Unaweza ingiziwa IUD ya homoni wakati wowote wa mwezi. Watoa matibabu wengine hupendelea kuiingiza wakati wa hedhi, kwasabu ni wakati huo shingo ya kizazi huwa imepanuka, lakini wakati wowote ni sawa, ilimradi hauna mimba [4].
Ni kwa njia gani unajitayarisha kwa uingizaji wa IUD ya Homoni?
Hatua ya kwanza ya kupata IUD ya homoni ni kuzungumza na mtoa huduma za matibabu wako. Utaulizwa maswali na upimwe shingo ya kizazi kuchunguza ikiwa IUD itakufaa[4].
vipimo vitakavyofanywa kabla ya uingizaji wa IUD vinaweza kujumuisha vipimo vya magonjwa ya zinaa. Mara itabainiwa kwamba hauna mimba na maradhi yoyote,mtoa huduma za afya wako atakuomba ulale chali na uweke mguu kwenye stuli ya kuwekelea mguu. Hili ni sawa na na hali yoyote ya kuchunguza kizazi,; Ili kuwepo na faragha, utafunikwa kwa shuka sehemu ya chini ya mwili wako. Mtoa matibabu wako atachunguza fupanyonga kwa kutumia vidole. Hii itamsaidia kujua umbo , ukubwa na nafasi ya mji wa mimba na ovari zako. Ili usihisi vibaya wakati wa mchakato huu, mtoa matibabu anaweza kukuomba utumie dawa ya kutuliza maumivu au akudunge sindano ya ganzi karibu na shingo ya kizazi.
Utaratibu wa Uingizaji wa IUD ya Homoni huchukua muda gani?
Utaratibu wa kuingiziwa IUD kwa kawaida huchukua dakika 5-10. Mtoa matibabu atakueleza utaratibu na kukuonyesha IUD ya Homoni na kifaa kitakacho tumika kwenye utaratibu wa kuiingiza.Ataingiza kifaa cha speculum kwenye uke wako ili kushikilia shingo ya kizazi ubaki wazi.Hatua ya pili itakua kusafisha uke na shingo ya kizazi kwa kutumia antiseptiki. Mtoa matibabu kisha atatumia kifaa maalum cha uingizaji kuweka IUD kwenye mji wako wa mimba. Wakati IUD imeingia mahali pake,kifaa cha uingizaji kinatolewa na nyuzi za IUD kukatwa kufikia urefu unaofaa, kisha kifaa cha speculum kinatolewa. Mtoa matibabu atakuambia wakati uingizaji umekamilika na kwa kawaida atakuomba upumzike kwa muda, na uketi taratibu na uvae tu wakati utahisi uko sawa. Kisha utaelezwa ni kipi cha kutarajia cha kufuata.
Ni kipi cha kutarajia baada ya uingizaji wa IUD ya Homoni?
Ni kawaida kuhisi maumivu ya hedhi na maumivu kwenye mgongo ukiwa na IUD, lakini maumivu yataisha ukipumzika au ukitumia dawa ya kutuliza maumivu. Wanawake wengine wanaweza kuwa na kizunguzungu, kwa hivyo kupanga kupumzika baada ya utaratibu wa uingizaji ni muhimu. Pia , tarajia kutokwa matone ya damu au kutokwa damu mara baada ya uingizaji. Ingawa uingizaji wa IUD sio utaratibu mgumu, sheria katika nchi yako zinaweza kuhitaji kwamba uwe na mtu ambaye anaweza kukupeleka nyumbani. Thibitisha hili na mtoa matibabu wako wakati unapanga miadi yako. Hata hivyo, hata mahali sio lazima, kukuwa na mtu wa kukupeleka nyumbani kutakuruhusu kupata muda mzuri wa kupona bila madhara mara baada ya uingizaji.
Je, ni kwa muda gani maumivu ya hedhi hudumu baada ya uingizaji wa IUD ya Homoni?
Kuna uwezekano utahisi maumivu ya tumbo baada ya uingizaji.Kwa watu wengine, maumivu huenda yakazidi maumivu ya tumbo ya hedhi,lakini kwa kawaida yataisha ndani ya dakika 2. Unaweza kupata maumivu ya tumbo na uchungu kwa siku zingine kadhaa. Hii inaweza kutulizwa kwa urahisi kwa dawa ya kutuliza maumivu kama vile ibuprofen au paracetamol.
Je, ni kwa muda gani unatokwa damu baada ya uingizaji wa IUD ya Homoni?
