Ni kwa njia gani sindano ya kuzuia mimba huzuia mimba?
Sindano ya kuziuia mimba, pia inayojulikana kama ya kudunga au sindano ya kudhibiti mimba/ choma ni majimaji iliyo na aina za homoni bandia za homoni zinazopatikana kwenye mwili wa mwanamke. kwa kawaida, inadungwa kwenye mwili wa mwanamke kuzuia mimba. Mara imedungwa,homoni inawachiliwa polepole kwa mwili wa mwanamke. Sindano inafanya kazi kimsingi kwa kuzuia ovari kuwachilia yai. Pia inafanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito ili kusaidia kuzuia manii kufikia yai.[1].
Aina za sindano za kuzuia mimba
Sindano ya kila mwezi au Sindano mchanganyo
Pia inajulikana kama sindano mchanganyo ya kuzuia mimba. Ina homoni mbili-projestini na estrojeni-ambazo zinakulinda dhidi ya mimba kwa mwezi moja.
Sindano yenye projestini pekee
Sindano hii ina projestini, homoni bandia inayofanana na homoni ya projesteroni inayopatikana kiasili kwenye mwili wa mwanamke. Inaweza kudungwa moja kwa moja kwenye misuli (ndani ya misuli) au chini ya ngozi (subcuntaneous). Kuna aina mbili za sindano zenye projestini pekee [2].
NET-EN au sindano ya uzuiaji mimba ya miezi miwili.
Sindano hii ya muda mfupi inalinda dhidi ya mimba kwa miezi miwili. Inaweza kutumika na wanawake ambayo wenzi wao wamefanya vasektomi na wangoja ianze kufanya kazi kwa ufanisi, wanawake ambao wamepata chanjo ya rubella na wanangoja mwili upate kinga, au kwa hali yoyote inayoweza kuzuia mtu kutumia njia ya uzuiaji mimba ya muda mfupi au muda mrefu ambazo madhara yake yanaweza kupinduliwa. NET-EN pia inapatikana kwa jina Norigest, Noristerat, na Syngestal.
DMPA au sindano ya uzuiaji mimba ya miezi mitatu.
Inakupa kinga kwa miezi mitatu. Inapendekezwa kwa matumizi ya muda mfupi au muda mrefu. Inaweza kudungwa kwenye misuli ama chini ya ngozi.
Sindano ya miezi mitatu ya kudungwa kwenye misuli inajulikana kwa kawaida kama “”sindano””, “”depo Provera,”” “”Depo,”” au “”Petogen.””
Sindano ya kudungwa chini ya ngozi inapatikana kwa umbo mbili-kama sindano ya mara moja, inapatikana chini ya jina la chapa Sayana Press na kama sirinji ya kudunga chini ya ngozi yenye dozi moja iliyojazwa awali inayopatikana kwa jina “”Depo-SubQ Provera 104′.Mfumo wa sindano ya mara moja ya Sayana press ina sindano ndogo ambayo ni rahisi kutumia. Kulingana na sheria za nchi yako, unaweza kundugwa sindano ya Sayan press kwenye kituo cha afya ama ujidunge mwenyewe [3].Kujifunza zaidi kuhusu sindano ya kujidunga mwenyewe tembelea injectsayanapress.org
Sindano za uzuiaji mimba zina hutumika aje?
Ukiamua kuanza kutumia sindano, kitu cha kwanza unachostahili kufanya ni kujadiliana na mtoa matibabu au mtoa huduma za afya ya jamii wako ikiwa sindano itakufaa. Utaulizwa maswali chache kubaini ikiwa njia hii itakuwa sahihi kwako. Pia utafahamishwa kuhusu kipindi cha kutarajia kinga kutoka kwa sindano, madhara yake na wakati wa kurudi kwa sindano nyingine.
Sindano ya kudungwa kwenye misuli inadungwa na mtoa matibabu, wakati sindano ya chini ya ngozi inadungwa na mtoa matibabu au na mtumiaji akiwa nyumbani kwake.
Dozi ya kwanza ya sindano ya uzuiaji mimba hudungwa lini?
- siku yoyote kati ya siku ya kwanza na siku ya tano ya hedhi yako bila haja ya kutumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba (hii ni kwa sababu unapata kinga mara hio hio)
- siku yoyote ya hedhi yako bora umetumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba, kama kondomu, kwa siku saba za kufuata.
- punde baada ya kutoa IUD (kwa hali hii, njia ya ziada ya uzuiaji mimba inahitajika).
- punde baada ya kutoa mimba baada ya kutoa mimba ya trimesta ya kwanza au ya pili au wakati mwingine baadaye.
- wakati wowote baada ya kuzaa au hata mapema kwa wanawake ambao hawanyonyeshi [4].
Ni kwa sehemu gani ya mwili sindano itadungwa?
Sindano kwenye misuli ya DMPA.
Inadungwa kwenye sehemu ya juu ya mkono, kwenye nyonga au kwenye makalio. Wakati huo huo, sindano chini ya ngozi hudungwa chini tu ya ngozi kwa tumbo, nyuma ya sehemu ya juu ya mkono,au sehemu ya mbele ya paja.Ikiwa kuna chaguo ya kujidunga, mtoa matibabu wako atakupa maagizo yanayohitajikaa [5].
Sindano ya NET-EN (sindano ya miezi miwili).
Hii ni sindano kwenye misuli ya kina inayodungwa kwenye sehemu ya juu ya mkono, nyonga au makalio na inaweza kuwa chungu zaidi kushinda sindano ya DMPA kwenye misuli.
Sindano ya kila mwezi
Hii pia ni sindano kwenye misuli ya kina inayodungwa kwenye sehemu ya juu ya mkono, nyonga au makalio au kwenye sehemu ya nje ya paja.
Ni mapema au kuchelewa kiasi gani ninaweza kudungwa sindano?
Kuchelewa kupata sindano kunaweza kupunguza ufanisi wa njia hii ya uzuiaji mimba. Ikiwa kuna uwezo utasahau siku yako ya kudungwa sindano, weka ukumbusho kwenye simu yako au kalenda ili uweze kuifuatilia. Ikiwa hautaweza kuenda kudungwa sindano siku iliyopangwa, kuna muda wa mwisho wa mapema au wa kuchelewa ya kudungwa sindano ya uzuiaji mimba.
Kwa DMPA (sindano ya mwezi)
Unaweza kudungwa sindano wiki mbili kabla ya siku iliyopangwa kwa sindano au wiki nne baada ya siku iliyopangwa kwa sindano.
Kwa NET-EN ( sindano ya miezi miwili).
Unaweza kudungwa sindano wiki mbili kabla au baada ya siku iliyopangwa kwa sindano.
Kwa Sindano ya kila Mwezi
Unaweza kudungwa siku saba kabla au baada ya siku iliyopangwa kwa sindano.
Wanawake wanaopendelea kutumia(DMPA (Depo au sindano ya miezi mitatu) kama njia ya uzuiaji mimba ya muda mrefu
Ikiwa unapendelea kutumia DMPA kama njia ya uzuiaji mimba ya muda mrefu, inapendekezwa kwamba uende uangaliwe kila miaka miwili ili kutathmini hali yako na kujadiliana kuhusu hatari na manufaa. Wale wamefika umri wa miaka 50 wanashauriwa kubadilisha na kutumia njia tofauti, lakini ikiwa wangependa kuendelea, kwanza wanapaswa kutathminiwa kujua hatari zinazoweza kutokea na washauriwe inavyopaswa.