IUD bila Homoni ni nini?
IUD bila Homoni pia huitwa IUD ya Shaba, ni njia ya uzuiaji mimba ya muda mrefu ambayo imeundwa na kipande kidogo cha plastiki chenye umbo wa herufi T na shaba. IUD ya shaba huingizwa ndani ya mji wa mimba kupitia uke na shingo ya kizazi. Ina nyuzi ambazo huning’inia nje ya shingo ya kizazi ili kuwezesha itolewe kupitia uke.
Je, IUD bila Homoni hufanya aje kazi?
IUD bila homoni hufanya kazi kwa kubadilisha kidogo mazingira ya kikemikali ya mji wa mimba, hali ambayo huharibu manii na yai kabla zikutane.Kulingana na aina, IUD za shaba zinaweza kutoa kinga ya miaka 3-12 dhidi ya mimba. Utafiti unaonyesha kwamba wakati IUD ya shaba (T380A) imependekezwa kwa hadi miaka 10 ya ufanisi, inaweza kubaki na ufanisi hadi miaka 12 ya matumizi. Wale ambao wanataka kushika mimba wanaweza kufanya hivyo punde baada ya kutolewa IUD [1].
Ili mradi mtu hana mimba, IUD bila homoni inaweza kuingizwa wakati wiowote hata mara moja baada ya kutoa mimba au saa 48 baada ya kujifungu.Ikiwa umejifungua kwa njia ya upasuaji, IUD hio inaweza kuingizwa mara kabla ya kufunga mji wa mimba [2].