Jinsi ya kutoa IUD ya Shaba?

Jinsi ya kutoa IUD ya Shaba?
Jinsi ya kutoa IUD ya Shaba?

Mchakato wa kutoa IUD ya Shaba ni sawa na ule wa kutoa IUD ya homoni. Wakati IUD ya shaba ni njia ya uzuiaji mimba kwa muda mrefu inayokaa miaka 3-12, inaweza kutolewa wakati wowote ukitaka. IUD za shaba kwa kawaida zinatolewa kwa sababu mbalimbali, zikiwemo kubadilisha ile ambayo imefika tarehe ya mwisho ya matumizi, ili mtu aweze kushika mimba, na kubadilisha njia ya uzuiaji mimba kati ya sababu zingine. Utoaji wa IUD unapaswa kufanywa na mtoa matibabu aliyehitimu.
Kwenye kituo cha afya, utaombwa ulale chali, kama vile wakati wa kuchunguza uke. Mtoa matibabu atashikilia miguu yako juu kwa kutumia vifaa vya stirrups na apake mafuta ya kulainisha kwenye kifaa cha speculum ambacho kitatumika kushukia shingo ya kizazi ibaki ikiwa wazi. Huyo mtoa matibabu aliyehitimu kisha atatumia forceps kuvuta kwa utaratibu nyuzi za IUD. IUD itapinduka nyuma na kutoka nje kwa urahisi kutoka kwenye mji wa mimba kupitia shingo ya kizazi. Utaratibu huu huchukua karibu dakika mbili hadi tano. Kwa hali ambayo IUD haitelezi nje kwa urahisi, mtoa matitabu anaweza kutumia dawa kulainisha shingo ya kizazi. Kwa hali nadra kabisa, ambapo IUD ya shaba hukwama, mtoa matibabu wako ataitoa kwa upasuaji. Utatulizwa kwa dawa ili kutuliza maumivu yoyote yasiyovumilika.

Ni uchungu kiasi gani utahisi ukitolewa IUD ya Shaba?

Utahisi uchungu mdogo ukitolewa IUD kushinda ile uchungu utahisi wakati inaingizwa. Wakati wanawake wengine watahisi uchungu mdogo au kupata maumivu ya hedhi wakati wa utoaji, wengine hawatahisi chochote. Ukiwa na IUD ambayo imefika tarehe ya mwisho ya matumizi na unataka ibadilishwe, IUD ya shaba mpya inaweza ingizwa mara moja.

Ni nini itafanyika nikichelewa kutoa IUD ya Shaba ambayo muda wake wa matumizi umepita?

Mara IUD ya Shaba inafika tarehe ya mwisho ya matumizi,haitakuwa na ufanisi wa kukusaidia kuepuka hatari ya kushika mimba. Pia uko katika hatari ya kupata maambukizi ambayo inaweza kusababisha utasa. Inashauriwa uandike tarehe ya uingizaji na ya utoaji wa IUD au uombe mtoa matibabu akukumbushe wakati siku ya utoaji wa IUD yako inakaribia.

Je, naweza kutoa IUD ya Shaba mwenyewe?

Ingawa kuna makala kuhusu wanawake ambao wamefaulu kujitolea IUD zao, hakuna utafiti au miongozo ya kimatibabu ya kutosha yanayounga mkono hili wazo. Tunapendekeza kwamba IUD yako itolewe na mtoa matibabu. Hii itaifanya iwe rahisi kutatua matatizo yoyote ya utojai yanayoweza kutokea na pia kukupa nafasi ya kujadiliana chaguo ulizonazo za njia za uzuiaji mimba baada ya kutoa hii IUD. Ikiwa unatoa IUD ili upate mimba, pia utapata fursa ya kupokea ushauri kuhusu mimba wakati wa miadi hio.

Mwili wangu umeiondoa IUD bila Homoni. Nifanye nini?

Kutoka kwa IUD kunawezekana kwa asilimia 2-10 ya wanawake ndani ya mwaka wa kwanza baada ya uingizaji. Utafiti ulioendeshwa na Anthony na Wenzake, unaonyesha kwamba kutoka kwa IUD kunawezekana kwa wanawake ambao:

Hawajawahi kushika mimba;
Ni vijana (umri chini ya miaka 20);
Wana historia ya kuwa na hedhi nzito ;
Waliwekewa IUD punde baada ya kujifungua au mimba ilitolewa wakati wa trimesta ya pili;

Wakati mwingine, IUD kusonga kidogo kutoka eneo lake inasababishwa na IUD kusonga na kubadilisha eneo au isonge hadi sehemu ya chini ya mji wa mimba na ianze kuteleza nje. IUD kubadilisha eneo inaweza kuwa lilifanyika wakati wa kuingizwa au linaweza kuhusiana na umbo la mji wa mimba kama vile pembe, ukubwa, au kuwepo na hali kama uvimbe (fibroids) ambazo zinaweza kubadilisha umbo. Kwa wanawake ambao IUD ilitoka awali, kuna uwezekano wa asilimia 20-30 kwamba IUD ya pili pia itatoka. Ikiwa IUD yako itasonga kutoka eneo lake, inapaswa kutolewa na mtoa matibabu wako.

Mara iko nje, unaweza kujadiliana na mtoa matibabu wako kuhusu uwezo wa kuingiza ingine mpya mara moja au kubadilisha na kutumia njia nyingine ya uzuiaji mimba.

Je ninaweza kushika mimba haraka kiasi gani baada ya kutoa IUD ya Shaba?

Urutibisho wa uzazi kwa kawaida utarudi punde baada ya IUD ya Shaba kutolewa. Kwahivyo, unapaswa kuweza kushika mimba wakati wako wa kupevuka kwa yai inayofuata.Ikiwa haujaribu kushika mimba unapaswa kuweka IUD nyingine pahali pa ile imetolewa au utumie njia ingine ya uzuiaji mimba punde IUD ya shaba inatoka yenyewe au inatolewa.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...