IUD ya Homoni ni nini?
Njia ya uzuiaji mimba ambayo ni kifaa chenye homoni cha ndani ya mji wa mimba (IUD) , pia inayojulikana kama kifaa cha ndani ya mji wa mimba chenye levonorgestrel, ni njia ya uzuiaji mimba ya muda mrefu ambayo imebeba homoni ya progestin inayojulikana kama levonorgestrel.
Njia hii ya uzuiaji mimba,huwa ni kifaa kidogo cha plastiki chenye umbo wa herufi T.Kwa kawaida, inaingizwa ndani ya mji wa mimba kupitia uke na shingo ya kizazi na mtoa matibabu aliyehitimu.
IUD ya Homoni hufanya kazi vipi?
IUD Ya Homoni:
-Hufanya bitana ya mji wa mimba kuwa nyembamba zaidi na ute wa shingo ya kizazi kuwa nzito zaidi. Mazingira hii huzuia manii kurutubisha yai.
-Huzuia ovari kuwachilia yai kwahivyo hakuna cha kurutubisha [1].
IUD yenye homoni inaweza kuingizwa wakati wowote, hata kwa wanawake wanaonyonyesha na wasio nyonyesha, punde baada ya kutoa mimba. Pia inaweza kuingizwa ndani ya saa 48 baada ya kujifungua, hata baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji, ambapo hio huingizwa mara kabla ya kufunga mji wa mimba [2].
IUD ya Homoni hudumu kwa muda gani?
Kulingana na aina, IUD ya Homoni inaweza kutoa kinga hadi miaka tatu,tano au saba.Katika nchi zingine, matumizi ya aina ya Mirena inaweza idhinishwa kuenda hadi miaka nane [3].