Madhara ya sindano ya uzuiaji mimba

Madhara ya sindano ya uzuiaji mimba
Madhara ya sindano ya uzuiaji mimba

Madhara ya sindano yanayotokea sana ni mabadiliko kwenye mzunguko wa hedhi kwa watumiaji. Kama tu vile inavyotokea na njia za uzuiaji mimba zenye homoni, sindano tofauti zitakuwa na athari tofauti kwa miili tofauti.Ikiwa unapendelea kupata hedhi inayotabirika,utajiuliza ikiwa aina ya sindano umechagua itakuruhusu uwe na hedhi za kutabirika. Mabadiliko ya kutarajia kwa kawaida yatalingana na aina ya sindano unayotumia.

Je sindano ya kudhibiti mimba husimamisha hedhi?

Watumiaji wa DMPA:

Unaweza kupata hedhi isiyotabirika au hedhi inayokuja kwa muda mrefu ndani ya miezi mitatu ya kwanza; na, baada ya mwaka, hedhi inayokuja mara chache au ukose hedhi kabisa.

Watumiaji wa NET-EN:

Unaweza kukuwa na hedhi inayoathiriwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na DMPA kwa kukuwa na siku chache za hedhi ndani ya miezi sita ya kwanza na hedhi ya kila mwezi baada ya mwaka.

Watumiaji wa sindano ya kila mwezi:

Unaweza kupata hedhi nyepesi na inayokuja siku chache zaidi; ziwe za siku chache, zisizotabirika, au hedhi ya muda mrefu, au ukose hedhi kabisa.

Ukikosa kupata hedhi ya kila mwezi baada ya mwaka moja ya matumizi ya sindano, usiwe na hofu! Mabadiliko haya kwa hedhi ni kawaida na hayana hatari. Hata hivyo, ikiwa umechelewa kupata sindano zako na unashuku kwamba una mimba, pima mimba haraka iwezekanavyo. Ikiwa mabadiliko kwa hedhi yanakupa wasiwasi, unapaswa kuongea na mtoa matibabu wako kwa ushauri kuhusu chaguo zingine ambazo hazitakupa wasiwasi.

Madhara zaidi ya sindano ya uzuiaji mimba

Madhara yasiyo ya kawaida ya sindano ya uzuiaji mimba yanajumuisha:

  1. Kuumwa kichwa,
  2. kizunguzungu
  3. mabadiliko kwa tamaa ya ngono
  4. msongo wa mawazo
  5. kupoteza nywele au kupata nywele nyingi zaidi kwenye uso na mwili,
  6. mabadiliko ya hisia
  7. ulaini wa matiti, na
  8. tumbo kujaa na kusumbua

Hakuna njia ya kusimamisha madhara ya sindano. Ukihisi kwamba madhara ni zaidi na vile unaweza kuvumilia, zingatia kubadilisha na kutumia njia tofauti.

Mbona natokwa damu wakati ninatumia sindano ya kudhibiti mimba?

Ikiwa unatumia DMPA, kuna uwezo mkubwa kwamba utapata mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi ikilinganishwa na aina zingine za sindano. Kwa mujibu wa Pfizer, asilimia 54 ya watumiaji wa DMPA wanaweza kutokwa damu isiyotabirika au matone ya damu ndani ya mwaka wa kwanza, ilhali asilimia 32 wanaweza pata haya hadi kwa miaka miwili. Ukiendelea kutumia DMPA kwa muda mrefu, kuna uwezo matone ya damu yatapungua.

Je, sindano ya kudhibiti mimba husababisha uzito wa mwili kuongezeka?

kwa kawaida mwanamke huongeza kilo moja au mbili kwa mwaka, lakini wanawake wengine hupoteza uzani au wasipoteze uzani wowote. Wanawake kutoka Asia kwa kawaida hawaongezi uzito kwa kutumia DMPA.[9]
Wanawake wanaoongeza uzani ndani ya miezi sita ya kwanza ya matumizi wanaweza kuwa katika hatari ya kuendelea kuongeza uzito wakati wanatumia sindano. Ingawa wanawake wengine hawatapata wasiwasi kuhusu hii, wengine hawatafurahi. Ikiwa unataka kuepuka kuongeza uzani, fanya mazoezi kila siku au ongea na mtoa matibabu wako kuhusu vyakula unavyokula.

Je sindano ya kudhibiti mimba inaweza kusababisha utasa?

Hapana. Lakini wale wanaowacha kutumia sindano ili washike mimba wanaweza kuchelewa kushika mimba. Wanawake wanaowacha kutumia Depo ili washike mimba wanaweza kungoja hadi zaidi ya mwaka moja.Depo ina homoni inayopaswa kukukinga dhidi ya mimba kwa hadi miezi mitatu kwa kusimamisha kupevuka kwa yai. Ingawa homoni hii huwacha kufanya kazi baada ya miezi mitatu, mabaki yake husalia kwenye tishu za misuli kwa muda mrefu zaidi na huchelewesha urutubisho. kwa wastani, inachukua miezi 4-12 baada ya kuwacha sindano ya depo kuanza kupevuka kwa yai tena. Hata hivyo, watu wengine wataenda hadi miaka miwili kabla washike mimba. Haishauriwi utumie depo ikiwa unataka kushika mimba karibuni.

Je, sindano ya kudhibiti mimba ni salama kwa kiasi gani?

kama njia za uzuiaji mimba zingine zenye homoni, sindano za kudhibiti mimba ni njia salama ya kuzuia mimba na pia ina uwezo wa kuleta hatari ikijumuisha:

  • Kupoteza densiti ya mifupa. Kutumia Depo-Provera huathiri viwango vya estrojeni ya asili mwilini mwako, na hii inaweza kusababisha mifupa yawe nyembamba. Hali hii, hatahivyo, itapinduka mtu akiwacha kutumia njia hii ya uzuiaji mimba.
  • Kuna kudungwa sindano. Ikiwa unaogopa sindano, basi sindano ya uzuiaji mimba haitakufaa.
  • Kuna hatari ndogo ya kupata maambukizi sehemu iliyodungwa. Kwa hali nadra, watu wengine huwa na mzio wa sindano.
  • Haikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs)

Je unaweza kuondoa dawa ya sindano ya kudhibiti mimba mwilini?

Homoni zinazopatikana kwenye sindano hazina sumu. Na hakuna sababu ya kisayansi inayojulikana au njia ya kuondoa homoni za njia za uzuiaji mimba mwilini. Punde kipindi cha ufanisi kimepita, nguvu ya homoni huanza kuisha mwilini. Ingawa hii inaweza kuchukua muda mrefu zaidi na DMPA, ni salama kabisa na mchakato wa kawaida ambayo haihitaji aina yoyote ya uingiliaji kati. Lakini ikiwa unataka athari ya sindano mwilini ipungue haraka, kula vyakula bora, fanya mazoezi, epuka sigara na pombe na upate usingizi wa kutosha.

Contraception Quiz

Not sure on the method? - Take our dynamic Contraception Quiz.
When it comes to sex, protection is as important as pleasure. But what should one do to start their safe sex journey? Answer some simple questions and based on the responses, we will recommend the next steps.

Take the quiz
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...