Ufanisi wa sindano ya kudhibiti mimba
Aina zote za sindano zina ufanisi wa kutoa kinga dhidi ya mimba. Hata hivyo, lazima ukumbuke kudungwa sindano mara kwa mara na kwa saa. Ikitumika mara kwa mara, sindano za kila mwezi zina ufanisi wa asilimia 97 kwa kukinga mimba, na sindano za projestini zina ufanisi wa asilimia 96. Hatari ya kushika mimba pia huongezeka ukikosa sindano.
Manufaa mengine ya sindano ya kila mwezi ni kama yale ya tembe mchanganyo. Tofauti moja tu ni athari ya njia hizi mbili kwa ini. Kwa sababu sindano haichukuliwi kupitia mdomo, kuna ushahidi kwamba ina athari ndogo sana kwa ini. [7].
Manufaa maalum ya sindano ya projestini pekee
Manufaa ya afya
Zinafaa wanawake ambao hawawezi kutumia njia ya uzuiaji mimba yenye estrojeni.
Zinaweza kutumika kipindi chote mwanamke ananyonyesha, kuanzia wiki sita baada ya kuzaa.
DMPA
- ni chaguo nzuri kwa wanawake wenye shinikizo la juu la damu 160/110 mm Hg:
- inaweza kusaidia kupunguza makali ya ugonjwa wa selimundu kwa wanawake wanao ugua ugonjwa wa selimundu
- inaweza kupunguza dalili (hedhi isiyotabirika, maumivu kwenye fupa nyonga) ambazo zina uhusiano na ungonjwa wa endometriosis;
- inaweza kusaidia kutoa kinga dhidi ya saratani ya mji wa mimba;
- inaweza kusaidia kutoa kinga dhidi ya uvimbe kwenye mji wa mimba (fibroids);
- inaweza kusaidia kutoa kinga dhidi ya anemia ya upungufu wa madini ya chuma; na
- inaweza kupunguza kuwepo kwa degedege kwa wanawake walio na kifafa [8]
kando ya kutoa kinga dhidi ya mimba na hatari zinazohusiana, NET-EN:
- inaweza kusaidia kutoa kinga dhidi ya anemia ya upungufu wa madini ya chuma; na
- inaweza kutoa manufaa sawa na yale ya DMPA.
Manufaa kwa mtindo wa maisha
Sindano ni chaguo nzuri kwa wale wanaotafuta njia ya uzuiaji mimba ya muda mfupi. Sindano itakupa kinga kwa wiki 4 hadi wiki 13.
Kazi yake ni rahisi. Unahitaji tu kukumbuka kudungwa sindano mara kwa mara (kulingana na aina). Hautakuwa na wasiwasi wa kufanya chochote kabla ya ngono.
Sindano za projestini pekee haziathiriwi na dawa.
Sindano inaweza kuwa chaguo bora ikiwa hautaki kumeza tembe kila siku. Unapaswa kukumbuka tu kuenda kwenye kituo chako cha afya kwa sindano.
Haikatizi ngono.
Ina faragha. Hakuna atakaye jua kwamba umedungwa sindano. Hakuna pakiti na hakuna kitu unapaswa kufanya kabla ya ngono.
Je, antibayotiki itaathiri sindano ya uzuiaji mimba?
Rifamycin antibiotics. Antibayotiki nyingi hazipunguzi ufanisi wa njia za uzuiaji mimba zenye homoni. Isipokuwa tu Rifamycin antibiotics. Zinajumuisha rifabutin, rifapentine, na Rifampicin. Hizi ni dawa ambazo kwa kawaida zinatumika kutibu maambukizi ya bakteria, lakini hasa Kifua kikuu. Antibayotiki za Rifamycin zinajulikana kuchochea uzalishaji wa enzaimu kwa kiwango cha juu na hii huathiri viwango vya homoni kwa damu ya mtu. Kutumia antibayotiki ya Rifamycin wakati unatumia sindano mchanganyao inapunguza ufanisi wa njia hii ya uzuiaji mimba yenye homoni na kukuweka katika hatari ya kushika mimba. Hizi antibayotiki haziathiri ufanisi wa sindano zenye projestini pekee.
Ikiwa unatumia antibayotiki ya Rifamycin wakati unatumia njia mchanganyo ya uzuiaji mimba, tumia njia ya uzuizi kama kondomu au dayaframu wakati wa matibabu yako na kwa siku 28 zaidi baada ya kumaliza matibabu. Ikiwa matibabu yako yanapaswa kuendelea zaidi ya miezi miwili, jadiliana na mtoa matibabu wako kuhusu kubadilisha na kutumia njia tofauti ya uzuiaji mimba.
Kuna uwezo mgani wa kushika mimba baada ya kuwacha sindano za kudhibiti mimba?
Mara umewacha kuzitumia, sindano za uzuiaji mimba zinajulikana kuchelewesha urutubisho wa uzazi, na utangoja kwa muda mrefu kabla ushike mimba. Kwa kawaida, ukitumia DMPA utangoja karibu miezi 4-12, na ukitumia NET-EN na sindano za kila mwezi utangoja mwezi moja ukilinganisha na njia zingine za uzuiaji mimba. Wanawake ambao wanawacha kutumia sindano za uzuiaji mimba wanapaswa kutumia njia ya uzuiaji mimba tofauti mara moja hata ikiwa hedhi yao haijarudi [6].
Je sindano ya uzuiaji mimba husaidia kupunguza chunusi?
Tofauti na njia za uzuiaji mimba zenye homoni zingine kama vile pete ya ukeeni, Kiraka cha uzuiaji mimba, na tembe mchanganyo, sindano ya uzuiaji mimba haisaidi, kupunguza chunusi. Ikiwa unapata chunusi kwa urahisi, ni muhimu kujadiliana na mtoa matibabu wako kuhusu chaguo zako za uzuiaji mimba.