Tembe mchanganyo ni nini?
Tembe mchanganyo, ambayo inajulikana kwa kawaida kamba ‘tembe ya kudhibiti mimba”” au ‘tembe”” ni kidonge kidogo na inakuja ikiwa imewekwa kwa pakiti ya kila mwezi. Watu wengine huiita “”njia ya mdomo ya kuzuia mimba”” Unaimeza mara moja kwa siku, saa sawa kila siku. Kuna aina nyingi za tembe zinazopatikana, na pia aina mpya zinazidi kuongezwa kwenye soko. Tembe mchanganyo ina vipimo vidogo vya homoni bandia vya estrojeni na projestini, zinazofanana na homoni estrojeni na projestini ambazo kiasili zinapatikana kwenye mwili wa mwanamke.
Tembe mchanganyo hufanya aje kazi?
Tembe inafanya kwa:
1. kuzuia kupevuka kwa yai (yai kuwachiliwa kutoka kwenye ovari);homoni zinazuia ovari zako kuwachilia yai.
2. Kufanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito; hii hufanya iwe ngumu kwa manii kuingia kwenye mji wa mimba kurutubisha yai.
3. Kufanya bitana ya mji wa mimba kuwa nyebamba; hii huzuia yai lililorutubishwa kujipandikiza kwenye tumbo la uzazi.
Ufanisi
Uwezo wa kuzuia mimba hulingana na mtumiaji. Una uwezo wa juu wa kushika mimba ukichelewa kuanza kutumia pakiti mpya kwa siku tatu au zaidi au usipomeza tembe tatu au zaidi wakati wa kwanza au wa mwisho wa pakiti ya tembe.
Tembe zikitumika inavyofaa-kumaanisha kwamba hakuna siku umekosa kumeza tembe, tembe zimeanza kutumika tena kwa saa (baada ya wiki ya tembe bila homoni/ au wiki bila tembe), na njia ya ziada ya uzuiaji mimba inatumika inapohitajika-tembe inaweza kuwa na ufanisi wa kuzuia mimba wa asilimia 93. Kwa hali ambapo tembe za homoni zinatumika mfululizo, bila kuwacha matumizi kwa siku saba, tembe inaweza kufikia ufanisi wa asilimia 99 kwa kuzuia mimba.
Ni kwa njia gani tembe mchanganyo inatofautiana na tembe yenye projestini pekee?
Tofauti na tembe yenye projestini pekee ambayo ina homoni moja bandia (projestini), tembe mchanganyo huwa na homoni mbili bandia (estrojeni na projestini).
Tembe mchanganyo inapatikana kwa chapa tofauti na inakuja kwa pakiti yenye tembe za siku 21 au siku 28. Pakiti ya kawaida ya tembe mchanganyo ya siku 28, ina tembe zenye homoni za kutumika wiki tatu, na tembe bila homoni za kutumika wiki moja, ingawa kuna zingine ambazo zina tembe bila homoni za kutumika kwa siku chache (siku 24 ya tembe zenye homoni/ na siku 4 za tembe bila homoni). Utaona kwamba tembe hizi zina rangi tofauti. Ni kwasababu tembe hizi hazina homoni. Utatumia tembe bila homoni wakati unangoja hedhi yako kila mwezi. Utapata kipeperushi cha maelekezo ndani ya pakiti kila mara unanunua pakiti ya tembe. Soma maelekezo kila mara kwa makini na hakikisha kwamba umeelewa unachohitaji kufanya iwapo utakosa kumeza tembe au utahisi kichefuchefu [1].
Tembe zingine zitakupa hedhi kila mwezi, na zingine zitafanya hedhi ije mara moja kila miezi tatu,na zingine zitafanya ukose hedhi mwaka mzima. Pia unaweza kuchagua kukosa hedhi kwa kutumia tembe zenye homoni pekee za karibu chapa yoyote. Kwa vile kuna aina nyingi za tembe zinapatikana sokoni, na kupata inayokufaa inaweza kukuwa ngumu, mtoa matibabu ama mfanyakazi wa afya ya jamii aliyehitimu anaweza kukusaidia kuamua itakayokufaa [2].