Mtu anaweza kuamua IUD itolewe kwa sababu kadhaa. Hizi hujumuisha muda wake kuisha, kuwekewa nyingine, au kubadilisha na kutumia njia tofauti ya uzuiaji mimba. Utafiti huu uliofanywa nchini Ghana na Gbagbo na Kayi unaeleza sababu za kutoa IUD. Zinajumuisha hali za kijamii na kitamaduni. Ukitaka kuwacha kutumia IUD ya Homoni kwa sababu yoyote, inapswa kutolewa na mtoa huduma ya afya aliye hitimu.
Kutoa IUD ya Homoni huchukua muda gani?
Utaratibu wa kutoa IUD ya Homoni kwa kawaida huchukua karibu dakika 2-5. Kama tu utaratibu wa uingizaji, mtoa matibabu atakuomba ulale chali na atashikilia miguu yako kwa vifaa vya stirrups. Kifaa cha speculum kitatumika kushikilia shingo ya kizazi iwe wazi kisha mtoa matibabu atatumia forceps kuvuta nje nyuzi za IUD kwa utaratibu. IUD huwa inapindika na itatoka nje kwa urahisi. Ikiwa itatokea kwamba IUD haitoki kwa urahisi, mtoa matibabu atatumia dawa kupanua shingo ya kizazi, atakutuliza kwa dawa ya kutuliza maumivu, na atumie forceps kuvuta IUD nje. Ikiwa una IUD nzee na ungependa ibadilishwe, IUD mpya itaingizwa mara moja.
Utahisi uchungu kiasi gani wakati IUD ya Homoni inatolewa?
Wakati wanawake wengine wameripoti kuhisi uchungu kiasi na maumivu ya hedhi kidogo, wengine hawakuhisi chochote. Hata hivyo, uchungu utakayohisi wakati wa utoaji ni mdogo kuliko ule utahisi wakati wa uingizaji. Uchungu wowote unayohisi siku chache baada ya utoaji unaweza kutulizwa kwa dawa ya kutuliza maumivu kama vile ibuprofen.
Je, ni kwa muda gani unatokwa damu baada ya kutolewa IUD ya Homoni?
Mtu anaweza kutokwa na damu nyepesi au kutokwa matone ya damu baada ya kutolewa IUD ya Homoni. Hili linaweza kufanyika kwa siku chache. Inapendekezwa utumie sodo za hedhi kwa angalau saa 48, unaweza kutumia aina yoyote ya sodo unayopenda, ikiwa pamoja na tamponi au vikombe vya hedhi. Hedhi nzito au hedhi (inayolowesha sodo za hedhi au tamponi zaidi ya moja kwa saa moja) na iliyo na damu nyingi iliyoganda (inayotoshana na robo au kubwa zaidi) sio kawaida. Ikiwa utapata tatizo hili, unapaswa kuwasiliana na mtoa matibabu wako mara moja.
Baada ya kutoa IUD ya Homoni, kupevuka kwa yai hufanyika lini?
Baada ya kutoa IUD ya Homoni, inaweza kuchukua hadi miezi 3 kabla mzunguko wa hedhi yako ya kawaida kuanza tena. Hata hivyo, urutubisho wa uzazi wako utarudi punde baada ya kutolewa kwa IUD. Ikiwa haujaribu kushika mimba, mtoa matibabu wako atakushauri uanze njia ya uzuiaji mimba mpya angalau siku saba kabla IUD itolewe. Hili litahakikisha kwamba tayari una njia ya kuzuia mimba iliyo na ufanisi wakati IUD inatolewa. Chaguo zingine ni kuingiza IUD mpya mara moja. Pia unaweza kutumia njia ya kuzuia manii kama kondomu hadi wakati njia ya uzuiaji mimba utakayo anza kutumia ipate ufanisi.
Ngono baada ya utoaji wa IUD ya Homoni
Ni salama kufanya ngono siku chache kabla kutolewa au baada ya kutolewa IUD. Hata hivyo, ikiwa hautoi IUD ili upate mimba, mtoa matibabu wako atakushauri kuepuka ngono au utumie kondomu ukifanya ngono au uanze kutumia njia nyingine ya uzuiaji mimba siku saba kabla kutolewa IUD. Hii ni kwasababu manii inaweza kuishi kwenye mfumo wa uke hadi siku tano na kuna uwezekano wa kupata mimba punde IUD imetolewa. Mara IUD imetolewa, unaweza ingiziwa ingine mara moja, au uanze kutumia njia nyingine ya uzuiaji mimba. Tumia njia ya kuzuia manii kama kondomu hadi njia hiyo iwe na ufanisi wa kazi.
Je, nipata hedhi yangu baada ya muda gani baada ya utoaji wa IUD ya Homoni?
Ikiwa mzunguko wako wa hedhi ulikuwa sawa kabla kuingiza IUD, tarajia mzunguko wa hedhi urudi kama kawaida baada ya IUD kutolewa. Kwa watu wengine, hedhi itarudi mara moja, na kwa wengine inaweza kuchukua hadi miezi 3.
Je, naweza kutoa IUD yangu ya Homoni nikiwa nyumbani?
Unaweza kupata hadithi mtandaoni kuhusu watu kujitolea IUD zao.Hatupendekezi ujaribu. Hakuna utafiti wa kutosha hadi sasa kueleza kama ni salama. Ikiwa haujafurahia IUD yako, kuenda kwa mtoa matibabu wako kutahakikisha kwamba utaratibu umefanywa kwa njia salama. Itakupa nafasi pia ya ya kuzungumzia chaguo zingine kuhusu uzuiaji mimba. Ikiwa uko tayari kupata mimba, unaweza kuzungumza na mtoa matibabu wako kuhusu vitu unapaswa kufanya ili ujitayarishe kwa mimba yenye afya.