Jinsi ya kutumia tembe za kudhibiti uzazi

Jinsi ya kutumia tembe za kudhibiti uzazi
Jinsi ya kutumia tembe za kudhibiti uzazi

Tembe za kudhibiti uzazi huanza kufanya kazi lini?

Kitu cha kwanza unapaswa kujua ni kwamba wakati bora wa kuanza kutumia tembe ni siku ya kwanza ya hedhi yako. Hii ni kwasababu unapata kinga mara hio hio dhidi ya hatari ya kushika mimba. Hata hivyo, ni sawa kuanza kutumia tembe wakati wowote mwingine, tofauti tu ni utahitajika kutumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba, kama vile kondomu, kwa siku saba za kwanza.

Je, unapaswa kumeza tembe mchanganyo saa sawa kila siku?

Ili kupata kinga ya juu zaidi kutoka kwa tembe mchanganyo,inapendekezwa umeze tembe kila siku kwa saa sawa, hata iwe nini, na uanze pakiti mpya kwa saa. Ingawa tembe inaweza kubaki na ufanisi hata ukizimeza saa tofauti kwa siku tofauti, kuzimeza saa sawa hupunguza madhara na hukusaidia kukumbuka kumeza tembe. Tembe yoyote iliyosahaulikwa inapaswa kumezwa haraka iwezekanavyo.Kukosa kumeza tembe inaongeza hatari ya kushika mimba na inafanya madhara ziwe mbaya zaidi [3]. Ikiwa kuna uwezo wa juu kwamba utasahau kumeza tembe, unashauriwa kuweka king’ora cha kukukumbusha au uweke saa ya kumeza tembe iambatane na saa ya shughuli ya kila siku, kama, kupiga meno mswaki [4]

Ninapaswa kumeza tembe mchanganyo kwa saa sawa kila siku?

Tembe huhitaji nidhamu. Unahitaji kukumbuka kumeza tembe kwa saa sawa kila siku. Usipoimeza kwa saa sawa kila siku, haitafanya kazi vizuri sana.

Kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kutumia tembe:

1. Chaguo ya kupata hedhi inayotabirika

Chaguo hii ni kwa wale wangependa kupata hedhi kila mwezi. Ikiwa unatumia pakiti ya siku 28, tumia tembe za homoni siku 21 alafu hizo tembe saba bila homoni. Baada ya siku saba, anza kutumia pakiti mpya ya tembe. Ikiwa unatumia pakiti ya siku 21, tumia tembe za homoni kwa siku 21 kisha chukua muda wa mapumziko wa siku saba-sio zaidi-kisha anza kutumia tembe kutoka kwa pakiti mpya.
Utapata hedhi wakati unatumia tembe saba bila homoni au wakati wa mapumziko ikiwa unatumia pakiti ya siku 21. Tafadhali kumbuka kwamba wakati mwingine hedhi itakuja ikiwa imechelewa kidogo. Pia inaweza kuwa nyepesi, yenye maumivu ya hedhi kidogo ikilinganishwa na hedhi ya kawaida. Kwa njia zote mbili, utapata kinga dhidi ya mimba ndani ya hizo siku saba, bora umetumia tembe kwa njia sahihi na uanze pakiti ya kufuata kwa wakati. Lazima uanze pakiti ya kufuata baada ya siku saba,hata ikiwa unatokwa damu au la.
Tembe mchanganyo haitakukinga dhidi ya mimba ikiwa utasahau kumeza tembe mbili au zaidi ndani ya wiki moja.

2. Chaguo ya hedhi isiyotabirika.

Chaguo hii ni kwa wale wanataka kupata hedhi mara moja baada ya muda. Ili iwe hivi, unapaswa kutumia tembe za homoni mfululizo, kila siku, na uepuke kutumia tembe saba bila homoni kwa miezi nyingi. Unaweza kutumia tembe saba bila homoni wakati wowote unataka kupata hedhi.

3. Chaguo ya kutopata hedhi.

Hii chaguo ni kwa wale wanataka kuepuka kupata hedhi kabisa. Ili iwe hivi,tumia tembe zenye homoni mfululizo, kila siku, na usitumie tembe bila homoni au uchukue muda wa mapumziko kamwe. Hii iinaweza kuwa na maana kwamba unatumie tembe zilizo kwenye pakiti ya siku 21 bila kuwacha.
Kwa chaguo hii, unakingwa dhidi ya mimba isipokuwa usahau kumeza zaidi ya tembe nane mfululizo. Unaweza kufanya hivi kwa pakiti mingi zenye tembe za homoni unavyotaka, na pia una chaguo ya kumeza tembe bila homoni ili upate hedhi wakati wowote unapotaka.
Kwa mbinu hii, unaweza kutokwa na damu au matone ya damu mwanzoni kwa hali isiyotabirika, lakini hii huisha kwa muda.[5]
Kuna aina nyingi ya tembe zinapatikana, na inaweza kufanya uchanganyikiwe. Mtoa matibabu au mfanyakazi wa afya ya jamii aliyehitimu anaweza kukusaidia kuchagua tembe itakayokufaa.

Nini itafanyika nikikosa kumeza tembe?

Ukikosa kumeza tembe moja au mbili, meza tembe ya homoni haraka iwezekanavyo. Ukimeza tembe inayofwata hadi saa 48 baada ya ile ulimeza ya mwisho,unaweza kutokwa damu kwa hali isiyotabirika.

Ikiwa nilikosa kumeza tembe moja ya kudhibiti uzazi, je nina weza kumeza mbili kwa siku moja?

Ikiwa utakosa kumeza tembe na ukumbuke baada ya saa yako ya kila siku ya kumeza tembe kupita, unaweza kumeza tembe mbili ndani ya siku moja, bora uzimeze ukiwacha saa 10 kati yao. Ukimeza tembe ingine kabla saa 10 zipite, unaweza kupata kichefuchefu na kukusababisha kutapika [6].

Na ikiwa nilitapika baada ya kumeza tembe ya kudhibiti uzazi?

Ukitapika ndani ya saa mbili baada ya kumeza tembe, meza tembe ingine, kisha endelea kumeza tembe kama kawaida.

Kuna uwezekano gani wa kushika mimba ikiwa ninameza tembe za kudhibiti uzazi na nikatumia antibayotiki?

Antibayotiki moja pekee inayojulikana kupunguza ufanisi wa tembe za homoni za kudhibiti uzazi ikiwemo tembe mchanganyo, ni Rifampin. Dawa hii ambayo inatumika hasa kutibu Kifua kikuu, inavuruga homoni ya estrojini na kupunguza ufanisi wake wa kuzuia mimba. Ikiwa unahitaji kutumia Rifampin, ongea na mtoa matibabu wako kuhusu kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba kipindi hicho,

Je ninaweza kutumia tembe mchanganyo kama njia dharura ya uzuiaji mimba?

Ndio. Tembe mchanganyo, ikitumika kwa dozi za juu, inaweza kufanya kazi kama njia dharura ya uzuiaji mimba. Hii lazima ifanyike ndani ya siku tano baada ya kufanya ngono bila kinga. Ikiwa imepita saa 24 baada ya kumeza tembe yako ya mwisho, unapaswa kutumia njia ziada ya uzuiaji mimba kama kondomu kwa siku saba zinazofuata.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...