IUD bila homoni ni njia ya uzuiaji mimba salama na yenye ufanisi kwa wanawake wengi. Hata hivyo, huenda haitafaa watu walio na hali fulani za kiafya ikiwemo mzio wa shaba. Kwa hivyo ni muhimu kumueleza mtoa matibabu wako hali yoyote ya kiafya ulionayo au dawa unazotumia wakati wa kupima ikiwa IUD ya shaba itakufaa.
Matumizi ya IUD ya shaba haipendekezwi ikiwa;
-unaugua Wilson’s disease [13];
-Una mzio wa shaba;
-unatokwa damu kwenye uke kwa njia isiyo elezeka (daktari wako atahitaji kuchunguza chanzo cha hili kabla uingiziwe IUD);
-una hali ya magonjwa ya uke kama vile kifua kikuu ya fupanyonga au saratani ya uke;
-umekuwa na maambukizo ya viuongo vya kizazi (mji wa mimba) baada ya kujifungua au kutoa mimba ndani ya miezi tatu iliyopita (mara imetibiwa, daktari atakuchunguza tena ili kubaini ikiwa uko tayari kwa uingizaji wa IUD);
-una uvimbe kwenye mji wa mimba (fibroids); na
-una saratani wa mji wa mimba au shingo ya kizazi.
Ikiwa una hali zozote zilizotajwa hapo juu, tafadhali muone mtoa matibabu aliyehitimu. Utashauriwa kuhusu njia bora zaidi ya uzuiaji mimba itakayokufaa.