Kofia ya shingo ya kizazi haina madhara mabaya kwa mwili. Madhara ya kawaida ambayo yataisha mara umewacha kuitumia yanajumuisha
-mwasho kwenye uke au ngozi;
-maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo;
-mzio wa dawa ya kuua manii ama nyenzo za silicone ambazo hutumiwa kutengeneza kofia;
-mchozo wa ukeni ambao sio wa kawaida (hii hufanyika ikibaki ndani kwa muda sana);
– maambukizi kutokana na bakteria nyingi ukeni (bacterial vaginonosis) au maambukizi ya fangasi (candidiasis) ingawa sio kawaida na;
-madhara ya kuwepo na sumu inayoletwa na bakteria kuwemo mwilini ( kwa hali nadra mno) (7).
Mabaya ya kofia ya shingo ya kizazi
-Inahitaji jitihada kubwa. Inapaswa kuwa ndani kila wakati unafanya ngono. Kuingiza kofia ya shingo ya kizazi kunaweza kuchukua muda, na wanawake wengine hupata ugumu kufanya hio. Kwa hivyo, sio njia bora ikiwa unafanya ngono mara nyingi.
-Kofia za shingo ya kizazi huwa na ufanisi wa juu ikiwa bado haujajifungua.
-Katika maeneo mengine, unapaswa kuwa na agizo la daktari ili uipate.
-Inaweza kusukumwa kutoka mahali pake na uume mkubwa, mwanamume anaposukuma kwa nguvu, au staili fulani za ngono
-Ili kutumia njia hii ya uzuiaji mimba,unahitaji kuridhika na mwili wako. Ikiwa haupendi kuweka vidole vyako ndani ya uke wako, basi zingatia njia ingine.
-Inahitaji nidhamu ya kibinafsi na mpangilio. Unahitaji kukumbuka kuingiza kofia ya shingo ya kizazi kila wakati unafanya ngono.
-Ni ngumu kukumbuka kuitumia ikiwa ume lewa.
Je kofia ya shingo ya kizazi hulinda dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs)
Kofia ya shingo ya kizazi haitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa, lakini ikilinganishwa na Dayaframu, kofia za shingo ya kizazi huhusishwa kwa kiwango cha chini cha maambukizi kwenye njia ya mkojo.
Kutumia dawa ya kuua manii mara nyingi kunaweza kusababisha mwasho na kukuweka katika hatari ya magonjwa ya zinaa, ikiwemo VVU. Itumie pamoja na kondomu ya ndani au nje ili kupunguza uwezo wa kupata maambukizi.