Uingizaji wa IUD bila homoni (Shaba)

Uingizaji wa IUD bila homoni (Shaba)
Uingizaji wa IUD bila homoni (Shaba)

Mtoa matibabu aliyehitimu kwa kawaida huingiza IUD bila homoni ukiwa kwenye kituo cha afya. Hata ikiwa unaweza kuinunua kwenye duka la dawa, lazima uende kwenye kituo cha afya ili iingizwe. Ilhali inaweza kuingizwa wakati wowote wa mwezi, watoa matibabu wengine watapendelea kuiingiza wakati wa hedhi kwasababu watakuwa na uhahika kwamba hauna mimba. Kuongezea, shingo ya kizazi huwa imepanuka wakati wa hedhi, na kufanya uingizaji wa IUD uwe rahisi. [4].
Hautahitaji kipindi cha mapumziko baada ya kutolewa IUD ambayo tarehe yake ya mwisho wa matumizi imefika. IUD ya shaba inaweza kuingizwa punde baada ya kutolewa kwa ile mzee,mara baada ya kujifungua au baada ya kutoa mimba au hata kama njia ya dharura ya uzuiaji mimba (ndani ya siku 5 ya kufanya ngono bila kinga).

Jinsi ya kujitayarisha kwa uingizaji wa IUD ya Shaba?

Hatua ya kwanza ya kupata IUD ya Shaba nikujadiliana na mtoa matibabu wako ikiwa IUD ya shaba itakufaa. Utaulizwa maswali ambayo yatasaidia kugundua ikiwa una majongwa yoyote ya zinaa, mzio wa shaba au hali yoyote ile ambayo inaweza kukuzuia kutumia IUD ya shaba. Utaombwa kupimwa kwenye maabara ikiwa kutakuwa na sababu ya kushuku kuna maambukizi. Pia utapimwa fupanyonga kuhakikisha kwamba IUD inakufaa.[3].Punde inapobainiwa kwamba IUD itaakufaa, mtoa matibabu atakupa dawa ya kutuliza maumivu kukusaidia kwa maumivu yoyote utakayohisi wakati wa uingizaji na baada ya uingizaji. Kwa kawaida utapewa hizi dawa dakika 30 kabla ya uingizaji. Vinginevyo, mtoa matibabu atakudunga sindano ya ganzi kwenye shingo ya kizazi.

Ni nini utaratibu wa uingizaji wa IUD ya Shaba?

Kama tu hali yoyote ya kuchunguza kizazi, mtoa matibabu atakuomba ulale chali ili uingiziwe IUD. Miguu yako yatabebwa juu kwa kutumia vifaa vya stirrups. Kisha shuka itatumika kufunika mwili wako. Mtoa matibabu wako atakueleza kila hatua ya utaratibu na pia kukuonyesha vifaa atakavyo vitumia kwa uingizaji, ikiwemo IUD ya shaba yenyewe. Kifaa kinachojulikana kama speculum kitaingizwa kwenye uke ili kushikilia shingo ya kizazi ibaki wazi. Mtoa matibabu kisha atasafisha uke na shingo ya kizazi kwa kutumia antiseptiki. Hii itasaidia kuzuia maambukizi yanayoweza kutokea kutokana na uingizaji.IUD ya shaba itaingizwa katika uke kwa kutumia kifaa maalum cha uingizaji.Punde IUD imeingia, kifaa cha uingizaji kinatolewa na nyuzi za IUD kukatwa kufikia urefu unaofaa, kisha kifaa cha speculum kinatolewa. Mtoa matibabu kisha atakata nyuzi za IUD ifike urefu wa kufaa. Mara hili limefanyika, kifaa cha speculum kitatolewa.
Wanawake wengine wameripoti kuhisi maumivu ya hedhi wakati wa uingizaji. Wengine huhisi uchungu kiasi. Uchungu wa uingizaji kwa kawaida utaisha ndani ya dakika mbili. Unaweza pia kutulizwa kwa dawa za kutuliza maumivi kama vile paracetamol na ibuprofen. Mtoa matibabu atakujulisha mara uingizaji umekamilika na atakuomba upumzike. Ukiwa tayari, utashauriwa uketi taratibu na uvae. Mtoa matibabu kisha atakupa taarifa zaidi kuhusu ni kipi cha kutarajia na ni lini kuenda kwa uchunguzi (kwa kawaida wiki 3-6 baada ya uingizaji).

Ni kipi cha kutarajia baada ya uingizaji wa IUD ya shaba?

Mara nyingi, uingizaji wa IUD sio mchakato mgumu na unapaswa kuwa na uwezo wa kurudi kwa shughuli zako za kila siku punde baada ya uingizaji. Watu wengine hata hivyo watapata shinikizo la chini la damu, kizunguzungu, kichefuchefu na moyo kupiga polopole baada ya uingizaji lakini ni nadra wazimie. Wengine hupata maumivu baada ya uingizaji. Athari hizi zinaweza kupunguzwa kwa kupumzika na pia dawa za kutuliza maumivu. Katika nchi zingine, ni lazima kukuwa na mtu wa kukupeleka nyumbani baada ya uingizaji wa IUD. Hakikisha umeuliza kuhusu vitu vitahitajika kabla ya kupanga miadi yako.

Je, ni kwa njia gani utachunguza sehemu iliyoko IUD ya Shaba?

