- ikiwa una ugonjwa za ini kama uharibifu wa ini au saratani ya ini.
- ikiwa umekuwa na ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya miaka 20 na imeathiri ateri, macho, figo au mfumo wako wa neva;
- ikiwa umewahi kupata kiharusi, damu kuganda kwa miguu au kwenye mapafu, mshtuko wa moyo au matatizo mengine mazito ya moyo;
- ikiwa una, au umewahi kuwa na saratani ya matitii;
- ikiwa una hali ambazo zinaweza kuongeza vyanzo vya kupata ugonjwa wa moyo (ugonjwa wa ateri ya moyo)au kiharusi, kama vile umri mkubwa, uvutaji sigara, shinikizo la juu la damu au ugonjwa wa sukari;
- ikiwa un umri wa miaka 35 au zaidi na unavuta sigara zaidi ya 15 kwa siku; na
- ikiwa umejifungua na maziwa ya matiti ndio chakula pekee ya mtoto wako, unaweza tu kutumia sindano yenye projestini pekee baada ya wiki sita na sindano ya kila mwezi baada ya miezi sita. Lakini ikiwa haunyonyeshi, unaweza kupata sindano ya kila mwezi baada ya wiki tatu bora hauna hatari juu yake kama vile
Ikiwa una hali zozote zilizotajwa hapa juu, onge na mtoa matibabu aliyehitimu akupe muongozo wa njia bora kwako.