Kofia za shingo ya kizazi zinapatikana ndani ya nchi zingine na zinaweza kupatikana kutoka kwa vituo vya afya mtaani, ama vituo vya kuhudumia vijana na maduka ya dawa. Hata hivyo, upatikanaji wa aina na chapa maalum hutofautiana nchi moja hadi nyingine.Uliza kuzihusu kwenye vituo vyako vya afya mtaani au tembelea ukurasa wetu wa Mbinu za uzuiaji mimba katika nchi mbalimbali kujifunza zaidi kuhusu chaguo katika nchi yako. Pia unaweza kutafuta wauzaji wa kofia ya shingo ya kizazi walio karibu na wewe kwa kutembelea ukurasa wa Huduma za mbinu za uzuiaji mimba zilizo karibu nami kwenye tovuti yetu.
Unatafuta taarifa zaidi kuhusu kofia ya shingo ya kizazi? Tembelea ukurasa wetu wa maswali yanayoulizwa mara kwa mara.