Wakati Homoni ya IUD ni mojawapo wa njia za uzuiaji mimba yenye ufanisi zaidi, huenda haitawafaa watu ambao wana hali mbalimbali ambazo zinahitaji upungufu wa matumizi ya homoni ya progestini.
Huenda IUD ya Homoni haitakufaa ikiwa:
Una ugoonjwa ya damu kuganda kwenye mishipa ya kina
Umegunduliwa kuwa na saratani kali ya ini, uvimbe kali kwenye ini, na kuharibika kwa ini;
Unaugua ama umewahi ugua saratani ya matiti;
Unatokwa damu kwenye uke kwa njia isiyo elezeka-daktari wako atahitaji kuchunguza chanzo cha hili kabla uingiziwe IUD; na
Una hali ya magonjwa ya uke kama vile kifua kikuu ya fupanyonga au saratani ya uke.
Ikiwa una hali zozote zilizotajwa hapo juu, tafadhali muone mtoa matibabu aliyehitimu. Utashauriwa kuhusu njia bora zaidi ya uzuiaji mimba itakayokufaa [10].