Manufaa ya tembe mchanganyo

Manufaa ya tembe mchanganyo
Manufaa ya tembe mchanganyo

Manufaa ya kiafya

Ikitumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa na ufanisi wa asilimia 93-99 wa kinga dhidi ya hatari ya kushika mimba. [7].
Inaweza kupunguza maumivu inayoletwa na kupevuka kwa yai, maumivu ya tumbo kabla ya hedhi,na dalili zinazotokea kabla ya hedhi (PMS)
Inaweza kukupa hedhi inayotabirika, yenye maumivi iliyopungua, na ambayo ni nyepesi.
Inaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya mji wa mimba (ndani ya mji wa mimba) na saratani ya matiti kwa asilimia 50.
Inaweza kupunguza dalili za ugonjwa wa endometriosis.
Inaweza kupunguza hatari ya maambukizo kwenye fupanyonga kwasababu ute nzito unaotengenezwa na shingo ya kizazi unazuia manii na vijidudu kuingia ndani ya tumbo la uzazi.
Inaweza kutoa kinga dhidi ya uvimbe kwenye ovari.
Inapunguza dalili za ugonjwa wa polycystic ovarian syndrome (kutokwa damu isiyotabirika, chunusi, nywele nyingi sana kwenye uso au mwili).
Inaweza kutoa kinga dhidi ya magonjwa mengine ya matiti ambayo hayahusiki na saratani ya matiti (hayana athari mbaya).
Inaweza kusaidia kutoa kinga dhidi ya anemia ya upungufu wa madini ya chuma.
Tembe zingine zina manufaa ya urembo. Zinaweza kumaliza chunusi na kupunguza nywele kwenye uso na mwili.

Manufaa kwa mtindo wa maisha

Tembe ni rahisi kutumia-imeze tu na maji.
Inapatikana kwa urahisi na inaweza kununuliwa bila maagizo ya daktari kutoka kwenye duka la dawa na hospitali.
Inakupa uwezo wa kudhibiti wakati wa kupata hedhi. Tembe ni chaguo mzuri ukitaka hedhi inayotabirika. Ikiwa unapenda kupata hedhi kila mwezi au mara kwa mara bila matone ya damu, tembe inaweza kukuwa chaguo mzuri.
Pia unaweza kuruka hedhi. Tembe zingine zinaweza kufanya usipate hedhi kabisa (kwa kutomeza tembe bila homoni), ambayo ni salama kwa asilimia 100.
Hauhitaji kukatiza ngono ili kuitumia
Matumizi ya tembe inadhibitiwa kamilifu na mwanamke.
Matumizi yake yanaweza kukomeshwa saa yoyote bila usaidizi wa mtoa matibabu.
Haicheleweshi urutubisho wa uzazi. Unaweza kushika mimba siku chache baada ya kuwacha kutumia tembe. Ukiwacha kutumia tembe na hauko tayari kushika mimba, tumia njia ingine ya uzuiaji mimba.

Contraception Quiz

Not sure on the method? - Take our dynamic Contraception Quiz.
When it comes to sex, protection is as important as pleasure. But what should one do to start their safe sex journey? Answer some simple questions and based on the responses, we will recommend the next steps.

Take the quiz
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...