Kuingiza kofia ya shingo ya kizazi ni sawa na kuingiza dayaframu. Unaweza kuingiza dayaframu wakati wowote hadi saa 42 kabla ya kufanya ngono.
-Kwanza, nawa mikono kwa sabuni na maji, na uyawache yakauke yenyewe kwa upepo.
-Angalia kofia yako ya shingo ya kizazi kama ina matundu na sehemu dhaifu. Ni sawa kuijaza maji ili uichunguze-ikiwa ina vuja, basi kuna tundu.
-Weka milimita 1-2 ya dawa ya kuua manii kwenye sehemu yenye umbo wa kuba na kwenye mdomo wake pia.
-Ipindue sehemu iliyo na uzi ya kuitoa na uweke milimita 2-3 ingine ndani, sehemu kati ya mdomo na mahali pa umbo wa kuba.
-Iwe umeketi au umesimama, panua miguu yako. Ingiza vidole vya shahada na kati ndani ya uke wako. Tafuta shingo ya kizazi ili ujue ni wapi pa kuweka kofia. Tenganisha midomo za nje za uke kwa mkono mmoja.Tumia mkono mwingine kufinya midomo ya kofia pamoja,ingiza kofia ndani, upande wenye umbo wa kuba ukiwa chini, na upande wa mdomo mrefu kwanza.
-Songesha chini ikielekea kwenye mkundu,kisha juu hadi kwenye shingo ya kizazi. Hakikisha kuwa shingo ya kizazi imefunikwa yote. Finya sehemu yenye umbo wa kuba kwa upole ili kufyonza na kuifungua kofia (3).
Ili kofia kiwe na ufanisi, utahitaji kuiwacha ndani kwa saa 6 baada ya ngono.Ikiwa utafanya gono zaidi ya mara moja, angalia ikiwa kofia imekaa vizuri, na uweke tena dawa ya kuua manii kabla ya kila tendo la ngono. Hauhitaji kutoa kofia wakati unaongeza dawa ya kuua manii.
Usiwache kofia ndani kwa zaidi ya saa 48. Kuiwacha ndani zaidi ya saa 48 kunaweza kusababisha madhara ya sumu inayoletwa na bakteria kuwemo mwilini.Inaweza pia kusababisha kutokwa mchozo wa ukeni na harufu mbaya.
Epuka kutumia kofia ya shingo ya kizazi wakati wa hedhi kwasabu utakuwa katika hatari ya madhara ya sumu inayoletwa na bakteria mwilini.
Uko katika hatari ya juu ya kushika mimba ikiwa haukuingiza kofia ya shingo ya kizazi ndani ya saa mbili kabla ya kufanya ngono, haukuiwacha ndani saa sita baada ya kufanya ngono, haukuiingiza vizuri, na haukuitumia pamoja na dawa ya kuua manii, au ukigundua, wakati umeitoa, kwamba imepasuka au ina matundu. Ikiwa hali itakuwa hivi na hauko tayari kushika mimba, lazima utumie tembe za dharura za kuzuia mimba (4).