Wakati matumizi ya tembe mchanganyo hayafai

Wakati matumizi ya tembe mchanganyo hayafai
Wakati matumizi ya tembe mchanganyo hayafai

Wanawake wengi wanaweza kutumia tembe ya uzuiaji mimba. Ikiwa una afya, hauvuti sigara, hauna uzito kupita kiasi, na hauna sababu zozote za kiafya za kufanya usitumie tembe, unaweza kuitumia hadi ufike komahedhi. Tembe, hata hivyo, huenda haitakufaa ikiwa:
-unavuta sigara na una umri wa miaka zaidi ya 35 (kwa wanawake ambo umri umezidi miaka 35, kuvuta sigara wakati unatumia tembe inaongeza hatari ya madhara fulani);
-una umri wa miaka zaidi ya 50 (utahitaji kujadiliana na daktari wako kuhusu chaguo zingine zitakazo faa mwili wako);
-una kipandauso (migrane) iliyo na aura ( eneo la jicho linalong’aa lililopoteza uwezo wa kuona, kabla ya maumivu makali sana ya kichwa);
-ulizaa hadi miezi sita zilizopita na unanyonyesha ( hata hivyo, unaweza kuanza kutumia tembe baada ya miezi sita au wakati maziwa ya matiti sio chakula kuu cha mtoto wako);
-umekuwa na ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya miaka 20, na imeathiri ateri, uwezo wa kuona, figo au mfumo wa neva;
-una au umewahi kuwa na saratani ya matiti;
-umekuwa na kiharusi, kuganda damu kwa mguu au mapafu zako, mshtuko wa moyo au matatizo mengine mbaya ya moyo;
-una ugonjwa wa uharibifu wa ini au maabukizi kwenye ini au uvimbe;
-una ugonjwa wa kibofu cha nyongo au unatumia dawa za kutibu kibofu cha nyongo; na
-unatumia dawa za degedege [9].
Ikiwa una dalili zozote ambazo zimetajwa hapo juu, unashauriwa kumwona mtoa matibabu aliyehitimu ili akupe mawaidha kuhusu njia za uzuiaji mimba. Utashauriwa kuhusu njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa zaidi.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...