Manufaa ya kiafya
Kwa matumizi ya kawaida, pete ya uzuiaji mimba ina ufanisi wa asilimia 93 wa kuzuia mimba. Ikitumika sahihi, inaweza kuwa na ufanisi wa asilimia 99.
Inaweza kupunguza maumivu ya hedhi, na dalili kabla ya hedhi (PMS) na maumivu wakati wa kupevuka kwa yai.
Inaweza kukupa hedhi za kutabirika, isiyo na maumivu na nyepesi.
Pete inaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya mji wa mimba (ndani ya mji wa mimba) na saratani ya matiti kwa asilimia 50.
Inaweza kukupa kinga dhidi ya uvimbe kwenye ovari.
Inapunguza dalili za ugonjwa wa polycystic ovarian syndrome (kutokwa damu isiyotabirika, chunusi, nywele nyingi sana kwenye uso au mwili).
Inaweza kutoa kinga dhidi ya magonjwa mengine ya matiti ambayo hayahusiki na saratani ya matiti (hayana athari mbaya).
Inaweza kusaidia kutoa kinga dhidi ya anemia ya upungufu wa madini ya chuma.
Inaweza kuwa na manufaa ya urembo kama vile kusaidia kumaliza chunusi na kupunguza nywele kwenye uso na mwili.
Pete ina kiwango cha chini cha homoni ikilinganishwa na njia zingine za uzuiaji mimba zenye homoni.
Manufaa kwa mtindo wa maiasha
Ni rahisi kutumia- Ni kama kuweka tamponi- na inahitaji bidii ndogo kiasi kila mwezi. Ikiwa unaogopa sindano, au utakuwa na shida ya kukumbuka kumeza tembe kila siku, pete huenda ikawa chaguo bora kwako. Unahitaji tu kukumbuka kufanya kitu mara mbili kwa mwezi.
Inahitaji bidii wa wastani: ingiza pete, ngoja wiki tatu, toa pete, ngoja wiki moja, kisha rudia mzunguko mwingine.
Inanyambulika kwa urahisi ili kutoshea uke wowote.
Ni salama kwa wanawake wenye mzio wa ulimbo wa mpira (latex).
Ina faragha. Hakuna atakaye kuona ukiitumia jinsi watakuona ukitumia tembe.
Hauhitaji kukatiza ngono ili kuitumia.
Tofauti na tembe ya kudhibiti mimba, hauhitaji kukumbuka kuitumia.
Unaweza kuruka hedhi yako.Ikitumika mfululizo, pete inakupa chaguo ya kuruka kabisa hedhi yako, na hii ni salama kwa asilimia 100.
Haicheleweshi kurudi kwa urutubisho wa kizazi. Utaweza kushika mimba punde baada ya kutoa pete. Ikiwa hautaki kushika mimba, unapaswa kuingiza pete ingine au ujikinge kwa njia ingine ya uzuiaji mimba [6].