Madhara ya IUD ya Homoni ni gani?

Madhara ya IUD ya Homoni ni gani?
Madhara ya IUD ya Homoni ni gani?

Wakati IUD ya Homoni inachukuliwa kuwa na ufanisi kiasi kushinda IUD bila Homoni, madhara yao huwa tofauti. Watumiaji wa IUD ya Homoni watapata madhara yanayohusiana na homoni, kama vile kuumwa kichwa, ambayo sio kawaida kwa watumiaji wa IUD bila homoni. Hata hivyo, wanawake huzoea IUD ya Homoni ndani ya miezi 6-8 [8].

Ni IUD ya Homoni gani huwa na madhara zaidi?

Madhara ya njia za uzuaji mimba ya IUD ya Homoni huwa tofauti kwa kila mwanamke.Wakati chapa kadha za IUD zina viwango vya homoni zaidi ya zingine, chaguo ya chapa bora zaidi kwa kila mtu itategemea sababu mbalimbali. Hizi zinajumuisha;miaka kinga inatarajiwa;ukubwa au udogo wa shingo ya kizazi mimba au ikiwa una watoto au hauna,ikiwa unataka kuendelea kupata hedhi wakati wa matumizi, na jinsi mwili wako huathiriwa na homoni za bandia, ikijumuisha sababu zingine. Gazeti la Women’s Health Magazine inaorodhesha vitu vya kutarajia kutoka kwa chapa tofauti za IUD za Homoni.

Madhara ya kawaida ya IUD ya Homoni

  1. Maumivu ya hedhi na maumivu ya mgongo kwa siku chache baada ya uingizaji .
  2. Kutokwa matone ya damu au kutokwa damu baada ya uingizaji.
  3. Mzunguko wa hedhi usiotabirika. Hii itatokea kwa kupata hedhi nyepesi, siku chache za hedhi kila mwezi, au kutopata hedhi kabisa kwa mwaka wa kwanza hadi wa pili baada ya uingizaji wa IUD ya Homoni. Kutopata hedhi haipaswi kuchukuliwa kama kukuwepo mimba. IUD za Homoni zimeripotiwa kupunguza hedhi nzito na maumivu ya hedhi na kutibu anemia.
  4. Kuumwa Kichwa.
  5. Chunusi
  6. Ulaini na uchungu wa matiti
  7. Kubadilika kwa hisia

Matatizo nadra ya IUD ya Homoni:
Maambukizi (maumivu ya fupanyonga, ute, na joto). Mara nyingi, daktari atachunguza ikiwa kuna ugonywa wa uvimbe kwenye fupanyonga (PID). PID imeripotiwa mara chache mno ambapo mwanamke alikuwa na klamidia au kisonono wakati aliingiziwa IUD. Kulingana na makali ya maambukizo, PID inaweza kutibiwa na dawa za antibayotiki, na IUD itolewe au isitolewe.
IUD inaskuma kuta za mji wa mimba.Hii inaweza kugunduliwa tu kwa kituo cha afya (kulingana na dalili maalum). Kwa hali kama hii, IUD inatolewa na mtoa matibabu aliyehitimu.
IUD kuteleza na kutoka nje.Ikiwa unashuku kwamba IUD yako inakaribia kutoka au imetoka tayari, tafuta ushauri wa mtoa matibabu aliyehitimu kwa mwongozo na utunzaji unaofaa.
Ikiwa, baada ya miezi mitatu, unahisi madhara yamezidi kiasi unachoweza kuvumilia, unaweza itoa na utumie njia ya uzuiaji mimba tofauti. Kumbuka kwamba njia ya uzuiaji mimba ya IUD ya homoni haitoi kinga dhidi ya maambukizi ya zinaa (STI)

Maswali ya kawaida kuhusu IUD ya Homoni

Unaweza kupata IUD ya Homoni ikiwa una ugonjwa wa zinaa?

