Madhara ya tembe mchanganyo

Madhara ya tembe mchanganyo
Madhara ya tembe mchanganyo

Madhara sio ishara ya ugonjwa na ingawa ni kawaida, wanawake wengine hawapati madhara yoyote kamwe. Madhara yakitokea, kwa kawaida yanapungua au kuisha ndani ya miezi michache za kwanza za matumizi ya tembe. Madhara yanayoripotiwa sana yanajumuisha:
-Mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi, kama vile, ziwe ambazo hazitabiriki, zikuje mara chache, ziwe nyepesi au zije siku chache, au zipote kabisa (ukitokwa damu nyepesi kati ya hedhi ya mwisho na inayofuata, usiwe na wasiwasi. Hali hii inatarajiwa kuisha wakati utamaliza pakiti ya tatu, lakini ikiwa haitaisha, unapaswa kumwambia daktari wako);
Kuumwa kichwa;
kizunguzungu;
kutokwa matone ya damu;
matiti chungu;
mabadiliko kwenye uzani;
kuisha au kuongezeka kwa chunusi;
mabadiliko kwa tamaa ya ngono;
mabadiliko ya hisia; na
kichefuchefu (kuepuka kichefuchefu, meza tembe pamoja na chakula au wakati wa kulala)
Tembe zingine zinaweza kuongeza shinikizo la damu. Wale ambao wanatumia tembe wanashauriwa kupima presha kila miezi michache. Ikiwa ongezeko lililo sababishwa na tembe litakuwa juu sana, ni vizuri uwache matumizi ya njia hii ya uzuiaji mimba. kwa kawaida presha itarudi chini unapowacha kutumia tembe [8].

Matatizo za tembe mchanganyo

Nadra sana

Wanawake wanaotumia tembe wana hatari ya juu kidogo ya kupata tatizo la damu kuganda (thrombosis). Damu iliyoganda inaweza kuziba mishipa, hali ambayo inaweza kusababisha damu kuganda kwenye mishipa ya ndani (deep vein thromosis) au damu igande kwenye ateri ndani ya mapafu (pulmonary embolisms) na mwishowe isababishe mshtuko wa moyo au kiharusi.Hii ikifanyika, itafanyika ndani ya mwaka wa kwanza wa kutumia tembe.
Unapaswa kuenda kumwona daktari ikiwa utaona yafuatayo;
-Kuzirai au kuzimia bila sababu;
-kupata matatizo kupumua;
-mguu kufura na iwe na maumivu;
-hisia ya kufa ganzi au ya udhaifu kwenye mkono au mguu;
-matatizo ya ghafla kuongea au kuona;
-kukohoa damu;
-maumivu kwenye kifua, hasa ikiwa unahisi uchungu wakati unavuta hewa ndani; na
-maumivu makali ya tumbo.
Dalili hizi zinaweza kusababishwa na damu kuganda.

Nadra kabisa

Kuharusi.
Mshtuko wa moyo.
Ikiwa, baada ya miezi mitatu, unahisi kwamba madhara yamezidi kiasi unaweza kuvumilia, tumia njia tofauti ya uzuiaji mimba na ubaki una kinga. Kondomu zinakupa kinga nzuri wakati unatafuta njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa. Kumbuka kwamba tembe machanganyo haikukingi dhidi ya mangonjwa ya zinaa.

Je nina paswa kukuwa na wasiwasi kuhusu damu kuganda?

Hatari ya damu kuganda wakati unatumia tembe iko chini sana. Kuna hatari hata ya chini zaidi ya kifo. Hali zingine za kimaunbile au kiafya zinaweza kuongeza hatari ya kuganda damu hata hivyo. Ukiwa na hoistoria ya damu kuganda, au una wasiwasi kuhusu damu kuganda, ongea na mtoa matibabu wako ili kubaini ikiwa tembe itakufaa vyema.

Je ni kawaida kutokwa matone ya damu wakati unatumia tembe mchanganyo?

Matone ya damu ni madhara ya kawaida ya tembe mchanganyo. Hii hufanyika kwa sababu kadhaa. Ikiwa unatumia tembe bila kuwacha, utapata kile kinajulikana kama damu ya ‘mafanikio’ (breakthrough bleeding). Hii huonekana kama matone ya damu kidogo au kwa hali zingine kutokwa damu nzito wakati hautaraji hedhi yako. Hii sio dalili ya afya mbaya. Pia haimanishi kwamba njia ya uzuiaji mimba unayotumia haina ufanisi.
Je, ni salama kutumia tembe mchanganyo kwa miaka mingi bila kuwacha?
Ndio. Ikitumika kwa njia inayotabirika, tembe mchanganyo inaweza kukukinga dhidi ya mimba kwa miaka kadhaa bila wewe kuhitajika kuwacha kuzitumia kwa muda. Hakuna ushaidi kwamba kuwacha matumizi ya tembe kwa muda inahitajika. Kuwacha matumizi kwa muda ina hatari zaidi kwasababu unaweza kushika mimba ndani ya kipindi hicho.

