Kondomu bila latex. Ikwa una mzio wa latex au unapendelea mafuta ya kulainisha yenye oili, basi tafuta kondomu bila latex. Kwa kawaida zimeundwa kwa polysoprene (mpira bandia) au polyurethane (plastiki). kama vile kondumu za latex, zitakulinda dhidi ya mimba na magonjwa ya zinaa. Kwa aina hizi za kondomu,unaweza kutumia mafuta ya kulainisha yenye oili au maji. Kwa jumla,mafuta ya kulainisha yenye maji yanapendekezwa wakati unatumia kondomu na zinaweza kuongeza raha ya ngono.
Kondomu za ngozi ya wanyama. Pia zinajulikana kama kondomu za ngozi ya mwana kondoo, zimeundwa kwa utando wa matumbo wa mnyama. Ni chaguo bora mbadala kwa watu walio na mzio wa kondomu za latex. Hata hivyo, ujue kwamba zinasaidia kuzuia mimba lakini hazitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Na aina hii ya kondomu, unaweza kutumia mafuta ya kulainisha yenye maji au oili.
Kondomu za nje zina ufanisi wa kiasi gani?
Ufanisi wa kondomu ya nje unategemea kwa kiwango cha juu jinsi unavyoitumia. Utakuwa katika hatari ya juu ya mimba/ au kupata magonjwa ya zinaa ikiwa hautatumia kondomu kila mara unafanya ngono.Mimba zinazohusishwa na kondomu zinasababishwa na matumizi yasiyo sahihi, kupasuka au kuteleza.
Inavyotumika kwa kawaida, wanawake 13 kati ya 100 wanaotumia kondomu ya nje kama njia ya kuzuia mimba hushika mimba ndani ya mwaka wa kwanza ya matumizi. Hii inamaanisha kwamba ina ufanisi wa asilimia 87 kwa matumizi ya kawaida. Kwa matumizi kamilifu, ni wanawake 2 tu kati ya 100 wanaotumia kondomu za nje kama njia ya kuzuia mimba wanashika mimba ndani ya mwaka wa kwanza ya matumizi. Hii inamaanisha ina ufanisi wa asilimia 98 ikitumika kila wakati unafanya ngono na kwa njia sahihi.
zikitumiwa kila mara na kwa njia sahihi wakati wa ngono wa ukeni au kwenye mkundu, kondomu zinapunguza hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa.Kwa matumizi kamilifu, kondomu za kiume zina ufanisi wa asilimia 80-95 wa kupunguza maambukizi ya VVU ambayo yangepatikana ingekuwa kondomu haikutumiwa.
Matumizi sahihi ya kondomu za nje hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa yanayosambazwa kupitia mchozo (klamidia,kisonono, VVU) na yale yanayosambazwa kupitia kugusana kwa ngozi ya watu (virusi vya binadumu vya papillovirus na herpes) (2).