Hapana. Haushauriwi kuingiziwa IUD ikiwa una ugonjwa wowote wa zinaa. Hii ni kwasababu inaweza kuleta ugonjwa wa uvimbe kwenye fupanyonga. Mtoa matibabu wako anafaa kwanza kukupa matibabu na kuhakikisha kwamba hauna ugonjwa wowote wa zinaa kabla ya kuingiza IUD.

Je, ninaweza kutumia IUD ya Homoni ikiwa ninanyonyesha?

Ndio. Kulingana na planned parenthood IUD ni njia moja salama zadi kwa mtu anayenyonyesha. Inaweza kuingizwa mara baada ya kuzaa na haitakudhuru wewe au mtoto wako

Nina maumivu ya hedhi makali kwa sababu ya IUD ya Homoni. Nifanye nini?

Ijaribu kwa miezi michache, na utumie dawa za kutuliza maumivu kama ibuprofen siku za kwanza za hedhi yako.Ikiwa unapenda urahisi wa kutumia njia ya uzuiaji mimba ya muda mrefu, lakini madhara ya IUD ya Homoni hayapungui kwa muda, zungumza na mtoa matibabu wako kuhusu kubadilisha na kutumia njia tofauti ya muda mrefu, lakini ambayo haikuletei matatizo.

IUD ya Homoni yangu ilitoka, je inaweza kutoka tena?

Kutoka kwa IUD kunawezekana kwa asilimia ndogo ya wanawake ndani ya mwaka wa kwanza baada ya kuingizwa. Kutoka kunawezekana zaidi kwa wanawake ambao:
Hawajawahi kushika mimba;
Wana umri chini ya miaka 20;
Wana historia ya kuwa na hedhi nzito au hedhi iliyo na maumivu makali;
Waliwekewa IUD punde baada ya kujifungua au mimba ilitolewa wakati wa trimesta ya pili.
IUD kusonga kidogo na kutoka eneo lake kunaweza kumaanisha kwamba IUD haikuingia sawa: Pengine ilikuwa chini sana kwenye mji wa mimba na ikasonga. Hili linaweza kuwa lilifanyika wakati wa kuingizwa au linaweza kuhusiana na umbo la mji wa mimba kama vile ukubwa,pembe, au kuwepo na uvimbe (fibroids) ambazo zinaweza kubadilisha umbo. Kwa wanawake ambao IUD ilitoka awali, kuna uwezekano mkubwa kwamba IUD ya pili pia itatoka [2].
Ikiwa unapenda urahisi wa kutumia IUD ya muda mrefu na ambayo ina kazi ndogo ya utunzaji kama vile IUD ya Homoni, lakini una matatizo ya IUD kutoka, unaweza kujaribu kutumia njia tofauti ya muda mrefu kama vipandikizi.

Je, IUD ya Homoni itamkwaruza mwenzi wangu?

Kuna uwezekano kwamba wenzi watahisi nyuzi za IUD wakati wa ngono ndani ya uke. Hii hufanyika ikiwa nyuzi zilikatwa fupi sana. Ikiwa unaamini kwamba nyuzi za IUD zinaathiri ubora wa maisha yako ya ngono, enda ukamwone mtoa matibabu wako kwa ushauri. Wakati utapewa ushauri wa kupunguza nyuzi hizo zaidi, pia utapewa onyo kwamba kukata nyuzi za IUD ziwe fupi sana inaweza fanya iwe ngumu kutoa IUD baadaye (utahitaji mtoa matibabu aliyepata mafunzo maalum kuzitoa). Chaguo ingine itakuwa kumuomba mwezi wako awe mwenye subra kidogo kwasabu hatimaye nyuzi zitakuwa laini kana kwamba hatazihisi.

Contraception Quiz

Not sure on the method? - Take our dynamic Contraception Quiz.
When it comes to sex, protection is as important as pleasure. But what should one do to start their safe sex journey? Answer some simple questions and based on the responses, we will recommend the next steps.

Take the quiz
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...