Manufaa ya kiafya
IUD za Homoni zinajulikana kuwa na manufaa mengi ya kiafya yakijumuisha:
-kutoa kinga ya asilimia 99 dhidi ya mimba.IUD ya Homoni ni moja wapo wa njia za uzuizji mimba zilizo na ufanisi-Watu 99 kwa watu 100 wanaotumia njia hii wataweza kuzuia mimba.
-Kuna uwezo wa kupunguza uwezo wa kupata saratani ya shingo ya kizazi au saratani ya mji wa mimba (ndani ya mji wa mimba)
-kupunguza makali ya maumivu ya hedhi na hedhi nzito.
-kupunguza hatari ya mimba nje ya mji wa mimba.
-kupunguza dalili zinazoletwa na ugonjwa wa endometriosis, ikijumuisha kutokwa damu isiyotabirika na maumivu kwenye fupanyonga.
-Kinga dhidi ya anemia ya upungufu wa madini ya chuma
Manufaa kwa mtindo wa maisha
IUD kama njia ya dharura ya uzuiaji mimba
Takwimu mpya zimeonyesha kwamba IUD ya Homoni (52mg LNG) ni njia ya dharura ya uzuiaji mimba yenye ufanisi ikiingizwa ndani ya saa 120 (siku 5) baada ya kufanya ngono bila kinga [8].
Ni salama kwa miili yote ya wanawake
IUD ya Homoni ni salama kwa miili ya wanawake wengi ikijumuisha;wasichana balehe na wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40. Wataalamu wengi wanakubali kwamba ikiwa una afya na una mji wa mimba, kuna uwezo kwamba utatumia IUD, na ni ukweli hata ikiwa wewe ni kijana, haujawahi kuwa na mimba au kuwa na watoto, umetoka tu kutoa mimba au mimba imeharibika (ili mradi hautibiwi kwa maambukizi),umewahi kuwa na mimba nje ya mji wa mimba, umekuwa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupanyonga hapo awali, una VVU, yenye dalili kidogo au bila dalili (unatumia / hautumii dawa za kupunguza makali ya VVU au una anemia. Pia ni njia bora kwa wanawake waliojifungua karibuni (wanaonyonyesha/wasio nyonyesha)
Ni rahisi kuficha
IUD ya Homoni ni kifaa kidogo cha plastiki chenye umbo wa herufi T ambacho kinaingizwa kwenye mji wa mimba (tumbo la uzazi),na watu wengi hawawezi kugundua kwamba iko hapo.Haina pakiti na hauhitajiki kufanya chochote kabla ya ngono. kwa viza chache sana, mwenzi anaweza gusa IUD au nyuzi zake wakati wa ngono,lakini mtoa matibabu anaweza kata nyuzi hizo kwa urahisi.
Inahitaji bidii ndogo
Iingize na uisahau.Ikiwa hautaki wasiwasi kwamba utasahau kutumia njia ya uzuiaji mimba, IUD huenda ikakufaa. Inaingizwa mara moja na hufanya kati ya miaka tatu hadi saba, kulingana na aina (ukubwa na idadi ya levonorgestrel)
Haizui ngono.
Inadumu muda mrefu bila kuhitaji mtumiaji afanye chochote.
Ni rahisi kutumia
Kwa vile uingizaji unafanywa katika kituo cha afya, hakuna pakiti wala dawa za kuchukuliwa kwenye duka la dawa.Kwahivyo, hakuna kinachoweza kupotea au kusahaulika.
Itachukua muda gani kushika mimba baada ya kutoa IUD?
Unapaswa kuweza kushika mimba haraka sana baada ya utoaji wa IUD. Ikiwa hauko tayari kushika mimba mara baada ya kutolewa IUD, hakikisha umejikinga kwa njia tofauti.
Inapatikana kwa urahisi
Ungependa kutumia njia hii?Inapatikana kwa wingi, uliza tu kwenye kituo chako cha afya.