Jinsi ya kutumia kondomu ya nje

Jinsi ya kutumia kondomu ya nje
Jinsi ya kutumia kondomu ya nje

Ikiwa unatumia kondomu ya nje pekee kama njia ya uzuiaji mimba ya kila siku, unapaswa kukumbuka kutumia kondomu kila wakati unafanya ngono.

Kitu cha kwanza unahitaji kufanya ni kununua kondomu yenye ukubwa inayokufaa kwenye mtindo unaopendelea kisha angalia tarehe ya mwisho ya matumizi. Kondomu zilizofika tarehe ya mwisho ya matumizi hupasuka virahisi, na kuzitumia hukuweka katika hatari ya maambukizi au mimba.

Jinsi ya kuvaa kondomu

-Mara uume umesimama, toa kondomu kwenye pakiti. Kuwa mwangalifu usiirarue wakati unaifungua. Ikiwa imeraruka, dhaifu au ngumu, itupe na utumie ingine.
-Shika karibu nusu inchi ya kipeo cha kondomu kati ya kidole gumba na kidole cha shahada, kisha ichune hewa itoke. Nafasi ya ziada kwenye kipeo ni ya kusaidia kukusanya manii baada ya kumwaga manii.
-Weka sehemu iliyo wazi juu ya uume na uikunjue juu ya uume hadi itakapofika. Ukipata ugumu kuivingirisha, weka tone moja au mawili ya mafuta ya kulainisha ambayo haina oili ndani ya kondomu. Yatasaidia kondomu kuvingirika na hii itakupa wewe na mwenzi wako raha zaidi. Mwenzi wako pia anaweza kukusaisia kuvaa kondomu. Iwapo uume haujatahiriwa, ni muhimu kuvuta nyuma govi kabla ya kuviringisha kondomu kwenye uume.
-Lainisha kutoa mapovu ya hewa yoyote yalioingia kwenye kondomu. Mapovu ya hewa yanaweza kufanya kondomu ipasuke.
-Ukipenda, tumia mafuta zaidi ya kulainisha yenye maji nje ya kondomu ili kupunguza maumivu.
Sasa, uko tayari kufanya ngono iliyo na kinga!

Jinsi ya kuvua kondomu

-Mara tu baada ya uume kumwaga manii, shikilia sehemu ya juu ya kondomu kwa uthabiti ikiwa imeshikilia uume ambao bado umesimama na hakikisha kuwa inabaki hivyo uume unapotolewa. Hakikisha kwamba uume umetolewa ndani ya uke kabla uume kulegea.
– Shikilia sehemu ya mwisho ya kondomu wakati unapo toa uume wako. Hii iitasaidia kuzuia manii ndani ya kondomu kumwagika.
-Ili manii ibaki ndani ya kondomu, funga fundo kwenye sehemu iliyo wazi.
-Kagua kondumu kama kuna matundu au uharibufu wowote. Ikiwa utaona uharibifu wowote au ikiwa kondomu iliteza na ikatoka wakati wa ngono, mwenzi wa kike anapaswa kuzingatia kutumia njia ya dharura ya uzuiaji mimba (ndani ya saa 72). Iwapo una wasiwasi kama ngono ilikuwa salama, weka miadi ya kupimwa maambukizi ya zinaa na utaratibu wowote mwingine muhimu wa usalama, kama vile kutumia Dawa za Kinga Baada ya kuwemo hatarini (PEP). Tahadhari sawa na hii inapaswa kuchukuliwa ikiwa kondomu itateleza na kutoka wakati wa ngono.
-Funga kondomu kwa karatasi ya tissue kisha uitupe kwenye pipa la taka au choo cha kuchimba (kama kiko). Usiitupe kwenye choo cha maji kwasabu itakiziba. Kumbuka kila mara kuweka kondomu mbali na watoto na wanyama kipenzi.
-Osha uume kwa sabuni na maji kabla ya kufanya ngono tena.

Vidokezo zaidi vya kutumia kondomu kwa njia sahihi

Kondomu za nje ni rahisi sana kutumia, lakini hapa kuna vidokezo vya kukusaidia kuzitumia kwa njia sahihi:
-Tumia kondomu kila wakati unafanya ngono.
-Kila mara soma maelekezo kwenye pakiti na kumbuka kuangalia tarehe ya mwisho ya matumizi. Kondomu iliyofika tarehe ya mwisho ya matumizi itapasuka virahisi.
Kila mara kumbuka kuangalia kama kondomu imeraruka au imeharibika kabla ya kuitumia.
-Hakikisha umevaa kondomu kabla uume wako ugusane na uke wa mwenzi wako. Umajimaji kabla manii-umajimaji unaotoka kwenye uume kabla mwanamume amwage manii- unaweza kuwa umebeba manii iliyobaki mara ya mwisho mwanamume alimwaga manii.
-Usitumie zaidi ya kondomu moja kwa wakati mmoja. Kutumia zaidi ya kondomu moja haikupi kinga zaidi. Badala yake, inaifanya iwe rahisi kwa kondomu kuteleza naitoke na hii inaongeza hatari ya mimba au magonjwa ya zinaa.
-Epuka kutumia bidhaa zenye oili pamoja na kondomu, kama vile losheni, mafuta ya watoto, mafuta ya petroleum jelly, au mafuta ya kupika. Zitafanya kondomu ipasuke.
-Usiwahi kurudia kutumia kondomu ambayo ishatumiwa. Tumia kondomu moja tu kwa kila unapomwaga manii na uwe na kondomu za ziada karibu.
-Kila mara hifadhi kondomu mahali penye baridi, pakavu.
EPUKA kuhifadhi kwenye pochi yako. Msuguano na joto kutokana na kutembea inaweza kuziharibu. (4).

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...