Manufaa ya IUD ya Shaba

Manufaa ya IUD ya Shaba
Manufaa ya IUD ya Shaba

Manufaa ya Kiafya

IUD za Homoni zinajulikana kuwa na manufaa mengi ya kiafya yakijumuisha:
-kutoa kinga ya asilimia 99 dhidi ya mimba.IUD ya Homoni ni moja wapo wa njia za uzuizji mimba zilizo na ufanisi-Watu 99 kwa watu 100 wanaotumia njia hii wataweza kuzuia mimba.
-kuwa chaguo bora kwa watu ambao wanaipendelea au wale hawawezi kutumia IUD ya homoni kwa sababu za kiafya.
-kupunguza hatari ya mimba nje ya mji wa mimba.
-Kuna uwezo wa kupunguza uwezo wa kupata saratani ya shingo ya kizazi au saratani ya mji wa mimba (ndani ya mji wa mimba)
-kuwa salama kwa wavutaji sigara.
-kuwa salama kwa walio na shinikizo la damu na ugonjwa wa sukari.[8].

Manufaa kwa mtindo wa maisha

IUD ya shaba kama njia ya dharura ya uzuiaji mimba

IUD ya Shaba, ikiingizwa ndani ya saa 120/siku tano baada ya kufanya ngono bila kinga, zinajulikana kuwa njia ya dharura ya uzuiaji mimba yenye ufanisi wa juu zinazopatikana. Na baadaye, unapata kufurahia miaka ya kinga dhidi ya mimba isiyopangwa.

Ni salama kwa miili yote ya wanawake.

Ikijumuisha wasichana balehe na wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40. Wataalamu wengi wanakubali kwamba ikiwa una afya na una mji wa mimba, kuna uwezo kwamba utatumia IUD, na ni ukweli hata ikiwa wewe ni kijana, haujawahi kuwa na mimba au kuwa na watoto, umetoka tu kutoa mimba au mimba imeharibika (ili mradi hautibiwi kwa maambukizi),umewahi kuwa na mimba nje ya mji wa mimba, umekuwa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupanyonga hapo awali, una VVU, yenye dalili kidogo au bila dalili (unatumia / hautumii dawa ya kupunguza makali ya VVU), au una anemia. Pia ni njia bora kwa wanawake waliojifungua karibuni (wanaonyonyesha/wasio nyonyesha)

Haina madhara kwa homoni za mwili

IUD za shaba hazina homoni na kwahivyo, viwango vyako vya homoni havitaathiriwa.

Ina ufaragha

Njia ya uzuiaji mimba ya IUD bila homoni ni kifaa kidogo cha plastiki chenye umbo wa herufi T na shaba ambacho kinaingizwa kwenye mji wa mimba (tumbo la uzazi),na watu wengi hawawezi kugundua kwamba iko hapo.Haina pakiti na hauhitajiki kufanya chochote kabla ya ngono. kwa viza chache sana, mwenzi anaweza gusa IUD au nyuzi zake wakati wa ngono,lakini mtoa matibabu anaweza kata nyuzi hizo kwa urahisi.

Inahitaji bidii ndogo

Iingize na uisahau.Ikiwa hautaki wasiwasi kwamba utasahau kutumia njia ya uzuiaji mimba, IUD huenda ikakufaa. Inaingizwa mara moja na hufanya kati ya miaka tatu hadi saba, kulingana na aina (ukubwa na idadi ya levonorgestrel)

Ni rahisi kutumia

Kwa vile uingizaji unafanywa katika kituo cha afya, hakuna pakiti wala dawa za kuchukuliwa kwenye duka la dawa.Kwahivyo, hakuna kinachoweza kupotea au kusahaulika. Haikatizi ngono
Itachukua muda gani kushika mimba baada ya kutoa IUD ya shaba?
Unapaswa kuweza kushika mimba haraka sana baada ya utoaji wa IUD. Ikiwa hauko tayari kushika mimba mara baada ya kutolewa IUD, hakikisha umejikinga kwa njia ya uzuiaji mimba sawa au tofauti.

IUD ya shaba hudumu kwa muda gani?

Inadumu kwa muda mrefu sana bila kuhitaji bidii nyingi kwa mtumiaji

Je kuna utangamano gani kati ya tamponi na IUD bila homoni (ya shaba)?

Mtu aliye na IUD ya shaba pia anaweza kutumia tamponi, bora asivute nyuzi za IUD. Lakini inatokea mara chache sana kwamba mtu anaweza kuvuta nyuzi kimakosa kwasababu nyuzi za tamponi huwa zinaning’inia nje ya uke, wala sio ndani ya uke. Kwa hali utahisi nyuzi za IUD zikiwa karibu na nyuzi za tamponi, unapaswa kumuona mtoa matibabu wako kwasababu kuna uwezo kuwa IUD pengine imetoka kwenye mji wa mimba.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...