Pete ya uke ni nini?
Pete ya uke, pia inayojulikana kama, ‘Pete ya ukeni ya kuzuia mimba’, ‘Pete ya kudhibiti uzazi’ au NuvaRing, ni pete ndogo inayojikunga ambayo mwanamke anaweza kuingiza ndani ya uke kama njia ya kuzuia mimba. Ina unene wa 4mm na ina kipenyo cha 5.5cm.
Unaivaa kwa wiki 3, kisha unaitoa kwa wiki moja, kabla ya kuanza kifungu kingine.
Ufanisi wa Pete ya uke
kwa matumizi kamili, pete ya uke itazuia mimba kwa wanawake 99 kati ya 100. Kwa matumizi ya kawaida ama jinsi watu wengi huitumia, pete inazuia mimba kwa wanawake 93 kati ya 100[1].
Pete ya uke hufanya aje kazi?
Pete ya uke huwa ina estrojeni na projestini, sawa na estrojeni na projesteroni zanazopatikana kiasili kwa mwili wa mwanamke. Pete huwachilia homoni hizi mbili na zinanyonywa kwa ukuta wa uke moja kwa moja hadi ndani ya mkondo wa damu wa mwanamke.
Pete huzuia mimba kwa njia mbili: inawachilia homoni ambayo inazuia ovari kuwachilia mayai na inafanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito ili kuziba manii isifikie yai. Inakinga dhidi ya mimba kwa mwezi moja wakato moja.[2].
Aina za Pete za ukeni
Kuna aina mbili za Pete za uke za kuzuia mimba: ya tumika mara moja na ya kutumika tena.
Pete ya ukeni ya kutumika mara moja inatupwa baada ya kuitumia mara mora kwa muda wa matumizi yake. Mifano ni kama NuvaRyng na EluRyng, ambazo zinatumika kwa muda wa wiki tatu.
Pete ya kutumika tena inatumika kwa njia sawa na pete ya kutumika mara moja. Hata hivyo, mara imetolewa, baada ya kutumika wiki tatu, inaoshwa kwa maji na sabuni bila manukato, inakaushwa, na kuhifadhiwa kwa siku saba. Baada ya mapumziko ya siku saba, inaingizwa tena ukeni. Ina homoni ambazo zinaweza kufanya kazi kwa ufanisi kwa mwaka mmoja, lakini hio haimanishi kwamba haipaswi kutolewa kwa uke kwa mwaka mmoja. Baada ya kutumika kwa mwaka mmoja, inatupwa kwa njia sawa kama vile pete ya kutumika mara moja hutupwa. Mfano mzuri ni pete ya uzuiaji mimba inayoitwa Annovera.