Wanawake wengi wanaweza kutumia Pete ya Uke ya uzuiaji mimba. Ikiwa una afya, hauvuti sigara, hauna uzito kupita kiasi, na hauna sababu zozote za kiafya za kufanya usitumie pete ya uke, unaweza kuitumia hadi ufike komahedhi. Vigezo vya kuweza kutumia pete ya ukeni ni sawa na vile vya tembe mchanganyo ya uzuiaji mimba. Pete ya Uke huenda haitakufaa ikiwa:[8]:
- unavuta sigara na una umri wa miaka zaidi ya 35 (kwa wanawake ambo umri umezidi miaka 35, kuvuta sigara wakati unatumia pete inaongeza hatari ya madhara fulani-unashauriwa kujadiliana na mtoa matibabu wako kuhusu hili);
- una umri wa miaka zaidi ya 50 -jadiliana na daktari wako kuhusu chaguo zingine;
- una kipandauso mkali (migrane) iliyo na aura ( eneo la jicho linalong’aa lililopoteza uwezo wa kuona, kabla ya maumivu makali sana ya kichwa);
- ulizaa hadi miezi sita iliyopita na unanyonyesha ( unaweza kuanza kutumia pete ya uke ya kuzuia mimba baada ya miezi sita au wakati maziwa ya matiti sio chakula kuu cha mtoto wako);
- umekuwa na ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya miaka 20, na imeathiri ateri, uwezo wa kuona, figo au mfumo wa neva;
- una au umewahi kuwa na saratani ya matiti;
- umekuwa na kiharusi, kuganda damu kwa mguu au mapafu zako, mshtuko wa moyo au matatizo mengine mabaya ya moyo;
- una ugonjwa wa uharibifu wa ini au maabukizi kwenye ini au uvimbe;
- una ugonjwa wa kibofu cha nyongo au unatumia dawa za kutibu kibofu cha nyongo; na
- unatumia dawa za degedege
Ikiwa una dalili zozote ambazo zimetajwa hapo juu, tafadhali muone mtoa matibabu aliyehitimu. utapewa mawaidha kuhusu njia za uzuiaji mimba. Utashauriwa kuhusu njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa zaidi.