Madhara sio ishara ya ugonjwa na baadhi yao yatapungua au kuisha ndani ya miezi ya kwanza ya matumizi ya pete. Wanawake wengine hawapati madhara yoyote kamwe. Madhara yanayoripotiwa sana yanajumuisha:
Mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi ya mtumiaji (hedhi ambazo hazitabiriki au zinazokuja mara chache, hedhi nyepesi au ziwe za siku chache zaidi, au zipote kabisa- hedhi nyepesi kati ya hedhi zako sio kitu cha kukupa wasiwasi);
- kuumwa kichwa;
- kichefuchefu na kutapika;
- tumbo kujaa
- matiti chungu
- mabadiliko kwa uzani
- kuisha au kuongezeka kwa chunusi;
- kufura kwa kifundo cha mguu kwa sababu ya uhifadhi wa maji;
- mabadiliko kwa hisia; na
- maambukizo kwenye uke (mwasho, kuwa nyekundu au kufura kwa uke);
Vitu ambavyo vinaweza kuendelea kwa muda:
- mabadiliko kwa tamaa ya ngono
- ongezeko la mchozo wa uke, kuwasha na maabukizo kwenye uke; na
- Uwezo wa ongezeko kwa shinikizo la damu. Ikiwa unatumia pete ya kuzuia mimba, unashauriwa kupima presha kila miezi michache. Ikiwa ongezeko litakalo sababishwa na pete litakuwa juu sana, ni busara kuwacha matumizi ya pete. Shinikizo la damu kwa kawaida litarudi chini ukiwacha matumizi [7].
Matatizo ya Pete ya Uke
Nadra sana
Wanawake wanaotumia pete ya kuzuia mimba wana hatari ya juu kidogo ya kupata tatizo la damu kuganda (thrombosis). Damu iliyoganda inaweza kuziba mishipa, hali ambayo inaweza kusababisha damu kuganda kwenye mishipa ya ndani (deep vein thromosis) au damu igande kwenye ateri ndani ya mapafu (pulmonary embolisms) au kwenye ateri na mwishowe isababishe mshtuko wa moyo au kiharusi.Hii kwa kawaida itafanyika ndani ya mwaka wa kwanza wa kutumia tembe.
Unapaswa kuenda kumwona daktari wako mara moja ikiwa utaona yafuatayo;
- kuumwa kichwa sana, au kipandauso;
- kupata matatizo kupumua;
- mguu kufura na iwe na maumivu;
- hisia ya kufa ganzi au ya udhaifu kwenye mkono au mguu;
- matatizo ya ghafla kuongea au kuona;
- kukohoa damu;
- maumivu kwenye kifua, hasa ikiwa unahisi uchungu wakati unavuta hewa ndani;
- maumivu makali ya tumbo; na
- Kuzirai au kuzimia bila sababu;
Dalili hizi zinaweza kuwa ishara ya damu kuganda.
Nadra kabisa
- Kiharusi
- Mshtuko wa moyo
Ikiwa, baada ya miezi mitatu, unahisi kwamba madhara yamezidi kiasi unaweza kuvumilia, tumia njia tofauti ya uzuiaji mimba na ubaki una kinga. Kondomu zinakupa kinga nzuri wakati unatafuta njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa. Kumbuka kwamba pete ya kuzuia mimba haikukingi dhidi ya mangonjwa ya zinaa.