Wakati watumiaji wengine wameripoti kupata madhara baada ya uingizaji wa IUD ya shaba, nyingi kati ya madhara haya huisha mwili wako ukishazoea IUD, na hili huchukua kati ya miezi tatu hadi sita [9].
Madhara ya kawaida za IUD bila Homoni
-kutokwa matone ya damu kabla ya hedhi inayofuata (hasa ndani ya miezi michache baada ya kupata IUD);
-kutokwa damu nyingi zaidi na maumivu ya hedhi zaidi (kwa watu wengine, hizi huisha ndani ya miezi michache, lakini zikiendelea, tunapendekeza umuone daktari)
-maumivu ya mgongo; na
-anemia kwa wanawake wengine ikiwa mwanamke huyo alikuwa na damu kidogo kabla ya kuingiziwa IUD.
Matatizo nadra ya IUD ya shaba
Ikiwa mwanamke alikuwa na kisonono au klamidia wakati IUD iliingizwa, ugonywa wa uvimbe kwenye fupanyonga (PID) unaweza kutokea. Kulingana na makali ya maambukizi, PID inaweza kutibiwa kwa dawa za antibayotiki, hata ikiw
IUD inaskuma kuta za mji wa mimba.Hii inaweza kugunduliwa tu kwa kituo cha afya (kulingana na dalili maalum) na IUD inapaswa kutolewa na mtoa matibabu aliyehitimu.
IUD kuteleza na kutoka nje.Ikiwa unashuku kwamba IUD yako inakaribia kutoka au imetoka tayari, tafuta ushauri wa mtoa matibabu aliyehitimu kwa mwongozo na utunzaji unaofaa.[10] Katika hali nadra ya IUD kuingzwa ukiwa na mimba, matokeo yanaweza kuwa maambukizi, mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati [10].
Ikiwa, baada ya miezi mitatu, unahisi madhara yamezidi kiasi ulichoweza kuvumilia, unaweza itoa na utumie njia ya uzuiaji mimba tofauti. Kumbuka kwamba njia ya uzuiaji mimba ya IUD bila homoni haitoi kinga dhidi ya maambukizi ya zinaa (STI)
Nina IUD ya shaba na ninapata maumivu ya hedhi, nifanye nini?
Ni kawaida kupata maumivu ya hedhi wakati wa uingizaji na siku chache baadaye. Hili linaweza kutulizwa kwa dawa za kutuliza maumivu kama ibuprofen.Ukiwa na IUD ya shaba, inatarajiwa kwamba utakuwa na hedhi nzito zaidi, na maumivu ya hedhi kwa miezi 3-6 inayofuata. Ikiwa maumivu ya hedhi hayatapungua ndani ya miezi sita, tembelea mtoa matibabu wako mjadili chaguo zako.
Ni njia gani ya kusitisha kutokwa damu na matone ya damu baada ya uingizaji wa IUD ya shaba?
Kutokwa damu au matone ya damu baada ya uingizaji wa IUD sio dalili ya ugonjwa. Ingawa damu itaonekana nzito zaidi, sio ishara kwamba unapoteza damu nyingi. Ikiwa unashuku kwamba unapoteza damu nyingi sana, miezi saba baada ya uingizaji, zungumza na mtoa matibabu wako. Kuna uwezo utashauriwa kufanya kipimo cha kiwango cha hemoglobini na ikiwa damu iko chini au una anemia, utapewa matibabu ya kuongeza damu mwilini.
Je, IUD bila Homoni inaweza kuumiza mwenzi wangu?
Ingawa wenzi wengi wamedai kwamba wanahisi nyuzi za IUD wakati wa ngono wa uke, wengi hawatahisi chochote. Kwa vyovyote vile, nyuzi za IUD huwa laini kwa muda hadi kiwango ambacho mwezi wako hawezi huzihisi kamwe. Hatahivyo,Ikiwa mwenzi wako anasumbuliwa na nyuzi hizo, tembelea mtoa matibabu wako ili nyuzi zipunguzwe zaidi. Utashauriwa kwamba kadiri nyuzi zina katwa fupi sana, ndivyo kuzitoa itakua ngumu zaidi na huenda utahitaji mtoa matibabu aliyepata mafunzo maalum kuzitoa.
Je, IUD bila Homoni inaweza kusababisha ongezeko la uzito wa mwili?
Hapana. IUD bila homoni haisababishi upungufu au ongezeko wa uzito.Hii ni kwasababu haina homoni zozote ambazo zinajulikana kuleta mabadiliko kwa uzito wa mtu.