Je kuna madhara yoyote ya kutumia kondomu ya nje?

Je kuna madhara yoyote ya kutumia kondomu ya nje?
Je kuna madhara yoyote ya kutumia kondomu ya nje?

Isipokuwa uwe na mzio wa latex, kondomu za nje hazina madhara makubwa. Hata hivyo, zinaweza kuwa na baadhi ya ubaya.

Ubaya wa kondomu

-Kondomu ya nje haifai ikiwa una mzio wa latex. Ni mtu 1 au watu 2 kati ya watu 100 ambao wana mzio. Ikiwa wewe ni mmoja wao, utahitaji kutumia kondomu bila latex, ambayo wakati mwingine huwa ghali au haipatikani katika baadhi ya maeneo. Ikiwa hauwezi kupata kondomu bila latex, jaribu njia nyingine.
-Kutumia kondomu ya nje kunahitaji jitihada na kujitolea. Ili iwe na ufanisi, lazima ivaliwe kila mara kwa njia sahihi kwenye uume, hata iwe nini.
-Kutumia kondomu kunaweza kutoa hamu ya ngono kwa mwenzi mmoja. Katika hali zingine, mwenzi wa kike anaweza kupata ugumu wa kushurutisha mwenzi wake wa kiume atumie kondomu kila wakati kwa njia sahihi.
-Kondomu za nje hazitakukinga kutokana na magonjwa ya zinaa yanayosambazwa kwa njia ya kugusana kwa ngozi., ikiwemo HPV na herpes.
-Kondomu za ngozi ya mwana kondoo zinazuia tu manii na hazitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Uchunguzi wa kimaabara umeonyesha kwamba virusi kama vile homa ya ini B, homa ya ini simplex, na VVU vinaweza kupenya matundu yaliyo kwenye kondomu ya ngozi ya mwana kondoo.
-Kondomu zinazoitwa novelty condoms, kama vile zile zinapatikana kwenye maduka na katalogi za wanaserere wa ngono, baadhi zao zimeundwa kwa nyenzo ambazo hazitakupa kinga dhidi ya mimba au magonjwa ya zinaa. Aina hizi za kondomu hazipaswi kutumiwa wakati moja na kondomu za latex kwa sababu zinafanya latex iwe dhaifu.
-Ingawa kondomu za latex hufika tarehe ya mwisho ya matumizi ndani ya miaka mitatu au mitano, zinaweza kuharibika katika halijoto ya juu ( juu ya njuzi joto 40) na katika hali ya uhifadhi yenye unyevu, au ikiwekewa mafuta ya kulainisha yenye oili.
-Watu wengine watakuwa na mzio wa aina fulani ya mafuta ya kulainisha kwenye kondomu. Ikiwa una mzio, jaribu chapa tofauti ya kondomu.
-Wanaume wengine hulalamika kuwa kondomu zinapunguza hisia za ngono (5).
-Ni ngumu kukumbuka kutumia kondomu wakati umelewa. Una uwezo zaidi wa kukumbuka kuzitumia ikiwa unaweza kuzipata kwa urahisi kila wakati.

Contraception Quiz

Not sure on the method? - Take our dynamic Contraception Quiz.
When it comes to sex, protection is as important as pleasure. But what should one do to start their safe sex journey? Answer some simple questions and based on the responses, we will recommend the next steps.

Take the quiz
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...