Na ikiwa ninahara baada ya kumeza tembe ya kudhibiti mimba?

Njia za uzuiaji mimba zenye homoni, ikiwemo tembe mchanganyo, zinaweza kusumbua tumbo ya mtu. Hii inaweza kusababisha kuhara. Ingawa kuhara haita athiri ufanisi wa tembe mchanganyo, kuhara kupindukia (kuhara majimaji mara 6-8 ndani ya saa 24) inaweza kumanisha kwamba tembe uliomeza ya mwisho haija nyonywa mwilini. Ikiwa unahara kupindukia, endelea kumeza tembe zako kama kawaida. Zaidi ya hio, tumia njia ya ziada kama kondomu kwa kipindi unahara na siku mbili baada ya kuhara kuisha.

Je tembe ya kudhibiti mimba ni njia ya uzuiaji mimba ambayo haiharibu mazingira?

Ingawa homoni zingine zitaingia kwenye mazingira kupitia mkojo wa mwanamkwe, viwango vyake ni vidogo kushinda vyanzo vingine vya estrojeni ndani ya mazingira. Kwa mfano, estrojeni kutoka kwenye viwanda; dawa za kuuwa wadudu;mbolea na dawa za wanyama zinaingia kwenye mazingira kwa viwango vya juu vikilinganishwa na estrojeni inayopita kwenye mkojo wa mwanamke.
Ikiwa una wasiwasi kuhusu kuongeza kiwango chochote cha homoni ndani ya mwili wako au ndani ya mazingira, kuna njia zingine za uzuiaji mimba unaweza kuchagua. IUD za shaba na kondomu za mpira wa asili ni chaguo bora kwako. Cha muhimu zaidi ni kwamba unatumia njia ya uzuiaji mimba itakayo kusaidia kuzuia mimba.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Pete ya Kudhibiti Uzazi

Hormonal

Hiyo ni nini?
Pete ya uke ni pete ndogo, inayopinduka ambayo inaingizwa ndani ya uke kama njia ya kuzuia mimba.
Matokeo mazuri
  • Ina ufanisi wa asilimia 93 hadi 99.
  • Faida
    • Inaweza kuwa na matokeo ya hedhi inayotabirika, yenye maumivu kidogo, na nyepesi.
    • Ina dozi ya chini ya homoni ikilinganishwa na njia zingine za uzuiaji mimba zenye homoni.
    • Haicheleweshi uwezo wa kupata mimba baada ya kuwacha kuitumia.
    Hasara
    • Inahitaji utunzaji wa mara kwa mara kwani lazima uibadilishe kwa saa, mara moja kwa mwezi.
    • Haitoi kinga kwa muda mrefu, na ina ufanisi tu kwa matumizi ya kila siku. Inavaliwa kwa wiki tatu,ikifuatwa na wiki moja bila pete.
    • Athari ya kawaida ni kutokwa na damu isiyotabirika kwa miezi michache ya kwanza, na kisha kutokwa damu nyepesi inayotabirika kunawezekana.
    • Athari zingine zinajumuisha maumivu ya kichwa, kichefuchefu, hisia ya tumbo kujaa, maumivu ya matiti, mabadiliko ya uzito wa mwili na maambukizi kwenye uke .
    Kiraka