Mara IUD iko ndani, unaweza kuona uzi ndogo ukining’inia karibu nchi mbili kutoka kwenye mji wa mimba hadi sehemu ya juu zaidi ya uke wako (uzi hauning’ini nje ya uke). Uzi uko hapo kuwezesha IUD kutolewa baadaye [5].Mara IUD iko ndani, angalia ikiwa nyuzi zina ning’inia mara chache kwa mwaka kuhakikisha kwamba IUD iko mahala pake.
-Nawa mikono kwa sabuni na maji, kisha chuchumaa.
-Weka kidole chako kwenye uke wako hadi uguse shingo ya kizazi, ambayo itakuwa imara na kuhisi kama mpira, kama vile ncha ya pua yako.
-tafuta nyuzi. Ukizipata, hongera! IUD yako iko sawa. Lakini ukigusa sehemu mgumu wa IUD kwenye pande za shingo ya kizazi, unaweza kuhitaji irekebishwe au ibadilishwe na mtoa matibabu wako [6].
-usivute nyuzi! Ukifanya hivyo, IUD inaweza kutoka pahali pake.

Je, ni kwa muda gani maumivu ya hedhi hudumu baada ya uingizaji wa IUD ya Shaba?

Maumivu baada ya uingizaji wa IUD ya shaba huwa tofauti kwa mwanamke moja hadi mwingine. Kwa wengine, maumivu ya hedhi na maumivu ya mgongo yataisha ndani ya siku 1 hadi 2. Kwa wengine, yataendelea hadi hata miezi 3 hadi 6. Unaweza pata hedhi isiyotabirika na kupata maumivu ya hedhi wakati wa hedhi kwa hizo miezi 3 hadi 6.

Je, ni kwa muda gani unatokwa damu baada ya uingizaji wa IUD ya Shaba?

Kuna uwezekano utatokwa damu kwa siku 1 hadi 7 baada ya kuingiziwa IUD. Damu itakuwa nzito baada ya uingizaji lakini itapungua kwa muda.Ikiwa baada ya uingizaji utapata joto, hedhi nzito sana (inayolowesha sodo 1-2 ndani ya saa moja), au damu inayonuka, inaweza kumanisha kwamba una maambukizi. Tafuta matibabu mara moja. Ni kawaida kuona damu iliyoganda siku ya kwanza baada ya uingizaji lakini haitaendelea sana. Kutokwa matone ya damu au damu inafaa kupungua ndani ya miezi 3-6, lakini ikiendelea zaidi ya miezi 6, tafuta ushauri wa mtoa matibabu wako.

IUD ya Shaba huanza kufanya kazi kwa ufanisi muda gani baada ya uingizaji?

IUD ya shaba huanza kufanya kazi kwa ufanisi mara moja baada ya uingizaji.

Ni lini nina weza kujamiana baada ya uingizaji wa IUD ya Shaba?

Ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi inashauriwa kwamba ungoje angalau saa 24 baada ya uingizaji wa IUD ya shaba kabla ufanye ngono kwenye uke, utumie tamponi au kikombe cha hedhi, uoge (ikiwa umejizamisha kabisa kwa maji) au uogele.

Je, unaweza kushika mimba ukiwa na IUD ya Shaba?

Kuna uwezekano mdogo sana wa kushika mimba ukiwa na IUD ya Shaba. Kulingana na kitabu cha maelezo cha Family Planning Handbook for Providers, ni asilimia 1 tu ya watu wanaotumia IUD ya copper watashika mimba ndani ya mwaka wa kwanza wa kutumia IUD ya shaba. Ukishika mimba, kuna uwezekano mdogo wa mimba kutungwa nje ya mji wa mimba. Ikiwa unashuku una dalili za mapema za mimba, enda upime mimba haraka iwezekanavyo. Ikiwa itathibitisha una mimba, shauriana na mtoa matibabu wako ili kuhakikisha kwamba sio mimba nje ya mji wa mimba. Ukiwa na mimba, IUD inapaswa kutolewa ili uwe na mimba salama au unaweza kutoa mimba. Mtu akibaki na IUD ya shaba kwenye mji wa mimba wakati ana mimba, kuna hatari wa juu wa kupoteza mimba hio.

Je, IUD ya Shaba inaweza kuwa chanzo cha ugonjwa wa uvimbe kwenye fupanyonga (PID)?

Kitabu cha maelezo ya Upangaji wa Uzazi kinaeleza kwamba IUD ya shaba haisababishi ugonjwa wa uvimbe kwenye fupanyonga (PID). Hatahivyo, IUD ikiingiziwa mtu anayeugua Klamidia au Kisonono,magonjwa haya yanaweza kusababisha PID. Wakati hii haifanyiki kwa kawaida, ikifanyika, itakuwa ndani ya siku 20 za kwanza baada ya uingizaji. Inakadiriwa kwamba kati ya watu walio kwa hatari kubwa ya kupata maabukizi ya zinaa (STI) na iwe kwamba maswali ya kugundua hali ya STI imetambua nusu ya watu hao walio na STI,kiwango cha PID kitakuwa chini ya watu 2 kwa kila watu 1000 waliyoingiziwa IUD.

Ukiona dalili zinazofwata zisizo za kawaida ndani ya siku 20 baada ya kuingiziwa IUD ya shaba, kuna uwezekano kwamba umepata PID. Unapaswa kurudi mara moja kwa mtoa matibabu kwa uchunguzi zaidi na matibabu ya kufaa.
Ute wa ukeeni usio wa kawaida;
kichefuchefu na/ama kutapika
Uchungu mkali wakati wa ngono;
joto/baridi; na
maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo yako.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...