Ni kawaida kuwepo na mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi baada ya kuingiziwa IUD, lakini hali hii kwa kawaida hupungua ndani ya miezi tatu hadi sita. IUD za Homoni zinajulikana kufanya maumivu ya hedhi yapunguwe na hedhi kuwa nyepesi. Watu wengine nao wameripoti kutopata hedhi baada ya miaka 1 hadi 2. Ikiwa mabadiliko kwenye mzunguko wa hedhi yatakuwa zaidi ya kiwango unaweza kuvumilia, jadiliana na mtoa matibabu wako kuhusu chaguo zako.
Je, ni kwa njia gani utachunguza sehemu iliyoko IUD ya Homoni?
Mara IUD iko ndani, unaweza kuona uzi ndogo ukining’inia karibu nchi mbili kutoka kwenye mji wa mimba hadi sehemu ya juu zaidi ya uke wako (uzi hauning’ini nje ya uke). Uzi uko hapo kuwezesha IUD kutolewa baadaye [6].Mara IUD iko ndani, angalia ikiwa nyuzi zina ning’inia mara chache kwa mwaka kuhakikisha kwamba IUD iko mahala pake.
-Nawa mikono kwa sabuni na maji, kisha keti au chuchumaa.
-Weka kidole chako kwenye uke wako hadi uguse shingo ya kizazi, ambayo itakuwa imara na kuhisi kama mpira, kama vile ncha ya pua yako.
-tafuta nyuzi. Ukizipata, hongera! IUD yako iko sawa. Lakini ukigusa sehemu mgumu wa IUD kwenye pande za shingo ya kizazi, unaweza kuhitaji irekebishwe au ibadilishwe na mtoa matibabu wako.
-usivute nyuzi! Ukifanya hivyo, IUD inaweza kutoka pahali pake.
-ikiwa huwezi tafuta nyuzi peke yako,unaweza mwacha mtoa matibabu wako afanye hivyo mwezi baada ya kuingiziwa, kisha kila mwaka baada ya hapo.
Ili kupunguza hatari ya kuwepo maambukizi,utapewa mawaidha na mtoa matibabu wako kuepuka,vikombe vya hedhi,tamponi, ngono kwenye uke, kuoga(ikiwa umejizamisha kwa maji), na kuogelea kwa angalau saa 24 baada ya uingizaji.
Imependekezwa pia kwamba ushauriane na mtoa matibabu wako mara moja ikiwa kama ndani ya siku 20 baada ya uingizaji wa IUD, utakuwa na dalili hizi ambazo sio za kawaida.
Ute wa ukeeni usio wa kawaida;
joto/baridi;
Uchungu mkali wakati wa ngono;
kichefuchefu na/ama kutapika; na
maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo yako.
Dalili hizi huenda zikawa ishara ya ugonjwa wa uvimbe kwenye fupanyonga(PID). PID hutokea wakati IUD imeingizwa ndani ya mtu aliye na kisonono au klamidia. Isipokuwa unataka IUD itolewe, mtoa matibabu wako anapaswa kuweza kutibu IUD na maambukizi mengine ya zinaa, bila kutoa IUD.Lakini ikiwa PID haitatibiwa kwa dawa, utashauriwa utoe IUD, kisha uendelee na matibabu. Ni vyema kutumia kondomu wakati wa matibabu wa kisonono na klamidia kisha ubadilishe na utumie njia ya uzuiaji mimba tofauti ikiwa umetolewa IUD wakati wa matibabu. IUD inaweza kuingizwa tena baada ya kutibiwa PID.
IUD ya Homoni huanza kufanya kazi lini?
Ikiingizwa siku saba za kwanza za hedhi, IUD ya Homoni mara moja itakuwa na ufanisi wa kuzuia mimba.Ikiingizwa wakati mwinge wowote wa hedhi, itakuwa na ufanisi siku saba baada ya uingizaji.
Mtu anaweza jamiiana baada ya muda gani baada ya uingizaji wa IUD ?
Mara tu IUD imeingizwa, unaweza jamiiana punde unavyotaka.Hata hivyo, ikiwa IUD haiikuingizwa wakati wa hedhi yako, unapaswa kutumia njia ya uzuiaji mimba ya ziada kwa siku saba, unapongoja IUD iwe na ufanisi.
Ni wakati gani naweza kutumia tamponi baada ya uingizaji wa IUD?
Ili kupunguza hatari ya kuwepo maambukizi, inapendekezwa kwamba ungoje angalau saa 24 baada ya uingizaji kabla ya kutumia tamponi, kufanya ngono kwenye uke au kuoga.