Manufaa ya Kondomu
-Ufanisi. Kondomu ikitumiwa kwa njia sahihi,kila watu 98 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba. Lakini watu wengi hawatumii kondomu vikamilifu- kwasababu hii, ni watu 82 tu kati ya 100 wanaotumia kondomu wataweza kuzuia mimba.
-Kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.Kondomu nyingi za nje husaidia kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa, ikiwemo HIV. Hata hivyo, sehemu ya siri ambayo haijafunikwa na kondomu inaweza kuleta hali ya ngozi kugusana na hivyo kusambasa maambukizi ya virusi au bakteria kupitia ngozi.
-Zinaweza kusaidia kuzuia tatizo ya kumwaga haraka.
Zinaweza kuongeza tamaa ya kingono kabla ya kuingiza uume kwenye uke. Ikiwa unaweza kuzungumza na mwezi wako kuhusu ngono bila aibu, ni muhimu kuzungumza kuhusu jinsi mnavyoweza kutumia kondomu kuongeza ridhaa kwa maisha yenyu ya ngono.
-Inaweza kusaidia ngono iende muda mrefu zaidi. Kondomu za nje zinaweza kupunguza hisia za ngono. Wakati mwingine, hili ni jambo mzuri. (ikiwa una tatizo la kumwaga haraka, kondomu zinaweza kusaidia ngono yenyu kuenda muda mrefu.)
-Hauhitaji agizo la daktari.
-Zinapatikana kwa bei nafuu na ni rahisi kuzipata. Kondomu za latex ni za bei nafuu na pia unaweza zipata bure wakati mwingine. Unaweza kuzipata karibu kila mahali na kuna aina nyingi mbaimbali.
-Kondomu (bila latex) husambaza joto zaidi la mwili na kuruhusu hisia zaidi wakati wa ngono. Kondomu za Polyurethane (bila latex) zinajulikana kuhisi nyembamba zaidi na hutosha uume vizuri zaidi. Tofauti na kondomu za latex, haziharibiki haraka na zinaweza kutumiwa pamoja na mafuta ya kulainisha yenye oili.
-Zinaweza kutumiwa kama dental dam. Dental dam ni kipande nyembamba ya latex au polyurethane ambacho kinatumiwa kupunguza hatari ya kueneza magonjwa ya zinaa kupitia ngomo ya mdomoni.Inafanya kazi kama kizuizi kati ya mdomo wako na sehemu ya siri au mkundu wa mwenzi wako.