Kofia ya shingo ya kizazi

Kofia ya shingo ya kizazi
Kofia ya shingo ya kizazi

Kofia ya shingo ya kizazi ni nini?

Kofia ya shingo ya kizazi ni kikombe cha plastiki au ulimbo wa mpira (latex) ambacho kiko kitupu na kina nyumbulika na kinafunika shingo ya kizazi kikiki. Kinaingizwa ndani kabisa ya uke ili kuzuia manii isifike kwenye mji wa mimba. Kofia za kizazi huja kwa saizi tofauti kulingana na historia yako ya mimba.

-Kofia ya shingo ya kizazi ndogo inapendekezwa kwa wanawake ambao hawajawahi kushika mimba.
-Kofia ya shingo ya kizazi yenye ukubwa wa kati inapendekezwa kwa wanawake ambao walitoa mimba, mimba iliharibika au walizaa kupitia upasuaji.
-Kofia ya shingo ya kizazi kubwa inapendekezwa kwa wanawake ambao walizaa kwa njia ya uke.

Kuhakikisha kwamba unapata saizi inayokufaa, huenda akahitaji kupimwa na mtoa huduma za kiafya aliyehitimu. Nyenzo zingine, kama maagizo ya video, zinaweza kukufunza jinsi ya kuingiza kofia ya shingo ya uzazi.

Ili kofia ya shingo ya kizazi iwe na ufanisi, unahitaji kuiingiza kila wakati unafanya ngono.

Kofia ya shingo ya kizazi hufanya aje kazi?

Kofia ya shingo ya kizazi huwa kama kizuizi halisi kati ya manii na shingo ya kizazi (ambamo inashikiliwa kwa kunyonywa). Kofia hufanya kazi vizuri sana ikitumiwa pamoja na dawa ya kuua manii ili manii yoyote inayojaribu kuingia kwenye shingo ya kizazi inauliwa au inanyang’anywa uwezo wa kusonga kabla ipite.

Kofia ya shingo ya kizazi ina ufanisi wa kiasi gani?

Kofia ya shingo ya kizazi ina ufanisi wa kuzuia mimba mara baada ya kuingizwa. Hata hivyo, sio mojawapo ya njia za uzuiaji mimba zenye ufanisi. Inaufanisi sana ikitumiwa pamoja na dawa ya kuua manii.Ufanisi wake utategemea pia ikiwa umewahi kuzaa au bado. Ufanisi wa kofia ya kizazi uko juu kwa wanawake ambao hawajazaa.

Ikiwa umewahi kuzaa, kofia ya shingo ya kizazi ni njia ya uzuiaji mimba yenye ufanisi wa chini zaidi. Jinsi inavyotumiwa kwa kawaida na wanawake ambao tayari wamezaa, ina ufanisi wa asilimia 68. Hii inamaanisha kwamba wanawake 32 kati ya 100 wanaotumia njia hii wanashika mimba ndani ya mwaka wa kwanza ya matumizi. Kwa matumizi kamilifu, ina ufanisi wa asilimia 74 wa kuzuia mimba, inamaanisha kwamba wanawake 26 kati ya 100 wanaotumia njia hii wanashika mimba ndani ya mwaka wa kwanza ya matumizi.

Kama haujawahi kuzaa, kofia ina ufanisi wa asilimia 84 kwa matumizi ya kawaida, kumaanisha kwamba wanawake 16 kati ya 100 wanaotumia njia hii wana uwezo wa kushika mimba ndani ya mwaka wa kwanza wa kuitumia. Kwa matumizi sahihi, ina ufanisi wa asilimia 91. Hii inamaanisha kuwa ni wanawake 9 tu kati ya 100 wanaotumia njia hii ndio pengine watashika mimba ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi.

Urutubisho utarudi mara hio hio baada ya kutoa kofia ya shingo ya kizazi (2).

Ni nani anaweza kutumia kofia ya shingo ya kizazi?

-Ni chaguo nzuri kwa wanawake ambao hawawezi kutumia njia za uzuiaji mimba zenye homoni kwa sababu za kimatibabu au mapendeleo.
-Wenza ambao hawajali hatari ya mimba.
-Wanawake ambao hawashiriki ngono mara kwa mara na wanahaji tu kinga ya mara moja moja.
-Wanawake ambao wanahitaji njia ya ziada ya uzuiaji mimba kwasababu wamekosa kutumia tembe, wanangoja njia ingine ya uzuiaji mimba ianze kufanya kazi au wanatumia dawa ambayo pengine inazuia njia yao ya kawaida ya uzuiaji mimba kufanya kazi.
-Wanawake ambao zaidi ya wiki sita imepita tangu wazae. Kofia ya shingo ya kizazi huenda itapungua ufanisi punde baada ya kuzaa. Wiki sita baada ya kufingiua, shingo ya kizazi itakua imerudi kwa ukubwa wake wa kawaida na itakuwa salama kutumia kofia. Haitaathiri kunyonya au kukuwa kwa mtoto mchanga.Utahitaji kupimwa tena baada ya kujifungua kabla upate kofia ingine.
-Wanawake wanaonyonyesha walio na mzio wa ulimbo wa mpira (latex).

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...