    Hormonal

    Kiraka cha uzuiaji mimba ni kitu chembamba, chenye umbo wa mraba cha sentimita 5 kinachofanana na Band-Aid na kilichobeba homoni za projestini na estrojeni. Kinabandikwa kwa mwili ili kuzuia mimba.
  • Kina ufanisi wa asilimia 93-99.
    • Kinaweza kuwa na matokeo ya hedhi inayotabirika zaidi, nyepesi na iliyo na maumivu kidogo.
    • Kinaendelea kuwa na ufanisi hata unapotapika au kuhara.
    • Hakicheleweshi uwezo wa kupata mimba baada ya kuwacha kukitumia.
    • Sio rahisi kukificha kwasababu kinaweza kuonekana katika mwili wako.
    • Kinahitaji utunzaji wa kila mara. Kiraka kipya kinabandikwa kila wiki kwa wiki tatu,ikifuatwa na wiki moja bila kiraka.
    • Haitoi kinga ya muda mrefu, na ina ufanisi tu ikiwa imetumiwa ipasavyo kila mwezi.
    • Athari ya kawaida ni kutokwa na damu isiyotabirika kwa miezi michache ya kwanza, na kisha kutokwa damu nyepesi inayotabirika kunawezekana.
    • Athari zingine ni uwezekano wa ngozi kuwasha,kichefuchefu, maumivu ya kichwa, ulaini wa matiti na maambukizi kwenye uke. Athari hazidhuru na kwa kawaida zitaisha baada ya miezi michache.
    Njia za dharura za uzuiaji mimba tembe za Asubuhi ya kufuata

    Hormonal

    Tembe ya dharura ya kuzuia mimba inatumiwa kuzuia mimba baada ya ngono isiyo salama.
  • Ina ufanisi wa asilimia 99.
    • Ni salama kwa wanawake wote, ikujumuisha wale ambao hawawezi kutumia njia za kawaida za uzuiaji mimba zenye homoni.
    • Hauhitaji maagizo ya daktari au ushauri wa matibabu ili kuipata.
    • Haicheleweshi kurudi kwa rutuba.
    • Sio rahisi kukificha. Inaweza kupatikana ndani ya mkoba wako.
    • Haitoi kinga ya muda mrefu. Inatoa kinga ya mara moja na ina ufanisi tu inapochukuliwa ndani ya siku tano baada ya kufanya ngono bila kinga.
    • Inaweza kusababisha kichefuchefu na kutapika, kutokwa na damu kwa njia isiyotabirika ukeni, na uchovu. Athari hazidhuru.
    • Haipendekezwi kutumiwa kama njia ya uzuiaji mimba ya kila siku.
    Tembe mchanganyo ya uzuiaji mimba

    Hormonal

    Tembe Mchanganyo ya kuzuia mimba ni tembe ndogo yenye dozi ya kila siku iliyo na homoni mchanganyo, iliyowekwa kwenye kifurishi cha kila mwezi, ili kuzuia mimba.
  • ina ufanisi wa asilimia 93 hadi 99.
    • Inapatikana kwa urahisi (haihitaji agizo la daktari).
    • Inakupa udhibiti kuhusu lini kupata hedhi.
    • Inaweza kupunguza maumivu wakati wa kupevuka kwa yai, maumivu ya hedhi na dalili zinazokuwepo kabla ya hedhi (PMS).
    • Inatoa kinga kwa muda mrefu, lakini ina ufanisi tu kwa matumizi ya kila siku.
    • Ni ngumu kuficha na inaweza kupatikana na mwenza ambaye hataki uitumie!
    • Athari ya kawaida ni kuwepo na mabadiliko katika mtindo wa kutokwa na damu (matone ya damu kati ya hedhi, hedhi nyepesi, au kutokuwa na hedhi kabisa). Wanawake wengine wanaweza kupata maumivu ya kichwa kidogo, mabadiliko kwa uzito wa mwili na kuhara.
    • Athari hazidhuru na zitaisha baada ya miezi michache.
    Tembe yenye projestini pekee (Tembe ndogo)

    Hormonal

    Tembe yenye projestini pekee ya kuzuia mimba ni tembe ndogo yenye homoni moja ya kuzuia mimba.
  • Ina ufanisi wa asilimia 99 kwa wanawake wanaonyonyesha.
  • Ina ufanisi wa asilimia 93 kwa wanawake ambao hawanyonyeshi.
    • Ina dozi za chini za homoni (projestini pekee).
    • Inaweza kutumiwa na wanawake ambao wanavuta sigara na wana umri wa miaka zaidi ya 35.
    • Inapunguza maumivu ya kabla ya hedhi (PMS) na maumivu ya hedhi.
    • Athari inayoripotiwa kawaida ni kuwepo na mabadiliko katika mtindo wa kutokwa na damu (hedhi isiyotabirika, inayokuja siku nyingi au kutokuwa na hedhi kabisa).
    • Athari zingine zinajumuisha maumivu ya kichwa, kizunguzungu, maumivu ya tumbo, maumivu ya matiti, mabadiliko ya hisia na kichefuchefu.
    • Athari hazidhuru lakini zinaweza kusumbua.

    Our Monthly Top Articles

    Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

    Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

    Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

    Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

    Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

    Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

    Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

    Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

    Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

    Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

    Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

    Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

    Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

    Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

    Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...